Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda (katikati) na
Meneja wa QNET, kanda kusini ya Afrika
Biram Fall (kushoto) wakikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya bidhaa za
QNET 2019 jijini humo. Kulia ni Mshauri
wa Biashara wa QNET Tanzania, Edward Mkony.
·
Maelfu
wa hudhuria maonyesho ya QNET Dar es
salaam
·
Watanzania
kunufaika na bidhaa mbalimbali pamoja na fursa za biashara
Tarehe
16 Machi 2019, Dar es Salaam: Kampuni yenye asili ya Asia ya
mauzo ya moja kwa moja QNET imeendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake
jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019.
Maonyesho yenye jina la Absolute
Living, (Kuishi kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo
ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani
kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko
mapya. Onyesho hilo pia ilikuwa kama
jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo
wake wa biashara.
Nadharia ya Absolute Living
(Kuishi kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwendendo wa kujali afya,
mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, ustawi
na elimu.
Mgeni rasmi katika hfla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul
Makonda alisema ‘Maisha yangu ni mfano wa kufanya kazi kwa bidi na
kujiamini katika kitu chochote unachokifanya. Hii ndiyo njia pekee yakuleta
mabadiliko na maendeleo kwa mtu, familia na jamii”.
Akizungumza kwenye mkutano na
vyombo vya habari Meneja Mkuu wa QNET
kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema kwamba,
"Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma kwa wateja
wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia kutatua tatizo
la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia program za
mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri mwenyewe. Kutoka katika kozi za elimu kwa njia ya mtandao
kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu kama vile Tripsavr,
mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3, virutubisho kama EDGE, na
saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina mbalimbali za kukidhi
mahitaji mbalimbali ya watu. Katika
kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu
"Absolute Living”
Zaidi ya watu elfu mbili walipata
fursa ya kuona bidhaa za mfano katika onyesho hilo na kufundishwa namna ya
matumizi ya bidhaa na faida zake kwa wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea, wataalamu wa bidhaa na
biashara walikuwepo kwaajili ya kujibu swali lolote kutoka kwa wageni ili
kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET.
Maonyesho ya Dar es salaam
yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea,
Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.
Msafara wa maonyesho utasisimama
katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24
Machi mwaka 2019.
|
No comments:
Post a Comment