JB AU BONGE LA BWANA ALIKUWEPO |
MKURUGENZI MKUU BW RHYS TORINGTON AKISALIMIANA NA WASANII WA BONGO MUVIES KATIKA MAKAO MAKUU YA AZAM LEO ASUBUHI |
AzamTV
leo imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma
za matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6,
2013 kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi
hii leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa
mwezi.
Kwa
kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu
za kimataifa, chaneli maarufu za ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo
ni:
· Azam
One – burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa
lugha ya Kiswahili.
· Azam
Two – vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
· SinemaZetu
– Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa
pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya
michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi
ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media
Ltd.
“Ofisi hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni
kielelezo cha nia thabiti ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika
shughuli ya utangazaji hapa Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango
cha juu kwa familia kwa bei nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika.
Hili ni jambo ambalo kila mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema
Bakhresa
Rhys Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema:
“Naona faraja kubwa kwamba leo hii AzamTV ipo sokoni kwa ajili ya kila
mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote tutaburudusha watu kote
nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ katika ofisi hizi lakini pia
kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala 50 katika kila mkoa. AzamTV
ni ya kudumu”
Azam
Media pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake
tanzu, Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa
Tanzania.
YUSUFU AKIWA NA BAADHI YA WASANII WA BONGO MUVIE AMBAO NAO WALIKUWA MIONGONI MWA WALIOSHUGHUDIA TUKIO HILO |
MKURUGENZI MTENDAJI WA AZAM TV BWANA YUSUFU BAKHRESA AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUANZA RASMI KWA HUDUMA ZA AZAM TV |
No comments:
Post a Comment