Azam Media Ltd
leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo
kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.
Hatua hii muhimu sasa
inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake kote Tanzania
kuanzia tarehe16 Desemba. Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia zaidi ya
chaneli 50 za kitaifa na kimataifa ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia
kwa bei nafuu ya shilingi 12,500/= kwa mwezi. Kutakuwepo wigo mpana wa kuchagua
kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na tamthilia
kutoka Tanzania, barani Afrika na sehemu
mbalimbali za dunia. Baadhi ya vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli
maarufu kama vile National Geographic Gold na Nickelodeon, na pia matangazo yetu
yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10, Clouds, ZBC na
K24.
SOMA ZAIDI HAPO CHINI-------
Jambo la kusisimu zaidi ni kwamba AzamTV itakuwa na matangazo katika chaneli
zake tatu:
AzamOne - Itakuwa na vipindi
vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu masuala ya Afrika Mashariki
kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa ikirusha matangazo ya
Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;
AzamTwo – Hapa vitapatikana
vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya kimataifa na baadahi ya hiovyo
vitakuwa katika lugha ya kiswahili;
SinemaZetu – Chaneli maalum kwa
ajili ya tamthilia za kitanzania.
Mtendaji Mkuu wa Azam Media,
Rhys Torrington, alisema: “Huu ni wakati
wa kujivunia kwa Tanzania kwani sasa ina
huduma za luninga zinazopatikana kwa bei
ambayo wengi wanaweza kuimudu. Miezi
michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika
Mashariki na hata mbali zaidi. Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika
chombo hiki cha kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo”.
Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao hawatapenda kungojea kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi zake za Dar es Salaam itakuwa wazi kuanzia leo (Ijumaa Desemba 6, 2013). Wateja wataweza kununua vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala walioidhinishwa na hivyuo kuweza kujionea vipindi mbalimbali kuanznia sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.
No comments:
Post a Comment