Monday, March 5, 2018

MMILIKI WA GAZETI LA TANZANITE KUHOJIWA BAADA YA KUONEKANA ANATAKA KUHATARISHA AMANI KWA KUMTIBUA MANGE KIMAMBI


Tokeo la picha la GAZETI LA TANZANITE

Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas imesema  imewaita wahusika wa gazeti la Tanzanite ambalo limesambaa mitandaoni likiwa limebeba katika ukurasa wa mbele habari inayomhusu Mange Kimambi.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, Dkt Abbas amesema kuwa, amelazimika kuwaita wahusika hao ambao atakutana nao leo ili aweze kusikiliza upande wao baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu maadili ya kitaaluma ya gazeti hilo.

No comments: