Tuesday, August 29, 2017

LHRC + LISSU KUWASHA MOTO LEO ANGALIA VIDEO HII...

Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu kikishirikiana na Chama
cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) pamoja na mtandao wa haki za binadamu THRDC,
TANLAP na WiLDAF kwa pamoja wameungana kukemea vikali tukio la kuvamiwa na
kulipuliwa kwa mabomu ofisi ya mawakili ya IMMA tukio lililotokea usiku wa
kuamkia tarehe 26 mwezi agosti 2017 jijini Dar es salaam.


Kutokana na kutokea tukio hilo na mengi ya
kujaribu kuuminya uhuru wa wanasheria katika kutimiza majukumu yao kituo cha sharia
na mashirika rafiki wameroa maazimio yafuatayo..



                                                ANGALIA VIDEO HII.. 



                   

KAMATI YA NIDHAMU YA TFF KUKAA KITAKO KESHO

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kinatarajiwa kuketi kesho Jumatato Agosti 30, mwaka huu.

Kamati hiyo itakuwa na ajenda kadhaa ikiwamo ya mashauri yanayohusu wachezaji mbalimbali, viongozi na klabu.
Shauri mojawapo linahusu ripoti ya Mechi namba 236 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliokutanisha timu za Mbao FC na Yanga uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Yanga ikipoteza kwa bao 1-0.

Mara baada ya mchezo huo, Kamati ya 72 ya Bodi ya Ligi ilipitia matukio mbalimbali na kufikia uamuzi wa kuwasimamisha wachezaji Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga kucheza mechi za Ligi Kuu.

Walisimamishwa wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wachezaji hao walidaiwa kufanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati ya Saa 72 ulizingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Mwamuzi Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu w Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Tisheti na jinzi ya Manji zaibua mapya

Akizungumza na gazeti hili, Maalim Hussein alisema nguo nyeusi kinyota ina maana nyingi kama vile kuonesha huzuni, msiba, au kupatwa na mkosi. Maalim Hassan aliongeza kuwa inaweza kuwa ni kwa sababu hizo alizozitaja kwamba mshitakiwa anajua kwamba huu ni wakati wake wa huzuni.

“Ni kwamba Manji anajua kuwa yupo shimoni, hivyo anatakiwa afanye kila linalowezekana ili kujinasua, na ndiyo maana ameweka mawakili ili wamnasue kule shimoni,” alisema Maalim Hassan.

Akifafanua zaidi mtabiri huyo alisema nguo nyeusi huonesha pia kwamba ni siku ya mikosi ambayo kinyota ni Jumamosi.

“Hivyo mtu kuvaa nguo nyeusi iwe ni shati, suruali, jinzi au soksi, inamaanisha ana huzuni na ndiyo maana watu wengine wakifiwa huvaa nguo za rangi hiyo na kwa wale wenye imani nyingine huona kuwa nguo za rangi hiyo huashiria mkosi, hivyo huwa hawazivai hata kama ni siku ya msiba,” alisema.



“Kwa hiyo Manji kuvaa tisheti nyeusi au viatu vyeusi na soksi nyeusi au jinzi nyeusi siyo kwamba hana nguo au viatu vya kubadilisha lakini haina maana kwake kuvaa makoti makubwa ya rangi nyingine kwa sababu ana matatizo, ana huzuni na ni kama yupo shimoni kinyota,” alifafanua mnajimu huyo. Akaongeza:

“Amini kwamba Manji ataendelea kuvaa hivyo mpaka kesi zake zitakapokwisha na licha ya nguo nyeusi hata ndevu zake nyeusi kaziachia, hazinyoi, sababu ni hiyohiyo siyo kwamba hana fedha za kununua wembe wa kunyolea.” Manji hivi sasa ana kesi mbili mahakamani, moja ni tuhuma ya kuhujumu uchumi na ya pili inahusu madai ya kutumia madawa ya kulevya aina ya heroine.

Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambaye anasikiliza kesi ya madawa, wiki iliyopita alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi watatu wa upande wa mashtaka
ameridhika kuwa mshtakiwa huyo ana kesi ya kujibu hivyo ana haki ya kujitetea na kuita mashahidi. Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo alidai kuwa mteja wake atajitetea kwa njia ya kiapo na wana mashahidi 15.

Pia aliomba hati ya wito (samansi) kwa ajili ya kuwaita mashahidi hao. Kesi imeahirishwa hadi kesho Agosti, 30 na 31,2017 ambapo Manji ametakiwa aanze kujitetea. Awali upande wa mashtaka ulisema ungeita mashahidi wasiozidi 10 kutoa ushahidi lakini watatu ndiyo waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo.

Manji alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 akidaiwa kuwa kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Manji alikana kuwa siyo kweli na kwenye kesi hiyo anawakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Mosses Kimaro ambapo alipata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa ambaye alisaini bondi ya Sh. milioni 10.

Hata hivyo, mfanyabiashara huyo, licha ya kupata dhamana katika kesi ya kwanza, yupo rumande kutokana na kesi ya uhujumu uchumi ambapo anadaiwa alikutwa na vitambaa vya jeshi la wananchi na mihuri ya makamanda wa jeshi hilo la lile la kujenga taifa.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipoketi Agosti 25, mwaka huu iliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo ili matokeo ya kesi hiyo yajulikane mapema. Rai hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na wataeleza hatua ulipofikia katika tarehe itakayopangwa tena.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanajitahidi kukamilisha upelelezi ili matokeo yake yajulikane mapema ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31, 2017.

Mbali ya Manji, washtakiwa wengine ni Deogratius Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwere ambao wanakabiliwa na mashtaka saba chini ya sheria ya Uhujumu Uchumi na Usalama wa Taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeneza sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 200 na mihuri.

NAFASI ZA KAZI 1083 KUTOKA TAASISI MBALIMBALI ZIMETANGAZWA,SOMA HAPA

ZITTO KABWE KUGOMEA UTEUZI WA RAIS MAGUFULI

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa hatokubali endapo Rais Dkt Magufuli atamteua kushika nafasi yoyote ya uongozi kwani hatakuwa na fursa ya kukijenga chama chake ili kiwe tayari kushinda uchaguzi na kushika dola.


Zitto ambaye chama anachotoka tayari kimetoa viongozi wawili ambao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Elisha Mghwira alisema endapo atateuliwa, atamshukuru Rais na kukataa uteuzi huo.


Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Mwananchi wakati akijibu swali kuhusu uteuzi wa viongozi wa chama chao ambao mmoja alikuwa mshauri wa chama na mwingine alikuwa mwenyekiti wa chama hicho kichanga Tanzania.


“Sitakubali uteuzi kwa sababu jukumu langu na viongozi wengine wa ACT- Wazalendo ni kujenga chama ili kupata ushawishi na kuungwa mkono na umma na hatimaye kushika dola,” alisema Zitto.


“Kukubali uteuzi utakaoniondoa na kuniweka kando kwenye jukumu na malengo hayo ni kufifisha matumaini ya maelfu ya wana-ACT Wazalendo,” aliongeza Zitto.


Akizungumzia sababu za chama kuridhia uteuzi wa Prof. Mkumbo, Zitto alisema kwamba hapo hali ilikuwa ni tofauti kwa sababu kabla na baada ya uteuzi wa Mkumbo, yeye ni mtumishi wa umma, hivyo uteuzi wake haukushtua.



“Mama Anna Mghwira alikuwa ni mwanasiasa kwa nafasi yake ya uenyekiti Taifa, ndio maana tulimuondoa ili kumpa fursa kutumikia serikali.”

WALIMU WA FIELD WAKAMATWA NA POLISI KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAO

Walimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo.


Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, January Lugangika amesema waalimu wa wanafunzi hao wamekikuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.


Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa ushahidi wa tukio hilo umethibitishwa na Daktari ambaye aliwafanyia vipimo na kuthibitisha ni kweli kitendo hicho kilifanyika


Kwa upande wa Afisa elimu wa sekondari Wilaya ya Lushoto Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.


"Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita," alisema Singato.



Watuhumiwa wa tukio hilo ni mwalimu Fredriki Shebila na Saddat Mohamed.

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI DAR

Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.
Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba.

Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

MAJINA 8 YALIYOPITA MCHUJO WA AWALI UONGOZI TPLB

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Waliopitishwa ni kuwania uenyekiti wa Management Committee ni Clement Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan Crysostoms ameiptishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti. 

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.

Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.

Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.

Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.

Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

TAMKO KALI TOKA KWA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WAKISHIRIKIANA NA TUNDU LISSU


WAKATI leo na kesho mawakili nchi nzima wakiwa kwenye mgomo wa kutoudhulia kwenye Mahakama na Mabaraza ili kulaani tukio la kuvamiwa na kulipuliwa na mabomu ofisi ya mawakili wa Imma lililotokea mwishoni mwa wiki.
Mgomo huo umefanyika kwa aina baada ya Kituo cha Sheria na Haki na Binadamu (LHRC) ,Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC)  na mashrika mengine ya TANLAP pamoja na WILDAF ambapo nao wameungana na Chama cha Wanasheria Nchi (TLS) katika kuendeleza mgomo huo.

Hatua ya wao kufanya hivyo wamesema ni kukemea na kulaani tukio hilo ambalo wanadai linahatarisha utetezi wa haki ya uwakilishi na uwezo wa wanasheria kutekeleza majukumu yao. 

Huku wakiwa wakitekeleza mgomo huo asasi hizo za binadamu, washirika hao wakiwa wamevaa nguo nyeusi pamoja na kujifunga vitambaa vyeusi mdomoni pamoja na kuwa na mabango yenye ujumbe wa kulaani tukio hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutekeleza mgomo huo,Mkurugenzi wa (LHRC)Dkt Helen Bisimba amesema  tukio hilo limeleta hofu katika tasnia ya sheria nchini.
“Tunaungana TLS kulaani tukio hili kwani limeibua hofu kubwa katika tasnia nzima ya sheria ,hususani kwa mawakili,katika kutekeleza  majukumu yao kwa ujumla ,tukio hili ni la kikatili na la kigaidi ambalo linapaswa kukemewa na kupingwa vikali na wadau wote wa haki za binadamu ambapo sisi LHRC tunaungaza na wenzetu kulaani”amesema Bi Bisimba.
Bi Bisimba amendelea kusema kwa uchungu kuwa kwa kipindi cha miaka miwili sasa kumekuwa kukiripotiwa  matukio kadhaa ya kuwashambulia  na kuwatisha wanasheria  pale wanapokuwa wanatekeleza majuku yao .
Ametolea mfano mnamo mwezi Julai mwaka 2016 ,Naibu Mkurugenzi wa  Upelelezi  wa makosa ya Jinai Zanzibar ,Kamishna Msaidizi wa Polisi  Salum Msangi kusema wanasheria wanaotetea wahalifu wataunganishwa na wahalifu katika makosa pamoja tukio lilotokea katika mwaka huo la kukamatwa mwanasheria  LHRC ,Wakili Shilinde Ngulula ambaye alikamatwa na kuwekwa ndani na askari polisi  wilaya ya Ngorongoro wakati akiwa kazini amedai vitendo hivyo ni muendelezo wa ukandamizaji kwa wanasheria.
‘’Yapo matukio mengi  yanayokanyaga uhuru wa sheria nchini likiwemo lile agizo la Rais John Maguli wakati siku ya sheria 2/2/2017 alipoagiza watuhumiwa wa ujangili kuchukuliwa hatua punde wanapokamatwa,hii ni kauli ya kuingilia mhimili wa mahakama”amesema Bi, Bisimba
Bi Bisima ameenda mbali kwa kusema kitendo cha Rais Magufuli kutomteua Jaji mkuu mpaka sasa ,huku akiendelea kumtumia kaimu jaji mkuu ,kitendo hiki ni kinakwenda kinyume na katiba ya nchi na kinashindwa  kuimarisha mhimili wa mahakama na utawala wa sheria nchini.
Pamoja na hayo LHRC wameitaka serikali kupitia jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linawakamata watu wote ambao wamehusika katika shambulizi la ofisi ya IMMA na kuhakisha wanachukulia hatua.
Pichani ni Mkurugeni wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)Dkt Helen Bisimba akizungumza na waandishi wa habari leo kuunga mkono mgomo wa mawakili nchini

Aidha,wametaka viongozi wa serikali na vyombo vyake wenye dhamana ya kulinda usalama wa watu nchini na haki za binadamu  kwa ujumla wawajibike au kuwajibishwa  mara moja pale ambapo wameshindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao. 
Rais wa chama cha mawakili nchini (TLS)Tundu Lissu akiwa kwenye Mgomo huo
  TUNDU  LISSU ANENA.
Naya Rais wa TLS,ambaye pia ni Mbunge wa Singida mashariki,Tundu Lissu amesema kwa sasa hali ya nchi kwenye hali ya tasnia ya sheria sio nzuri kutokana kuwepo kwa vitendo mbali mbali.
“Nataka niwambie leo ofisi za Mawakili zinapigwa bomu,leo mwakili wamejaa hofu ,kesho uwenda ikawa zamu ya watu wengini,ndio maana tunapaza sauti zetu kulaani tukio hili”
“Kama yupo leo Wakili ambaye amesusia mgomo wa leo na kwenda mahakamani namuomba afikilie kuwa tukio lile likitokea kwake itakuwaje”amesema Lissu ambaye pia ni Mwanasheria mkuu wa Chadema.
   THRDC wafunguka .
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC),Onesmo Olenguruma amesema kitendo cha kulipuliwa ofisi ya IMMA ni cha kinyama kinatakiwa kupingwa na kila mtu kwani kimeleta hofu katika tasnia ya sheria nchini.
   HALI YA MAHAKAMA IPOJE
Fullhabari.blog ilifika kwenye mahakama mbali mbali jijini Dar es Salaam na kushudia idadi ya mawakili wengi wakiwa wameungana na TLS katika kutekeleza mgomo wa kulaani tukio hilo.
Akizungumza kwa sharti la kutotaja jina lake,wakili mmoja maarufu alisema lazima naye alishiriki kwenye mgomo huo kwani kitendo walichofanyiwa wenzao ni cha kinyama.
“Tunakwenda kubaya sana lazima wanasheria tuungane kulaani hali hii,huu mgumo ni wa kila mtu,maana leo tumeona ndani nchi yetu mihili aiheshimiwi kabisa ,Mahakama hazipo huru ambalo ni jambo la hatari kabisa katika nchini lazima tuungane kupiga vita”amesema Wakili huyo msomi.


SPARK TOUR YAJIZOLEA UMAARUFU JIJI

                                                  
TECNO Mobile, kampuni inayoongoza kwa simu bora nchini Tanzania imetambulisha mfumo mpya wa burudani na matangazo nchini ukiambatana na  simu mpya katika mpangalio wa matokeo mapya ya SPARK. Tecno Mobile imeanzisha mtindo mpya wa kuwafwata wateja wake mitaani na kuwapa burudani kupitia wanamuziki mbalimbali.  Mtindo huo maarufu kama SPARK TOUR umekua maarufu katka kona za mitaa za Jiji la Dar es Salaam.



Tecno Spark ambayo simu tambulishwa, ni simu  ambayo imekua gumzo kwa kuwapa wateja wengi wa kampuni hiyo furaha kwani bei inayouzwa linganisa na ubora wa simu hiyo ni faida kubwa kwa wateja wa Tecno Spark. Kupitia simu hii ya SPARK vijana wa kitanzania wameshawishika kuwasha cheche za vipaji  vyao na kuzionesha kupitia jukwaa la Tecno SPARK  udhamini wa karibu wa Tecno Mobile.


Afisa Mahusiano wa Tecno mobile Bwana. Eric Mkomoye amesema kua  nia na madhmuni ya Tecno ni Kuendelea kuwaltea  watanzania simu  bora  zenye uwezo mzur ila kwa bei  wanazoziweza kutokna na vipaji vyao. Aliongeza kua SPARK TOUR itawafikisha watanznia wote nyanda za ziwa, kaskazini  na hata mikoa ya katikati hivyo zawadi za aina mbalimbali ikiwemo Tecno spark yenyewe  zitatolewa. 
(Mitaa ya jiji la Dar es salaam ikiwashiwa cheche za burudani na SPARK TOUR)
Kama isemavyo kua kipaji chako ndio ufunguo wako , ndio inavyokua kwa vijana na watu wanonesha vipaji kupitia simu hii mtaa kwa mtaa jijini Dar es salaam, uvumizi wa kiburudani unafwanywa na  kamouni  Tecno Huku lengo likiwa pia kutoa nafasi kwa viijana wa kitanzania kuonesha uwezo wao ili waweze kusaidiwa.

Tecno SPARK imekuja ikiwa na utofauti mkubwa huu ikiigemea katika upande wa kiburudani zaidi .Simu inahamasisha vijana kua na mitindo  inatambulishwa ikiwa na kamera nzuri yenye picha ang’avu kwa 13MP, Teknolojia ya mix flash, usalama wa kibabe wa kutumia alama za vidole , kioo chake ni kina ukubwa wa inchi 5.5 , 16gb za kuweka vitu ndani wakati inasukuma data kwa 2gb ram. Tecno Spark inakuja ikiwa na rangi mbalimbali rangi nyeusi,(phatom black), rangi ya dhahabu (champagne gold) na rangi ya blue (coral blue).
(mitaa ya jiji la Dar es salaam ikiwashiwa cheche za burudani na SPARK TOUR