Jana
mitandao ya kijamii ilijazwa taarifa kwamba jana jioni, John Mnyika (Mb)
alimwandikia barua ya kujiuzulu Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ofisa Habari Mwandamizi wa CHADEMA, Tumaini Makene (0752 691569) alijibu kwa kukanusha kuhusu taarifa hizo na kuongeza kuwa kwa muda uliotajwa, Mhe. Mnyika alikuwa katika shughuli za chama akitimiza majukumu yake. Akasema taarifa hizo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa sababu ya, “kuwasumbua wanachama na Watanzania, lakini pia kutaka kuonesha kuwa kundi la wasaliti na wanafiki ndani ya chama linaungwa mkono na watu makini ndani ya chama ambao kama wangekuwa upande wao, wangesaidia kundi hilo kuondoa taswira hasi linalopata mbele ya jamii. Wanatafuta uhalali walioupoteza kwa kufanya harakati za kusaliti mapambano.Mioyoni mwao wanaumia kweli kweli kuonekana wanaungwa mkono na watu wasio wanachama wa CHADEMA, ambao wengine wanalazimika kwenda kuwanunua pale feri Posta na Kariakoo ili waje kuwashangilia Mahakamani na kukimbia barabarani. Tunajua wanaumia kutumia mamilioni kukodi watu kuja kulia kwenye msiba wasioujua wala usiokuwa wa kwao, huku wakidai ujira hadharani. aliandika Makene kwenye tovuti ya MwanaHalisiForum Kubenea katika tovuti hiyo aliandika, “Nathibitisha ifuatavyo: Nimeongea na Mnyika muda huu, amenihakikishia kuwa habari hiyo siyo ya kweli. Hajajiuzulu na wala hana sababu ya kujiuzulu. Anasema, hawezi kuungana na watu wanaokivuruga chama. Anaipenda Chadema na anaamini ndiyo chama bora kwa sasa. |
Thursday, January 9, 2014
UKWELI WA TAARIFA YA KIJIUDHULU KWA JOHN MNYIKA CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment