Meneja Uhusiano wa Zantel Rukia Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofa maalum ya mfungo wa Ramadhani jijini Dar es salaam, Ofa hiyo mpya itawapa wateja uhuru zaidi wa kuwasiliana pamoja na kuwapa taarifa muhimu kipindi cha mfungo kama nukuu za Quran pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala kufuturu na mwisho wa kula daku.
Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na
kupata taarifa muhimu kama vile nukuu mbalimbali za Koran takatifu pamoja
na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala na ujumbe wa sauti utakaoingia
kwenye simu zao
kama simu nyakati za iftar na nyakati za daku.
Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar
Mohammed Mussa alisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu
kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi
hiki cha mfungo.
“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa
mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga
mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii
itahakikisha kwamba wateja
wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia
kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.
Naye, Meneja bidhaa na huduma wa Zantel, Aneth Muga alisema
ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi
vilivyoboreshwa zaidi vya siku,wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia
nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.
“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu
zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa
Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya
Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema Muga.
Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi 2,000 mteja
atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata
dakika 1,250, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu,
jumbe za
kuwakumbusha muda wa kufuturu pamoja za kukumbusha muda wa
swala.
Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na
kuchagua namba 1 ambayo ni Ramadhani ofa na atajiunga na kifurushi
anachohitaji.
Kuhusu Zantel
Zantel ni Kampuni inyaoongoza kwa utoaji wa huduma za
mawasiliano Visiwani Zanzibar kwa miaka mingi hivi sasa ikiongoza kwa ubora
miundombinu ya mawasiliano, huduma pamoja na bidhaa.
Huduma ya kifedha ya Ezypesa ni ya kwanza nchini Tanzania
kutoa huduma za kibenki za kawaida pamoja na za kiislamu kwa ushirikiano na
benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Aidha, Zantel ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za
intaneti nchini Tanzania kupitia uwekezaji kwenye teknolojia ya fibre optic
cable ambayo inaiunganisha Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki
na duniani
umeiwezesha Kampuni hiyo kuleta mapinduzi ya haraka ya
kidigitali hapa nchini.
Aidha,Miundombinu hiyo imeiwezesha Zantel kutoa huduma za
kimataifa za sauti na data kwa jumla kwa kampuni nyingine na nchi jirani hivyo
kuchagiza ukuaji wa teknolojia ya digitali
Kwa Mawasiliano zaidi kuhusu
Zantel tembelea tovuti; www.zantel.co.tz
Rukia Mtingwa – Manager Brand and
Communication
Mobile: +255 774 55 9999
No comments:
Post a Comment