Watoto kutoka vituo mbalimbali kumi vya kulelea watoto wenye
uhitaji mkoani Dodoma wakisherehekea na Mshauri
wa QNET Tanzania, Edward Mkony
|
QNET
INAUNGANA NA YATIMA JIJINI DODOMA KWA KUANDAA FUTARI KWA ZAIDI YA WATU 200
Tarehe 2 June 2019..... Dodoma.
QNET, kampuni ya biashara ya mtandao duniani, sambamba na tamaduni zake na
jitihada za kusaidia jamii, kusambaza upendo, huruma na ukaribu kwa kutoa
msaada na kuleta faraja kwa jamii nyingi zisizo na uwezo barani Afrika. Katika
zoezi ambalo lilifanyika katika nchi zote ambako kampuni hii inaendesha
shughuli zake barani Afrika, QNET sambamba na wawakilishi wake wa kujitegemea
(IRs), mawakala na wafanyakazi imeleta faraja, tumaini na tabasamu kwenye nyuso
za wengi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kampuni
ya QNET inaendeshwa na falsafa ya RYTHM - Jiinue Kusaidia Wanadamu ('Raise Yourself to Help Mankind’)
imeandaa kampeni hii ya mwaka kusaidia kuboresha maisha ya familia na watoto
wengi wasio na uwezo kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula, vinywaji
na msaada wa kifedha kwa madhumuni ya elimu na
kibinadamu.
Hafla
ya Futari Jijini Dodoma imewaleta pamoja zaidi ya watoto yatima 200 kutoka
katika wilaya kumi za mkoa huo. Pamoja na hafla hiyo ya Iftar kampuni ya QNET
imetoa zawadi za mbuzi, kilo 100 za mchele, kilo 50 za unga, kilo 25 za
maharage, kilo 25 za sukari na lita 20 za mafuta ya kula kwa kila vituo kumi
vya watoto yatima mkoani humo.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shaaban alitoa wito wa amani na kuihamasisha
jamii kuiga mfano uliofanywa na QNET katika kusherehekea mwezi mtukufu wa
Ramadhani. Sheikh Shaaban ameipongeza kampuni ya QNET kwa kutayarisha Iftar kwa
vituo vya watoto yatima Jijini Dodoma, chaguo ambayo inaunga mkono mkakati wa
serikali ya kuhamisha makao yake Jijini humo. Pia alishukuru kampuni ya QNET
kwa moyo wa msaada na ushirikiano hasa katika mwezi huu wa Ramadhan.
Akiongea
katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Mwanahamisi Mukunda
alisema ‘Tendo hili la Iftar imesaidia serikali ya mkoa katika utekelezaji wa
majukuku yake pamoja na kuwaangalia watoto yatima’.
Hafla
ya Iftar Jijini Dodoma iliudhuriwa
pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma, wawakilishi wa baraza la kislamu
Tanzania-BAKWATA, viongozi wa dini la kislamu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa
kampuni ya QNET.
Katika nchi za Senegali, Cameroon, Kenya,
Niger, Mali, Burkina Faso, Togo, Guinea, Ivory Coast na Ghana, QNET imetoa
magunia ya mchele, magaloni ya mafuta ya mboga, vinywaji baridi, vifaa vya
usafi na fedha taslimu kwa yatima, jamii za waisiliamu, vituo vya kutoa msaada
wa kielimu na ofisi ya misaada ya Imamu mkuu.
Biram
Fall, Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Afrika chini ya jangwa la Sahara, wakati
akitoa maoni kuhusu CSR ya Ramadhani ya QNET kwa mwaka huu, alisema:
"QNET imekuwa ikifanya hivi kwa miaka
mingi. Kampeni ya kutoa msaada katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan ni moja ya
njia tunazotumia kuzifikia jamii kusaidia watu. Kadri tunavyoendelea katika
biashara yetu, tunaamini katika kusambaza faraja na utoshelevu unaokuja pamoja
nao. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET.
Inawezesha watu, inaonyesha upendo kwa jamii na pia inahamasisha wafanyakazi
wetu na Wawakilishi wetu wa Kujitegemea (IRs), kadri wanavyoshiriki wao binafsi
katika kuboresha maisha ya wengine. Malengo
yetu ya kibiashara pia ni kuhusu kutengeneza fursa kwa watu, kufanya maisha ya
watu kuwa bora na kuwawezesha watu kuwasaidia waweze kuishi maisha ya
ukamilifu. Tunaita hiyo kuwa ni kuishi
kikamilifu"
Mwaka
jana, Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirika kwa jamii cha Afrika ya Kusini
kiliitunukia QNET kuwa kampuni bora ya mwaka ya kimtandao ya uwajibikaji kwa
jamii (E-Commerce CSR Company of the Year)
kwa uwajibikaji wake katika kusaidia jamii na kuleta mabadiliko bora.
No comments:
Post a Comment