Punguzo kabambe la bei ya tiketi kwa
watakaonunua kupitia Tigo Pesa Masterpass QR
Morogoro,
Septemba 28, 2018 - Huku
nchi nzima ikisubiri kwa hamu kuanza kwa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote, mdhamini mkuu Tigo Tanzania pamoja
na waandaaji Clouds Media Group wameanza maandalizi rasmi ya tamasha hilo
litakalorindima Jumamosi hii tarehe 29 Septemba katika viwanja vya Jamhuri,
mjini Morogoro..
Akizungumza
katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Kamati ya
Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 – Viba Kama Lote, Gardner G. Habash aliwahakikishia
wote watakaohudhuria tamasha hilo usalama na mapokezi mazuri. ‘Tunawakaribisha
nyote kwenye shamrashamra za mwanzo wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama
Lote,’ Gardner alisema.
‘Tigo
inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa
kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Morogoro, tiketi zitakazonunuliwa kwa
mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000
kwa watakaonunua kwa pesa taslim,’ Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William
Mpinga alisema. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#
na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha
kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Wateja
wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila
siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za
mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni
10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya
http://tigofiesta.co.tz
na kuchagua Trivia.
‘Katika
miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii
unaotokana na tamasha la Tigo Fiesta. Bali na kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika,
pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za
biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama nitilie, vyombo vya usafiri
kama vile bodaboda, kumbi za starehe na biashara nyinginezo,’ Gardner
aliongeza.
Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la
muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu
litashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea,
Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku
kilele kikifanyika Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment