TANGAZO
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka kufanya
Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na
Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi
cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1
Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa
wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT
kitaishia tarehe 28 Februari,
2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili
mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye
mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba
rejea (reference number) zinazotolewa bure
na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA
MITIHANI LA TANZANIA.
No comments:
Post a Comment