Thursday, April 3, 2014

YANAYOENDELEA SASA----MANISPAA YA KINONDONI YANUNUA MAGARI MAPYA 10 YENYE THAMANI YA MIL 779 KWA KUTUMIA VYANZO VYA MAPATO YA NDANI

 Magari Mapya aina ya Toyota  Yakiwa Manispaa ya Kinondoni leo mara baada ya kukabidhiwa
 Mwonekano wa moja ya gari mpya zilizonunuliwa na manispaa ya kinondoni
 Gari mpya aina ya Landcruiser ikiwa Ofisi ya manispaa ya Kinondoni
 Mstahiki Meya Yussuph Mwenda akiongea na Vyombo vya habari Leo mara baada ya kukabidhiwa magari hayo
Meya wa Kinondoni Yussuph Mwenda akikabidhi funguo kwa mmoja wa madereva
 
Manispaa ya Kinondoni imenunua magari kumi (10) hard top na double cabin, Magari hayo yanayo gharimu kiasi cha Tshs. 779 milioni ikiwa ni mapato ya chanzo cha ndani ili kuboresha huduma za Mipango miji, elimu, ustawi wa jamii, afya, mapato pamoja na usimamizi wa miradi ya maendeleo . Magari haya yatasaidia sana kuleta maendeleo na vilevile kukuza mapato ya ndani. kwa pamoja tunajenga lipa kodi kwa maendeleo ya Kinondoni (tuulize info@kinondonimc.go.tz)

No comments: