Afisa Mtendaji Mkuu wa QNET, Ms. Malou Calouza(wa kwanza kushoto) na Maofisa wa serikali ya Malaysia
wakikata utepe kuzindua rasmi kongamano
la V-Convetion lililofanyika mjini Penang, Malaysia hivi karibuni. Wengine ni
wajumbe wa Bodi wa QNET
Kampuni maarufu ya kimataifa ya mauzo ya
moja kwa moja yenye asili ya Asia, QNET imeendesha kongamano la siku tano la
kimataifa ambalo linaleta pamoja takribani wajasiriamali 13,000 kutoka maeneo
mbalimbali duniani katika kisiwa cha Penang, Malaysia Takribani wajasiriamali
wa kiafrika wenye shauku wapatao 2600
walishiriki katika kongamano la mwaka huu.
Kongamano
ambalo hufanywa mara mbili kwa mwaka la (V-Convention) ni tukio la kipekee
ambalo huleta pamoja wateja na wasambazaji wa QNET kutoka maeneo mbalimbali
duniani, washirika wake wa kibiashara, na pia maofisa wa serikali kuja kujionea
bidhaa na huduma za QNET na kuelewa vyema biashara yake.
Kongamano la
siku tano ilijumuisha mfululizo wa programu za mafunzo, hotuba za uhamasishaji,
kutambulisha bidhaa mpya za mtindo wa maisha wa QNET na matukio ya burudani.
Kivutio kikubwa mwaka huu ni QNET Carnival ambayo ilionyesha zaidi ya nembo au
lebo 30 za bidhaa za QNET katika moja ya maonyesho makubwa kuwahi kufanywa na
kampuni hiyo. Bidhaa mpya zilizozinduliwa mwaka huu ni pamoja na virutubisho
vipya kwaajili ya afya ya wanaume vinavyoitwa QAlive, na toleo lenye ukomo la
saa za kifahari kwaajili ya kumbukizi ya miaka mitano ya ushirikiano kati ya
QNET na klabu ya mpira wa miguu ya jiji la Manchester (Manchester
City Football Club). Moja kati ya dondoo zilizoshika hisia za watu ni sherehe
za mahafali ya wateja ambao wamekamilisha kozi zao kwa njia ya mtandao kupitia
qLean, bidhaa ya elimu ya QNET, ambayo ni maarufu sana miongoni mwa wateja
katika kanda ya Sahara ya Afrika.
Washiriki vile vile walipewa fursa ya
kusikiliza kutoka kwa wazungumzaji rasmi ambao wameshinda vikwazo vikubwa na
kufanikisha ndoto zao. Farouk Saad Hamad
Al-Zuman, raia wa kwanza wa Saudi Arabia kupanda mlima Everest, na Sparsh Shah,
mvulana mwenye umri wa miaka 15 raia wa marekani mwenye asili ya India aliyezaliwa
na tatizo la mifupa dhaifu (brittle bones), ambaye alipewa siku 2 za kuishi na
madaktari baada ya kuzaliwa, na sasa ni nyota katika mtandao wa Youtube kwa
mtindo wake wa kipekee wa mziki ambao anaunganisha pamoja muziki wa classical
na rap.
Bwana Koné
Doupin, Mwakilishi wa Kujitegemea anayeshiriki katika kongamano hilo la (V-Convention)
kutokea Ivory Coast alisema: "Nina
furaha sana kuwa hapa mwaka huu. Tangu
nilipojiunga na QNET miaka kumi iliyopita, sijawahi kukosa kongamano la -V
lolote kwa sababu ni fursa ya kipekee kukutana na viongozi wetu wa juu,
kujifunza kutoka kwao, kukutana na watu kutoka sehemu mbalimbali na kugundua
upekee wa bidhaa mpya. Nina shauku kubwa
ya kujaribu bidhaa mpya ya QAlive, kirutubisho kipya cha wanaume na kugundua ni
jinsi gani kinaweza kuboresha maisha yangu."
Sherehe za
ufunguzi ziliongozwa na watu mbalimbali maarufu kutoka Malayasia na Asia ya
Kusini Mashariki. Mgeni rasmi kutoka
Afrika, Bwana Cissé Ibrahim Sory vile vile alikuwepo katika sherehe za
ufunguzi, Bwana Cissé Ibrahim Sory ni Mjumbe wa Baraza la Mawaziri kutoka ofisi
ya Rais katika Jamhuri ya Guinea-Conakry.
Afisa
Mtendaji Mkuu mpya wa QNET aliyeteuliwa, Bi. Malou Caluza alisema:
"Matukio kama haya ya Kongamano (V-Convention) hutupa fursa ya kuwahudumia
wasambazaji wetu na kuwapa fursa ya kuona na kushuhudia mtindo wa Kuishi Kikamilifu
(Absolute Living) ambao inaongoza biashara yetu, Vile vile ni jukwaa bora la
kusherehekea ari ya ujasiriamali ambayo kampuni ya mauzo ya moja kwa moja kama
QNET inachochea kwa mamilioni ya watu duniani kote, kuwasaidia kuboresha maisha
yao na kuchangia katika jamii."
Akiongeza
katika hilo, Meneja Mkuu wa QNET wa kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Bwana
Biram Fall, alisema: "V-Malayasia inafuata msimu wa kongamano la QNET Expo
wa mwaka 2019 wenye mafanikio wenye jina la Kuisi Kikamilifu (Absolute Living),
linaloenda sambamba na kanuni ya kampuni ya mauzo ya moja kwa moja QNET na
falsafa yake ya RYTHM - Jiinue Uweze
Kuwasaidia Wanadamu (Raise Yourself to
Help Mankind) Kongamano la mwaka 2019 lilianzia jijini Dar es salaam,
Tanzania mwezi uliopita, kisha likahalia Kumasi, Ghana na sasa nchini Malayasia
kwaajili ya kongamano la kiulimwengu la V-Convention. Baadae nchi zingine za Afrika zitakuwa
wenyeji wa kongamano la Kuishi Kikamilifu (Absolute
living expo)."
QNET, inauza
reja reja bidhaa mbalimbali za Afya na ustawi, huduma binafsi na urembo,
sikukuu, utunzaji wa nyumba na kozi kwa njia ya mtandao miongoni mwa nyingi
zingine ambazo zinaboresha maisha ya kila siku ya wateja wake duniani kote.
QNET iliwekwa katika moja kati ya makampuni 100 makubwa na imara ya MLM (Solid Top MLM Companies) kwa mwaka 2018 na
Portal ya habari za mauzo ya moja kwa moja ya Business for Home.
Katika Afrika
Magharibi, Chama cha Ghana cha CSR (GHACEA) mwaka 2018 kiliitunukia QNET kuwa
Kampuni ya Mwaka ya Biashara ya Mtandao (E-Commerce Company of the Year.)
|
No comments:
Post a Comment