Wakala wawili (2) washinda TZS 10 millioni na
TZS 5 millioni kila mmoja.
Nane (8) wapata TZS 3 millioni na TZS 2 millioni
kila mmoja, huku mamia wengine wakizoa zawadi na bonasi lukuki
Dar es Salaam, 14 Machi,
2018.
Kampuni inayoongoza kwa
huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania kupitia huduma yake ya Tigo
Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni ya pesa kwa utendaji wao mzuri.
Wakala RBB RBB ya Sinza,
Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka Tigo Pesa, huku Said Khatib
wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi ya pili ya TZS 5 millioni katika
promosheni iliyohusisha mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda
zawadi ya kanda katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi
kuwa uwekezaji na juhudi nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha
kutangazwa kama mojawapo wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.
Pamoja na zawadi hizio kwa
washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za TSH 3 millioni na TZS 2
millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda nchini. Pia zawadi za bonasi
zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia malengo waliowekewa katika kipindi cha
promosheni hiyo.
Mojelwa Mlinga wa Ukonga,
Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya Pwani na kujinyakulia
kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia hela alizoshinda kuboresha mtaji
wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi ya pili kitaifa katika promosheni
iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa natarajia kushinda zawadi ya kwanza
kitaifa, ila nashukuru kuwa nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.
Akizungumza katika hafla ya
kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es
Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed alisema kuwa
lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni kuwadhamini na kuwashukuru mawakala
zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini.
“Ningependa kuwapongeza
mawakala wetu kwa kazi kubw wanayofanya ya kuhakikisha kuwa huduma za kifedha
zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’ alisema.
Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za
mkononi ya pili kwa ukubwa nchini
Kampuni ya Tigo ilianza
kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu mfululizo ndiyo
kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio
kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini inayohudumia wateja zaidi
ya 11.6 milioni.
Tigo ni kampuni inayoongoza
kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa huduma bora za kipekee za sauti, SMS
na in
No comments:
Post a Comment