JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA MAMLAKA YA MAWASILIANO
TANZANIA: MIAKA KUMI YA MAPINDUZI YA MAWASILIANO TANZANIA
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea
maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa
dhahiri na ya kujivunia katika sekta ya mawasiliano nchini.
TCRA ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 23 mwezi Novemba
mwaka 2013 ili kusimamia Sekta ya Posta na Mawasiliano ya Elektroniki ikkiwemo
simu, utangazaji, wavuti pamoja na huduma za Posta. TCRA ilkianzishwa kwa
Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoziunganisha Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC)
na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mkakati
mahususi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni “Kuboresha Maisha ya Watanzania kupitia mfumo makini na thabiti ili
kuhakikisha kunakuwa na huduma za mawasiliano kwa wote nchini”. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita,
Tanzania imeshuhudia kukua kwa kasi kwa Sekta ya Mawasiliano. Mamlaka
ilianzisha mfumo wa leseni za Muingiliano mnamo tarehe 23 Februari 20005.
Mfumo huu wa
leseni za muingiliano (Convergence Lisensing Framework) umekuwa chachu ya
kuongezeka kwa miundombinu mbalimbali ya mawasiliano, huduma mbalimbali kwa
kutumia mtandao wa mawasiliano ikiwemo wavuti (internet) na utangazaji.
Makampuni ya
simu yameongezeka kutoka kampuni moja ya simu TCRA ilivyoanzishwa mwaka 2003
hadi kufikia makampuni saba (7) yenye wateja wenye laini za simu takribani
milioni 28 kulinganisha na idadi iliyokuwepo miaka kumi iliyopita. Huduma za
simu za mkononi zimebadilisha maisha ya Watanzania kutokana na huduma
mbalimbali zinazopatikana kupitia simu za mkononi. Kuanzia huduma za kutuma
fedha kupitia simu, malipo ya Ankara mbalimbali na huduma nyingine nyingi
zilizobadilisha maisha na uchumi wa wananchi wa taifa hili.
Sekta ndogo
ya Posta nayo haijabaki nyuma kwani kumekuwepo na ongezeko la watoa huduma
kutoka mmoja hadi zaidi ya hamsini wenye kutoa hduma ndani nan je ya Tanzania.
Tunatarajia mabadilikjo makubwa kwa watanzania hasa baada yan kukamilika kwa mradi
wa anwani mpya za makazi na misimbo ya Posta.
Hali
kadhalika, yako mabadiliko makubwa sana katika msekta ndogo ya utangazaji.
Kutoka nchi yetu kuwa na Radio moja hadi Zaidi ya redio 85. Aidha kutokuwepo
kwa Kituo cha Utangazaji wa Runinga hadi vituo vya utangazaji vipatavyo 26.
Watumiaji wa wavuti (intanet wameongezeka kutoka watumiaji million moja hadi
takribani milioni 8 na ushee. Sekta ya Mawasiliano imekuwa chimbuko la
maendeleo ya nchi kwa kutoa ajira kwa watanzania wengi na hali kadhalika
kuongeza mapata ya serekali kwa tozo na kodi mbalimbali zinazotolewa katika
sekta..
Mamlaka ya
Mawasiliano imeshinda tuzo mbalimbali katika masuala ya Udhibiti na Usimamizi
Bora wa Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi cha kuweko kwake miaka kumi
iliyopita. Nchi mbalimbali zimekuja Tanzania kujifunza udhibiti na usumamizi wa
masuala nyeti ya mawasiliano kama vile masuala ya uhamaji kuelekea mfumo mpya
wa utangazaji wa dijitali, Mifumo ya uanzishwaji wa anwani za makazi na misimbo ya posta, Usimamizi
mzuri wa masafa na namba za mawasiliano na mambo mengine mengi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO TANGU 25 – 29 NOVEMBER 2013
Katika kusheherekea miaka kumi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
kutakuwa na maadhimisho ya wiki nzima yenye matukio mbalimbali. Tukianzia na
mkutano huu na waandishi wa habari uliokusudia kutoa taarifa kwenu na kwa
wananchi kuhusu maadhimisho haya, kutakuwa na matukio kadha wa kadha kuelekea
kilele cha sherehe za maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika tarehe 29 Novemba
2013.Maadhimisho haya yanafanika chini ya kauli mbiu ya; Miaka 10 ya TCRA: Miaka
Kumi ya Mapinduzi Katika Sekta ya Mawasiliano
Kesho tarehe
26 Novemba 2013 kutakuwa na tukio maalumu kwa wafanyakazi wa mamlaka ambapo
wale waliokuwepo tangu wakati wa kuanzishwa kwa TCRA watatunukiwa vyeti pamoja
na zawadi mbalimbali kutambua mchango wao kwa taasisi.
Aidha siku ya
tarehe 27 Novemba 2013; kutakua na sherehe ya kutoa udhamini kwa
wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu wanaochukua masomo ya mawasiliano,
sayansi na teknolojia. TCRA kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo imekuwa
ikitoa udhaminim katika masomo hayo kwa wanafunzi mahiri kwa nia ya kukuza
weledi na kuboresha utumishi katika sekta ya mawasiliano chini ya kinachoitwa “TCRA ICT SCHOLARSHIPS” kwa wanafunzi wa
digrii ya kwanza, digrii za Uzamili na Uzamivu.
Kuanzia
tarehe 27 – 29 Novemba, kutakuwa na maonesho maalumu katika viwanja vya ukumbi
wa mikutano wa Mlimani City ambapo watoa huduma mbalimbali za mawasiliano
nchini wataonesha mafanikio yao na huduma wanazotoa kwa wananchi. Napenda
kuchukua fursa hii kuwasihi waandishi wa habari kuhudhuria maonesho haya ili
kujifunza na kutumia fursa hiyo kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu huduma
mbalimbali za mawasiliano zinazopatikana nchini ili wachangamkie fursa.
Hali
kadhalika, katika maadhimisho haya, TCRA imeandaa washa maalumu ya siku mbili
wa wadau wa mawasiliano kujadili fursa, changamoto pamoja na namna gani kwa
pamoja tunavyoweza kufanya mawasiliano kuwa bora Zaidi nchini mwetu. Warsha
hiyo itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City na itafunguliwa rasmi
tarehe 28 mwezi huu na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na utaendelea hadi tarehe 29 Novemba 2013.
The Opening Ceremony will be graced by Dk. Mohammed Gharib Billal.
Wadau mbalimbali wa Mawasiliano kama
vile kituo cha Habari cha Tanzania Network Information Centre (tzNIC), Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote - Universal Communications Services Access Fund (UCSAF), Wamiliki
wa Vyombo Vya Habari - Media Owners Association of Tanzania (MoAT-
Broadcasting), na Umoja wa Makampuni ya Simu - Mobile Operators Association of
Tanzania (MoAT-Mobile Telephony Companies), Africa Media Group, Agape
Associates and TTCL watawasilisha mada mbalimbali.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa
katika shughuli zote za maadhimisho ya Miaka 10 ya TCRA ili kutoa elimu kwa
umma lakini pia kama fursa ya kujionea mafanikio ya sekta ya mawasiliano katika
kipindi cha miaka kumi iliyopita ili kuwawezesha wananchi kufahamu tulikotoka,
tunakoenda na fursa zilizoko katika sekta ili kuboresha maisha yao.
Imetolewa na:
Mkurugenzi
Mkuu
25th November
2012
No comments:
Post a Comment