Kampuni inayoongoza ya
mauzo ya moja kwa moja QNET, na mbia katika ligi ya mabingwa ya CAF,
Kombe la Shirikisho la CAF na kombe la Super Cup imewapongeza Shirikisho la
Soka Afrika, CAF na vilabu vyote vinavyoshiriki katika mashindano yote ya klabu
ya CAF mwaka 2019.
QNEt imekaribisha ushirikiano wake na CAF, katika mwaka 2018 na
inaelezea fahari yake katika mpira wa miguu wa Afrika.
Ushirikiano
kati ya kampuni ya QNET na CAF ni sehemu ya juhudi za QNET za kukuza michezo
Afrika na dunia kote.
Kwa
kweli, kama ilivyo katika michezo, QNET inaongozwa na ari ya kufanya kazi kwa
pamoja kama timu pamoja na shauku wakati inapofanya biashara zake kila siku.
Ushirikiano huu ni fursa nyingine kwa QNET kuwa karibu na
wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), walaji na wateja ambako QNET inaendesha
shughuli zake tangu zaidi ya muongo mmoja iliopita.
Meneja Mkuu wa QNET wa Kanda ya Kusini mwa Jangwa la Sahara,
Biram Fall amesema kwamba, “Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka mzuri kwa mpira wa
miguu barani Afrika. Katika QNET tunaona fahari sana kujihusisha na CAF na
ukuaji wa mchezo wa mpira wa miguu barani. Falsafa ya biashara yetu inashikilia
mwenendo wa mpira wa miguu, ambao kimsingi ni ufanyaji wa kazi katika timu,
ushirikiano, shauku na kufanyakazi kwa bidii. Tunawawezesha wajasiriamali
katika bara zima la Afrika na tumejikita katika kusaidia wengi zaidi waweze
kufanikiwa. Vilevile ni heshima kwetu kudhamini mashindano haya maarufu na
yanayoheshimiwa sana, na tusingeweza kupata mshirika bora zaidi kuliko
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kuweza kufanikisha lengo hili. Mwaka 2019
unaonekana kutia matumaini zaidi na QNET itakuwa katika upande wa CAF kwaajili
ya kuhakikisha utendaji bora zaidi”.
Katika mwaka 2019, QNET itakuwepo zaidi viwanjani ikiwa na
uhamasishaji, matukio zaidi kwaajili ya kuhamasisha mashabiki kuongeza nguvu
kazi ya mauzo ya QNET na wawakilishi wa kujitegemea (IRs).
QNET inaendelea kuongeza uwepo wake katika bara zima la Afrika,
ikiwa inatoa fursa za ujasiriamali kwa watu na kusaidia watu kubadili historia
zao vyema zaidi. Ukiachilia mbali ushirikiano wa kimichezo, QNET pia ni kampuni
ambayo inajihusisha na majukumu ya kijamii, kutoa kwaajili ya maendeleo
endelevu ya jamii katika kanda zote ambako inaendesha shughuli zake. Katika
mwezi Novemba, kampuni ya QNET ilitunikiwa tuzo ya mwaka ya e-commerce CSD
Company na Kituo cha Uwajibikaji kwa Jamii cha Afrika Magharibi (Centre for
Corporate Social Responsibility West Africa)
1 comment:
Casinos near me - MapyRO
Find 전라북도 출장샵 Casinos near 아산 출장샵 me near you from 4020 Casinos in The 통영 출장샵 United States, with locations in Nevada, New 밀양 출장안마 Jersey 경상남도 출장안마 and Pennsylvania, and more.
Post a Comment