Wateja 36 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure baada
ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#
Zaidi
ya simu 1,000 bado zinashandaniwa pamoja na bonasi za uhakika za intaneti!
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali
ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 36 wa promosheni ya Nyaka Nyaka
Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.
Akitangaza washindi hao wa kwanza 36 waliopatikana katika
promosheni hiyo inayoendelea kwa kipindi cha miezi mitatu, Meneja wa
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alibainisha kuwa washindi 13 wanatoka Dar
es Salaam, na wengine ni wakaazi wa mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dodoma,
Mtwara, Iringa, Mwanza na Arusha.
‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na
mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao
wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema.
Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa
Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00#
wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya
Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na haya, wateja hao pia
wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zaidi ya elfu moja zenye
uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo kila saa.
‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha
kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki. Pia sasa nitaweza kupiga picha za kazi
zangu na kuwatumia wateja kwa kasi zaidi kupitia mtandao wa Tigo 4G,’ Said
Abdallah Popote ambaye ni fundi wa kupaua nyumba na mkaazi wa Tabata, Dar es
Salaam alisema.
Advera Salum Abdallah, ambaye ni muuguzi na mkaazi wa Tegeta
alisema kuwa simu aliyoshinda itamwezesha mwanawe ambaye ni mwanafunzi wa Chuo
cha Ardhi kutafiti mambo mbali mbali ya kielimu kupitia mtandao wenye kasi ya
juu wa Tigo 4G.
“Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwa
kununua vifurushi vya data vya kuanzia TZS 1,000 kupitia menu yetu ya *147*00#
ili waweze kufaidi bonasi za papo hapo za intaneti kwa matumizi ya
mitandao ya jamii kama vile Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Vile
vile, kila kifurushi wanachonunua kitawaingiza katika droo ambapo watapata
nafasi ya kushinda mojawapo za zaidi ya simu janja 1,000 aina ya TECNO R6 yenye
uwezo wa 4G ambazo Tigo inatoa katika msimu huu,” Woinde alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya
watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments:
Post a Comment