Thursday, September 8, 2016

Tizama Maswali aliyoulizwa Lipumba Leo Redioni Jinsi alivyoyajibu




SWALI: Je, una uthibitisho kwamba Lowassa ana makosa na anapaswa kupelekwa mahakamani?

JIBU: Hilo mimi sijui, hilo ni la mahakama


SWALI: Sasa Kwanini unasema hafai?

JIBU: Hiyo Mwalimu Nyerere ndiye aliyesema kwamba huyu ana kipato kikubwa ambacho haijulikani amekipataje, sasa kama hadi mwalimu Nyerere alikuwa hamkubali, mimi nitamkubali vipi
SWALI: Kama utarudi CUF, halafu Lowassa akateuliwa na CHADEMA kugombea urais, utamuunga mkono?

NI VITA MPYAAA---MEYA WA KINONDONI AIBUKA NA KASHFA YA AJABU JUU YA SERIKALI YA MAGUFULI,SOMA HII



TAARIFA KWA UMMA
MHESHIMIWA RAIS AJIONDOE KWENYE HILI LA KUHUJUMU MAMEYA WA UPINZANI.
Ndugu wananchi na wakazi wa *Manispaa ya Kinondoni*, nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuepushia mabalaa na kutujalia Afya njema.Hatuna la kumlipa zaidi ya kusema ahsante.

Leo nimeamua kuita vyombo vya habari ili kuhabarisha uma na watanzania wote kwa dhumuni moja tu, la kuelezea masikitiko yangu dhidi ya Utawala huu wa awamu ya tano, ambapo mimi Mstahiki Meya wa kinondoni, nalazimika kwa namna moja kufanya nao kazi ya kuhudumia wananchi.
Naleta masikitiko yangu kwenu si kwa lengo la kuchochea hasira za watu bali kuonyesha, gilba, uzandiki, fitina na uchonganishi tunaokutana nao kutoka kwa viongozi wa serikali ya Awamu ya tano.
Ndugu wananchi lazma tuweke rekodi wazi ya kuwa mimi siyo mteuliwa bali mchaguliwa kutoka kwenye kundi kubwa la viongozi mliowachagua October 2015, hivyo mabosi wangu ni nyinyi na pakushtaki ni kwenu yani uma, ili mnitendee sawa na mapenzi yenu mliyonituma kuwaletea maendeo.

WASHINDI 10 WA SHINDANO LA KUINGIZA SAUTI KWENYE FILAMU KUPATA FURSA YA KUFANYA KAZI NA STARTIMES NCHINI CHINA


Na Dotto Mwaibale 

 WASHINDI 10 kumi watakaopatikana kwenye shindano la kuingiza sauti kwenye filamu na tamthiliya za Kichina kwenda lugha ya Kiswahili liloendeshwa na StarTimes Tanzania watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing, China.

Akizungumzia juu ya taarifa hiyo Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif amebainisha kuwa katika jitihada za kuboresha maudhui ya vipindi mbalimbali vinavyopatikana kwa lugha za kigeni kama vile Kichina yaweze kueleweka na kufurahiwa na wateja wao, kampuni hiyo inatoa fursa kwa watanzania kumi kwenda kufanya kazi ya kuingiza sauti za lugha ya Kiswahili jijini Beijing, China yalipo makao makuu ya kampuni hiyo.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI AGOSTI WAPUNGUA KWA ASILIMIA 4.9

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Agosti, 2016. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja. 
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.

Lipumba "TATIZO NI LOWASA" afunguka yote yanayoendelea sasa,amchana chana Seif.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Haruna Lipumba akjizungumzia sakata lake la kuvuliwa uanachama wakati wa mazungumzo maalumu na CLOUDS FM amesema mpaka maamuzi hayo yanafanywa kwanza hakuwa na barua ya kusimamishwa uanachama mpaka waliposikia kuwa atakuwa na mazungumzo na Clouds ndipo wakamletea barua ya kumsimamisha. 

PICHA BORA LEO BUNGENI--SALAMU NDUGU YANGU

mbo1Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzania na Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe (MB) wakati wa kikao cha tatu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

KUHUSU KUKAMATWA UKILALA GEST MCHANA DAR ES SALAAM-KAULI YA POLISI


 



Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.

Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

MKURUGENZI MTENDAJI MPYA WA TACAIDS AJITAMBULISHA KWA WADAU WA UKIMWI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko.
 Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto), akizungumza na wadau wa ukimwi katika mkutano wa kufahamiana uliofanyika Makao Makuu ya Tacaids Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria (Tacaids), Elizabeth Kaganda na Mkurugenzi wa Ufatiliaji na Tathmini, Dk. Jerome Kamwela.

Tizama--Msafara wa Shindano la “SHINDA GARI NA WHITEDENT” ulivyokuwa Mikoani.

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa Kigoma wakiangalia moja ya gari kati ya magari 25  yanayoshindaniwa  katika shindano la shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo.

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika foleni ya kwenda kujisajili kwenye droo ya bahati nasibu ya shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya  Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo.

Wakazi wa Bariadi, Mwanza wakishuhudia moja ya magari yatakayotolewa kwa mshindi wa shindano la Whitedent, katika msafara wa magari hayo unaozunguka nchi nzima, ikiwa ni sehemu ya kusheherekea  miaka 25 ya bidhaa hiyo tangu kuanzishwa.

Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Singida wakijisajili kwenye droo ya bahati nasibu ya shinda gari na Whitedent linaloendeshwa na kampuni ya kutengeneza dawa ya meno ya  Chemi cotex linaloendelea hivi sasa nchini ili kuadhimisha miaka 25 ya kampuni hiyo

Wednesday, September 7, 2016

VIDEO--RAIS ANACHOCHEA UHASAMA ZANZIBAR,ANABOMOA MUUNGANO WETU-MTIZAME ZITTO KABWE HAPA

PICHA MBILI BORA KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO

ms1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge  wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ms2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 7, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NA HAYA NDIYO MAKAZI MAPYA YA WAZIRI MKUU MAJALIWA HUKO DODOMA

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kushoto)  wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. 

MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA NA SHERIA -ACT WAZALENDO WAKILI ALBERT MSANDO AMVAA MAGUFULI

https://i.ytimg.com/vi/puq4EcS2p34/maxresdefault.jpg
-------------------------
Sina tatizo na hatua za Raisi kuleta 'maendeleo' kwa wananchi na kutetea 'wanyonge'.
ILA nina tatizo na kauli zake. Kuna jinsi ambavyo kama watanzania tumezoea kusemeshana na kuongeleshana.
Sisemi kwamba tuishi kwa mazoea la hasha. 

Ila ni vyema mtu yeyote uangalie unasema nini na wapi kufanikiwa nini.
Mlimani City mpango wa kuijenga ulianza kipindi cha Mh. Mkapa na kumalizika kipindi cha Mh. Kikwete kama sikosei.
Leo hii kusema kwamba mradi huo ni "magodown" ni kuwaonea waliokuwepo wakati unatekelezwa.
Mosi, maamuzi ya Serikali yeyote ni ya pamoja (collective responsibility).

Kama mtu alikuwepo kwenye mabaraza yote ya mawaziri kipindi cha Mh. Mkapa na Mh. Kikwete kipindi ambacho magodown yamejengwa basi hawezi kuepuka ushiriki katika kudanganywa kwetu!!
Pili, sijamsikia mtu akisema barabara ambazo zimebomoka (mfano maeneo ya Chalinze, barabara ya Mbeya, barabara za akachube nk) ni mitaro au mito kwa sababu zilijengwa chini ya kiwango!!
Au ule mradi wa ferry kutoka Bagamoyo - Dar ni WHITE ELEPHANT. 

Au kukumbushia uuzaji wa nyumba za Serikali halafu kwenda kujenga nyingine!! Au kuhusu wale samaki wa wachina kwamba tuliingizwa chaka.

Tatu, uongozi ni endelevu. Zaidi pale ambapo bado ni CCM ndio kipo madarakani. Inatuchanganya wananchi tunapoambiwa tulichezewa na kudanganywa sana huko nyuma. Nyuma tunayoijua sisi ni ya NYERERE, MWINYI, MKAPA na KIKWETE.

"Nyuma" ya CCM. Je ni yupi kati yao alikuwa mzembe na asiyejua kuongoza kiasi kwamba leo hii tuko hapa na magodown yetu???? Atuombe msamaha!! Kwa njia moja au nyingine ni ukweli kwamba sisi watanzania ni majuha. Tumechezewa wakati wa hao wote wala hatukujua. Leo angalau ametokea mtu kutuambia ukweli. Mzee Mkapa alikuwa sahihi kutuita malofa. 

Lakini najaribu kujiamiaminisha kwamba Mh. Raisi ni mtu wa kauli za utani. Mfano,
1. Kufyatua watoto
2. Siasa mpaka 2020
3. Kuwapoteza nusu walioimba kwenye mkutano
4. Kumzamisha kisimani aliyezuia watu kuchota maji 5. Kutoa matairi kwenye magari yanayovunja sheria za barabarani.
6. Polisi kutokuwa rafiki na raia.
7. Kutokusaini pensheni mtu asipokupa mkono wa salamu nk nk.
Natamani sana niamini hivyo. Ni utani tu. Naomba sana iwe hivyo.
*#TatizoNiSisi*
*Alberto Msando*