Wateja watakaoongeza salio au kuweka
Pesa Kwenye Tigo Pesa au Kutumia huduma yoyote ya Tigo watapata nafasi ya
kushinda zawadi nono za hadi TSH milioni 50!
Dar
es Salaam, 15 Novemba 2018; Tigo
Tanzania - kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, itawezesha wateja
wake kuwa mamilionea baada ya kuzindua promosheni kubwa zaidi itakayogawa kiasi
cha TSH milioni 600 katika msimu huu
wa sikukuu.
Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu
huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea
ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna
kujiunga kwenye promosheni hii.
‘Wateja wa Tigo watakaoweka pesa kwenye
akaunti zao za Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka
yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu
watapata fursa ya kujishindia TSH milioni
1 kila siku au TSH milioni 10 kila wiki. Pia kutakuwa na zawadi kubwa za TSH milioni
15, TSH milioni 25 au TSH milioni 50 zitakazotolewa mwishoni mwa promosheni hii
ya JIGIFTISHE!’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwaambia waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Akibainisha vigezo vya ushiriki katika
promosheni hiyo ya JIGIFTISHE, James Sumari, Mkuu wa Bidhaa za Huduma za Tigo
Pesa wa Tigo alisema kuwa ili kupata fursa ya kushinda, wateja wa Tigo wanahitaji
kununua kifurushi chochote kwa njia yoyote (ikiwemo kupitia *147*00#, *148*00# au
kuongeza muda wa maongezi kwa njia ya kielektroniki, kadi au kupitia Tigo Pesa)
au kufanya miamala ya Tigo Pesa kupitia *150*01# katika msimu huu wa sikukuu.
‘‘Ni rahisi sana! Hakuna kufanya kitu
chochote maalum ili uweze kushinda. Unachohitaji kufanya ni kuendelea kutumia
huduma au kununua bidhaa za Tigo ili upate nafasi ya kuwa milionea!” Woinde alisisitiza.
Kila muamala utakaofanyika utampa mteja
nafasi moja ya kushiriki katika droo, na wateja wanaweza kutazama nafasi zao za
kushinda kwa kupiga *149*22#. Kadri unavyofanya miamala zaidi ndivyo
unavyojiongezea nafasi za kushinda.
Promosheni
hii ya JIGIFTISHE itakayojaza mifuko ya wateja na manoti na kubadilisha maisha yao
inathibitisha kuwa Tigo ndio mtandao
unaotoa huduma bora zaidi za kidigitali kwa wateja wake na kuwawezesha kufurahia
msimu huu wa sikukuuu huku wakimaliza au kuanza mwaka mpya kwa mtindo tofauti.
‘Hii ndio njia yetu ya kuwashukuru
wateja wetu wote kwa kuendelea kutumia huduma zetu bora, zenye kasi ya juu na rahisi.
Tunachukua fursa hii kuongeza tabasamu katika nyuso za wateja wetu,’ Woinde alisema.
Tayari wateja wa Tigo wanafurahia unafuu
na urahisi wa kutumia huduma bunifu za Tigo kama vile kufanya miamala ya Tigo
Pesa (kutuma na kupokea pesa ikiwemo kutoka mitandao mingine na benki), kulipia
huduma mbali mbali kama vile LUKU, kufanya manunuzi kutoka kwa wafanyabiashara
tofauti, kukamilisha malipo ya Kiserikali na pia kufurahia huduma bora za maisha
ya kidigitali kwenye mtandao mkubwa zaidi wa 4G nchini.
No comments:
Post a Comment