·
Dar es
salaam inakuwa mwenyeji wa siku 2 za maonyesho ya Absolute Living (Kuishi
kikamilifu) ya bidhaa QNET
·
Watu
wote wanakaribishwa kuhudhuria na kuelewa bidaa za QNET, huduma na mtindo wake
wa biashara.
Tarehe
13 Machi 2019, Dar es salaam: Kampuni yenye asili ya Asia ya
mauzo ya moja kwa moja QNET itaendesha maonyesho ya bidhaa na huduma zake
jijini Dar es salaam siku ya tarehe 16 na 17 Machi 2019 katika ukumbi wa
Mlimani City kuanzia saa 4 asubuhi mpaka
saa 1 Jioni.
Maonyesho yenye jina la Absolute
Living, (Kuishi Kikamilifu) sambamba na falsafa ya bidhaa za kampuni ya mauzo
ya moja kwa moja, huwa yanafanyika kila mwaka katika nchi mbalimbali duniani
kote ikiwa na lengo la kuonyesha bidhaa zake na huduma kwenye masoko
mapya. Onyesho hilo pia linakuwa kama
jukwaa kwa wateja na wadau wengine wanaotaka kufahamu kuhusu QNET na mtindo
wake wa biashara.
Nadharia ya Absolute Living
(Kuishi Kikamilifu) inaakisi juhudi za QNET za kukuza mwenendo wa kujali afya,
mtindo wa maisha wenye uwiano sahihi, ikiwa inatilia mkazo katika Afya, Ustawi
na Elimu.
Akizungumza kwenye mkutano na
vyombo vya habari Meneja Mkuu wa Kanda
wa QNET kwa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, Biram Fall alisema
kwamba, "Tunatoa aina mbalimbali za bidhaa za kiwango cha juu na huduma
kwa wateja wetu kuwasaidia waweze kuishi maisha yenye uwiano sahihi, na pia
kutatua tatizo la msingi kama vile elimu, ufahamu, na maendeleo binafsi kupitia
program za mafunzo yetu, ambayo yanawasaidia katika safari yao ya kujiajiri
mwenyewe. Kutoka katika kozi za elimu
kwa njia ya mtandao kama vile SELI/qLearn, mpaka katika vifurushi vya sikukuu
kama vile Tripsavr, mpaka bidhaa za kuongeza nguvu kama vile Bio Disc3,
virutubisho kama EDGE, na saa za mkononi kama Bernhard H. Mayer, QNET ina aina
mbalimbali za kukidhi mahitaji mbalimbali ya watu. Katika kitovu cha yote haya, ni hamu yetu ya
kutoa fursa ya Kuishi Kikamilifu "Absolute Living”
Zaidi ya watu elfu mbili
wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho ya siku 2 ambayo yatakuwa na bidhaa za mfano
katika onyesho, na kuonyesha namna ya matumizi ya bidhaa na faida zake kwa
wateja na watumizji wa mwisho. Kwa kuongezea,
wataalamu wa bidhaa na biashara watakuwepo kwa ajili ya kujibu swali lolote
kutoka kwa wageni ili kuelewa vizuri ulimwengu wa QNET.
QNET inaalika watu wote
kuhudhuria onyesho hili jijini Dar es salaam na kujifunza kwanza kuhusu bidhaa,
huduma na fursa za biashara.
Maonyesho ya Dar es salaam
yanafuata mfululizo wa maonyesho kama hayo yaliyofanikiwa nchini Togo, Guinea,
Ivory Coast, Senegali, Burkina Faso na Cameroon mwaka jana.
Msafara wa maonyesho utasisimama
katika mji wa Kumasi, Ghana, baada ya Dar es salaam kuanzia tarehe 23 mpaka 24
Machi mwaka 2019.
No comments:
Post a Comment