·
QNET,
kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inaimarisha soko la kanda kwa kutoa bidhaa
zenye ubora wa hali ya juu na kukuza ari mpya ya ujasiriamali.
Na
mwanandishi Wetu
Mauzo ya moja kwa moja (maafuru
kama network marketing) yanakuwa kwa kasi katika eneo la kusini mwa Jangwa la Sahara
ya Afrika na hasa Afrika Mashariki, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limesababishwa
na ongezeko la idadi ya watu katika kanda hii pamoja na vijana mahiri ambao kwa
mujibu wa taarifa ya Uchambuzi wa Ongezeko la Vijana ya Taasisi ya Maendeleo ya
Afrika - sasa Afrika Mashariki ina zaidi ya 45% ya vijana kati ya watu milioni
150 walioko Kenya, Tanzania, Rwanda na Uganda.
Wengi wa vijana hawa wana elimu, kwa ujumla wana ufahamu wa teknolojia,
wepesi kufuata mienendo mipya, wana hamasa ya kuweka juhudi na fikra za ujasiriamali
- jambo ambalo ndio sifa ya awali ya mafanikio endelevu katika biashara ya
uuzaji wa moja kwa moja.
Kwa wanaoanza, mauzo ya moja kwa
moja ni wazo la biashara ya kimataifa na linaelezewa kama 'uuzaji wa bidhaa za
matumizi au huduma, kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine, mbali na maeneo
ya maduka ya kawaida'. Mtindo huu wa
mauzo una zaidi ya miaka 100 na mwanzoni kabisa ulianzia huko USA. Leo, sasa
karibu takribani watu milioni 117 wanajihusisha nayo. Kwa mujibu wa ripoti ya
mwaka 2018 ya Shirikisho la Chama cha Wauzaji wa moja kwa moja Ulimwenguni.(World Federation of Direct Selling
Association (WFDSA), mauzo ya moja kwa moja yalizalisha $190 bilioni na
karibu nusu ya mauzo yote yametoka katika masoko yanayochipukia:
Inatosheleza kusema, Afrika ina chukua chini ya 1% ya jumla
ya mauzo ya WFDSA lakini wataalamu wanakadiria kwamba soko la Afrika Mashariki
linatoa fursa ya kukua kwa wajasiriamali wanaochipukia na hata kwa wale walioajiriwa
na wana kiu ya kujipatia kipato cha nyongeza kupitia mauzo ya moja kwa moja.
Katika kanda ambayo mahitaji ya ajira rasmi yanazidi kuwa na
ushindani mkubwa na uhaba wa ajira rasmi, mauzo ya moja kwa moja yanatoa njia
mbadala za ajira tofauti na ilivyozoeleka kwa wale wanaohitaji kipato cha ziada
au mazingira haya ruhusu ajira.
Akiongea hivi karibuni
wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET
kwa kanda ya kusini mwa Jangwa la Sahara alisema "QNET imesaidia
kuwawezesha maelfu ya watuAfrika, hasa vijana, katika muongo uliopita. Tunaona ongezeko la kukubalika kwa Mauzo ya
Moja kwa Moja, na idadi ya watu zaidi ya milioni 200 katika Afrika Mashariki,
Mtindo huu ni mtindo unaobadilisha
maisha kwa wengi"
QNET inatoa aina mbalimbali
za bidhaa za afya, ustawi na mitindo ya maisha kupitia mifumo yake ya biashara
ya mitandao (e-commerce) kwa
mamilioni ya wateja katika zaidi ya nchi 100, ikiwa inasaidia watu kuishi
maisha bora, na kutoa njia mbadala ya kujipatia kipato kwa yeyote anayehitaji
kutumia fursa hii. Kampuni pia ina ofisi na
mawakala washirika katika nchi 25 duniani kote, na zaidi ya stoo 50, shughuli
za uendeshaji na maduka na wauzaji katika nchi kadhaa duniani. Sasa kwa uwepo wake imara katika Afrika
Mashariki, QNET imejidhatiti katika kuendeleza mtindo wa mauzo wa moja kwa moja
katika kanda hii.
Kwa kuongezea QNET pia
inarudisha faida yake kwa jamii. Baadhi ya wanufaikaji wa Majukumu ya Kampuni
kwa jamii ni pamoja na kituo cha kulelea yatima cha Maunga, na Kituo cha kulele
yatima cha Newlife Orphans Home ambavyo vimepokea msaada wa chakula na michango
kwa miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Biram Fall
Meneja Mkuu wa QNET katika Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara;
"QNET ina nia ya kurudisha kwa jamii, Hii ndio sababu kwa nini tumewekeza
kwa kiasi kikubwa katika miradi ya uwajibikaji endelevu ya kampuni kwa jamii
katika maeneo mbalimbali ya Afrika kupitia katika mkono wetu wa uwajibikaji kwa
jamii” alisema Fall.
QNET Ghana, kwa kupitia
RYTHM Foundation, imetoa vifaa maalumu 50 vya kusomea vitabu vya kielektroniki
(Kindle e-readers) ambavyo vina
vitabu 100 vinavyoendana na tamaduni zao kila kimoja. kwaajili ya wanafunzi wa
Nima, eneo lenye watu wa kipato cha chini zaidi ndani ya jiji wa Accra,
Ghana. Ilikuwa ni mradi uliofanyika kwa
ushirikiano na Worldreader, NGO ya
utoaji wa elimu duniani na Achievers Ghana, taasisi ya elimu kwa jamii.
QNET
pia inafanya vizuri katika udhamini wa michezo duniani. Baadhi ya ushirikiano
mkubwa wa hivi karibuni unajumuisha kuwa Wauzaji wa Moja kwa Moja wa Klabu ya
Mpira wa miguu ya Manchester City na Klabu ya mpira wa miguu kwa wanawake ya
Manchester city na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwaajili ya ligi
ya mabingwa ya Total CAF, Kombe la shirikisho la Total CAF na Total CAF Super
Cup kwa mwaka 2018 na 2019. Hapo awali washirika wakubwa walikuwa ni pamoja na
Formula One, badminton na zaidi, kutokana na imani thabiti ya kampuni kwamba
msukumo, shauku na kufanya kazi katika timu iliyopo katika michezo inaendana na
ule wa QNET.
Manufaa
Imani thabiti ya QNET kwamba hakuna kinachowezesha zaidi kwa mtu
binafsi kama uhuru wa kifedha ambao unatolewa na jitihada katika sekta ya mauzo
ya moja kwa moja, na inaamini kwamba watu wa Afrika Mashariki, pamoja na shauku
yao na fikra za ujasiriamali, watafurahia kiwango bora cha bidhaa zinazotolewa
na QNET na fursa za kibiashara kwaajili ya maendeleo binafsi.
Mauzo ya Moja kwa Moja yanaweza kuwa ni kazi ya kutosheleza kwa
wale ambao wanachagua kuchukua fursa hii kama kazi yao kuu au hata kuchukua
kama kazi ya ziada kwa sababu inatoa faida za kifedha kutegemeana na muda na
juhudi unazoweka katika kukuza biashara yako.
Kwa kuongezea, tofauti na biashara zingine za kawaida ambazo zinahitaji
mtaji mkubwa, rasilimali na hata uzoefu, biashara ya mauzo ya moja kwa moja
inatoa fursa hii ya biashara yenye gharama nafuu kwa kila mmoja anayehitaji
kuianzisha, bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu. Zaidi ya hayo, mafunzo na maelekezo ambayo
wafanyabiashara wanaoanza wanapitia (Wawakilishi wa Kujitegemea au IRs kama
ilivyo katika QNET) inawapatia ujuzi wa pekee ambao unapelekea kuwa na ujasiri,
kujitambua na hatimae ukuaji binafsi ambao unatambua utaalamu wa mtu kama
mjasiriamali aliyekamilika.
Huenda, manufaa makubwa zaidi ya mauzo ya moja kwa moja katika
masoko yanayoibukia kama Afrika Mashariki ni kwamba mtindo huu unakuwa na
athari zaidi hapa kuliko katika masoko yaliyoendelea kwa sababu ya athari za
kifedha inayoweza kuleta katika maisha ya watu - kutoa fursa za ujasiriamali
kwa wote, bila kujali ujuzi au uzoefu, hivyo hatimae kuchangia katika kupunguza
umasikini katika jamii.
Katika mizizi ya QNET kuna falsafa ya RYTHM – Raise Yourself To
Help Mankind - ambayo inaongoza jitihada zake zote, na kuendesha kampuni sio tu
kubadilisha maisha ya watu duniani kote, lakini pia kushirikiana nao katika
kupanua athari hizi.
Kama alivyosema bwana Trevor Kuna, Mkurugenzi Mtendaji wa
QNET "Tunaamini kwamba mafanikio ya
kifedha peke yake hayatoshelezi"
Ili tuweze kuleta athari, tunahitaji kuendeleza watu kuwa binadamu bora
ili waweze kutumia mafanikio yao kuchangia katika jamii zao"
Changamoto
Kama ilivyo katika biashara nyingine yoyote Sekta ya Mauzo ya Moja
kwa moja pia inakabiliana na changamoto.
Changamoto ambayo ni kubwa zaidi miongoni mwa hizi ni kuenea kwa mifumo
ya pyramid schemes inayoenda kinyume cha sheria ambayo inaonekana kama
makampuni halisi ya biashara ya moja kwa moja, ikiwa inaahidi wawekezaji kuwa
watajipatia faida nyingi kupita kiasi iwapo wataunganisha watu wengine. Ukweli ni kwamba hawa 'matapeli'
wanatengeneza taswira potofu ya Sekta ya Mauzo ya Moja kwa Moja, jambo ambalo
linatengeneza kikwazo kwa makampuni halisi kama QNET kusajili washauri wa
kibiashara kuendesha biashara zao halisi na halali. Wakati inapokabiliana na hali kama hizo,
QNET inasema inatatua tatizo kwa kuelimisha umma kuwa makini na 'matapeli' kama
hao na kuwahimiza kuthibitisha uhalali wa kampuni yeyote kufuatana na kutii
kwake kwa kanuni, taratibu na sheria zilizowekwa na bodi zinazosimamia na
mamlaka zinazohusika.
Mpaka kufikia hapa, maelezo kutoka QNET yanasema: "Kampuni
yoyote inayokuahidi njia rahisi ya kuwa tajiri inapaswa kuangaliwa kwa
tahadhari. QNET kwa mfano, ina maelezo
ya kutosha ya mapato yanayopatikana kwenye tovuti yake na vifaa vya mauzo.
Kampuni za Masoko ya mtandao zinatoa bidhaa zenye ubora au huduma tofauti na
mifumo ya pyramid schemes ambayo haina bidhaa halali au huduma. Kampuni bora ya Masoko ya mtandao huwa
inatenga kiwango kikubwa cha rasilimali kwaajili ya utafiti na uendelezaji,
kutengeneza bidhaa zenye ubora ambazo zina matumizi halisi kwa watu wakati
mifumo ya pyramids scheme huwa haifanyi hivyo"
Inaongeza: "Kampuni za masoko ya mtandano yana sera
na taratibu sahihi, pamoja na kanuni za maadili za masoko. Kamuni yoyote halisi ya masoko ya mtandao ina
lengo la kufikia ukuaji endelevu kwa kukuza utamanuni wa masoko ya
kimaadili. QNET inaweka msisitizo mkubwa
katika kanuni za maadili za utendaji kwa wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs)
na kuwapatia miongozo ya kina kuhusu masoko ya kitaalamu pamoja na sera na
taratibu".
Kusisitiza
uhalali wa mauzo ya moja kwa moja, utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na
Taasisi ya Ngazi Mbalimbali za Masoko ya India (India Multi-Level Marketing Institute) ilichunguza uendeshaji wa
aina mbalimbali kama vile Avon, Mary Kay, QNET na Tupperware na kubaini kwamba
'sio mifumo ya scheme) ya aina ya piramidi au aina nyingine yoyote.
Changamoto nyingine inayoikabili
sekta ya mauzo ya moja kwa moja ni ujuzi ambao haujaendelezwa hasa kwa wale
ambao wamechukua fursa hii hivi karibuni.
QNET inasema kwamba inatatua changamoto kwa kuweka msisitizo mkubwa sana
katika mafunzo na elimu kwa IRs. Mafunzo hayo
sio tu kamba yanaendeleza ujuzi wao wa kitaalamu lakini pia unalenga katika
ukuaji na maendeleo binafsi.
Ni wazi kwamba, kufikisha bidhaa katika maeneo ya
vijijini na maeneo ya mbali ni kikwazo kingine lakini QNET imeweza kutatua hili
kwa kuajiri IRs ambao wanatengeneza mtandao ndani ya jamii zao kwaajili ya
kurahisisha upatikanaji na pia kuwasaidia kuagiza mzigo mkubwa kwa punguzo kwa
lengo la kutoa mzigo, hivyo kuhakikisha usambazaji endelevu wa bidhaa.
Kuingia kwa QNET katika soko la kanda inaweza pia
kukabikiana na ushindani kutoka kwa kampuni ambazo tayari zilishaanzishwa za
bidhaa za reja reja na nembo za kimataifa lakini mtindo wake wa pekee wa
usambazaji utaiweka QNET tofauti na kutengeneza njia ya mafanikio.
No comments:
Post a Comment