Mechi namba 199 ya Ligi Kuu ya
Vodacom kati ya Mbeya City na Yanga iliyopangwa kufanyika Mei 1, 2018 kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya itapangiwa tarehe nyingine.
Uamuzi wa kuipangia tarehe nyingine
ni kukidhi matakwa ya Kanuni inayotaka nafasi kati ya mechi moja na nyingine
isiwe chini ya angalau saa 72.
Kwa mujibu wa ratiba, Yanga itakuwa
na mechi dhidi ya Simba itakayofanyika Aprili 29, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA
BODI YA LIGI KUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment