Friday, March 3, 2017

VIDEO-LEMA ALIVYOTOKA NDANI TU AKASEMA HAYA KUHUSU RAIS MAGUFULI

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA KIWANDA CHA VIGAE MKURANGA PWANI MARCH 2,2017

VIDEO): KIJANA PAUL MWILOMBWA MLEMAVU WA VIUNGO ANAOMBA MSAADA WAKO ILI AWEZE KUTIMIZA MALENGO YAKE KUPITIA SHUGHULI ANAYOIFANYA


Paul Ibrahim Mwilombwa ni Kijana anayeishi Mkoa wa Geita Wilaya ya Chato, ni mlemavu wa viungo na mwenye kujishughulisha na maswala ya upigaji picha na mambo ya 'Graphic Design'.  hapa anaelezea historia yake na kuwaomba msaada watanzania ili apate kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

RAIS MAGUFULI ATOA MIEZI MINNE MRADI WA MAJI WA NG’APA MKOANI LINDI UKAMILIKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi minne na si vinginevyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mshindi wa Tigo Reach for Change kutangazwa March 9

Washiriki Wa Tigo Reach  For Change Waliofanikiwa Kuingia Katika Mchujo Wa Mwisho Wakiwasilisha Wazo Lao Ubunifu Mbele Ya Majaji Mapema Wiki Hii Katika Ofisi Za Makao Makuu Ya  Tigo ,Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.
Majaji wa Tigo Reach for Change wakimsikliza kwa makini mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuingia katika mchujo 

Na Mwandishi Wetu

  Mashindano ya mwaka huu  ya Waleta mabadiliko ya kidijitali wa Tigo yamefikia katika hatua ya juu  ya kuchagua washindani watano  kufuatia mchakato wa mapitio ambao ulijumuisha waombaji 358. Shindano hili hufanyika kila mwaka na liko wazi  kwa waombaji kutoka  nchi nzima  limejielekeza katika  kuibua vijana mahiri  walio na ubunifu wa miradi ya kidijitali inayoboresha maisha ya watu, hususani watoto kwa kutumia programu za kidijitali.

Thursday, March 2, 2017

JUKATA WACHOKOZA TENA KATIBA MPYA,SASA WAMBEBESHA ZIGO LA LAWAMA RAIS MAGUFULI


Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa La katiba Tanzania
                                         Na Vicent Macha 
Jukwaa la katiba nchini Tanzania leo limezindua mkutano wake utakaodumu kwa siku mbili ukiwa na lengo la kuitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoa mustakabadhi wa katiba mpya baada ya  kudai kuwa mchakato ulianzishwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na kuhitaji serikali ya awamu ya tano kuweza kumalizia mchakato huo.

DIWANI WA KATA YA BUGURUNI ADAM FUGAME AMEWAAGIZA VIONGOZI WA KATA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WASIOFANYA USAFI.


Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya buguruni kwa malapa kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. (PICHA NA ELISA SHUNDA)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu baada ya kufanya usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na Katibu tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo.
NA EMERISIANA ATHANAS
DIWANI wa Kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame ameagiza viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.

WADAU WA MUZIKI WA INJILI KUKUTANA JUMAMOSI UKUMBI WA CHUO CHA USTAWI WA JAMII JIJINI DAR ES SALAAM

 Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam leo wakati akifafanua kuhusu sheria ya haki miliki ya kazi za wasanii wa muziki.
 Rais wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kassanga  akifafanua mambo kadhaa katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na TMF, kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na dawa za kulevya.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba akizungumza katika mkutano huo.

MALAWI YAISHAURI GIHON TANZANIA KUFUATA SHERIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry,  Rebecca Stanford (kushoto), akiwa na  Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja wakati walipokwenda ofisi ya Balozi wa Malawi nchini.
 Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry,  Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  Gihon, Leonce Zimbandu na Ofisa Habari, Michael Malanyingi.
 Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry,  Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  Gihon, Leonce Zimbandu

WAZIRI MKUU KASSIM MAJARIWA KUFUNGUA MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF JIJINI ARUSHA

 Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa tisa wa LAPF utakaofanyika Machi 9 na 10, 2017 Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kulia ni Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata na Ofisa Masoko na Mawasiliano wa LAPF, Rehema Mkamba.
 Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.

Wednesday, March 1, 2017

JINSI ALIKIBA ALIVYOPOKELEWA JANA NA TUZO YA MTV


Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika
Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tuzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika

Mashabiki wa Ally Kiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani
Kiba akielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzungumza na mashabiki wake

RAIS MAGUFULI AMTEUA MKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KUWA MBUNGE TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tigo, Ericson washirikiana kuunganisha maeneo ya vijijini Tanzania

 Tigo na Ericson wazindua maeneo ya kwanza ya 3G katika miundombinu ya ushirikiano ya GSMA inayojielekeza  kuunganisha maeneo ya vijijini nchini Tanzania.
·   Mfumo wa Redio wa Ericsson  kwa mara ya kwanza utawapatia wateja huduma bora ya mtandao wa simu, huduma iliyo na ubora ambayo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo  imekuwa ikiitoa kwa wateja mbalimbali.
·  Katika ushirikiano huu, kampuni ya Tigo itakuwa na asilimia 40 katika uendeshaji wa mtandao.
Ericsson (NASDAQ:ERIC) na mtandao wa simu  unaoendeshwa Tanzania Tigo  wameungana  katika kuzindua maeneo ya minara ya mfano katika maeneo ya vijijini  itakayotoa  huduma za simu kwa maeneo  ya Chiwale na Mingumbi katika mikoa  ya  Lindi  na Mtwara ambayo yamo ndani vijijini  na awali yalikuwa hayajaunganishwa.