Pia imeagiza taasisi zote, leo na kesho kuhakiki upya vibali vyao vya kufanyia kazi nchini.
"Natoa tamko na kuelekeza kwamba nasimamisha utoaji wa hati ya kusafiri 'Passport' za jumla. Vijana wetu wanapata mikasa ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya," amesema.
Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema "Tunasimamisha hadi hapo tutakapokuwa tumeweka utaratibu uliorasmi na mzuri kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya nchi husika ambako kutakuwa na mahitaji ya aina hiyo. Mfano mzuri Kenya ilipokuwa inahitaji madaktari walitumia utaratibu uliyo rasmi kuomba madaktari hao. Kwa hiyo huo ndio utakaji wa kundi wa raia walio wengi kwa pamoja."
"Pia nazitaka taasisi zote zilizo na vibali vya kufanya shughuli zake nchini zihakiki upya kuanzia aleo na kesho itakuwa mwisho na endapo hawatafanya hivyo hatua kali zitafuatwa," amesema
No comments:
Post a Comment