Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akiwa na mke wake Ester Sumaye wakati wa mkutano huo wa kutangaza nia.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (kulia), akizungumza na wanahabari na wadau wengine wakati akitangaza nia hiyo.
Waziri Mkuu mstaafu Sumaye (katikati), akiwa meza kuu. Kutoka kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kiluvya, Juma Semendu Nauchiwa. Kada wa CCM, Shabani Uronu, Mama Ester Sumaye na Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo, Charles Kaenja.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu Bwana FREDERICK SUMAYE amesema akiteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya urais na kupewa ridhaa hiyo, kipaumbele cha serikali yake ni kuimarisha uchumi.
Akitangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, Bwana SUMAYE ameyataja mambo mengine atakayoyapa kipaumbele kuwa ni kuimarisha elimu,kilimo,kulinda viwanda kwa kuboresha kilimo pamoja na kupambana na rushwa na ufisadi na kusisitiza kuwa ataunda mahakama maalum ya kushughulikia kesi za rushwa ufisadi na uhujuju uchumi.
Amesema uchumi wa nchi ukiimarika utawezesha mengine kuimarika ikiwemo elimu, kilimo, afya na kupunguza tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho.
Pia amesema kuwa kupenda na kuwa kumbatia wala rushwa bila maamuzi mazito niswala ambalo halikubaliki na yeye hawandi na anawachukia kwa nguvu zote,kwani kumkumbatia mlarushwa nisawa na kuchanganya Maji na mafuta jambo ambalo ni vitu viwili tofauti.
Kuhusu suala la maslahi ya taifa si la mchezo mchezo kama wanaojinadi kuwa watamaliza matatizo mbali mbali ikiwemo rushwa yenye harufu kali,swali analojiuliza wakati wapo ndani ya uongozi wameshindwaje kumaliza tukiwapa muongo wakuongoza taifa wataweza?amesema hilo sijambo jepesi na atashangaa kama chama kitateua mtu yeyote mwenye harufu ya rushwa kuongoza taifa yeye atang'atuka na atalipinga vikali kwakuwa haiwezekani mla rushwa aongoze taifa.
Mheshimiwa Sumaye anasema hivi,Nimekumbanana mambo magumu katika miaka hio
kumi ikiwemo ajali ya MV Bukoba na ajali ya treni, ukame wa mwaka 1997.
Niliunda kamati ya kushughulikia jambo hilo na kuchimba visima zaidi ya 300 Dar
es Salaam.
Mambo magumu yalinikomaza katika uongozi. Mvua za El nino zilifata
baada ya ukame, ilikuwa hali ya hatari lakini tulijikwamua na tuliendelea na
kazi wa kujenga taifa letu. Kifo cha baba wa taifa, mimi sikulala siku tatu
nzima hata kwa nusu saa, sijawahi kuona kipindi cha amani kama kili, polisi
waliripoti hata uhalifu haukuwepo.
Wakati waziri mkuu, sikuweza kusikia watu wanapigana,
asubuhi nisiwepo pale, leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita sasa.
Mfano mgogoro wa waancholi na wahadzabe.
Huwezi kuzungumzia amani wakati watu wana njaa, tatizo la
uchumi, watu wanaangalia takwimu badala ya uhalisia.
Tunatakiwa tuendeleze
kilimo, hata wakati wa Nyerere tulileta matrekta lakini tuliendelea? Kuleta
matrekta ni jambo jema sasa nitalima heka 50, lakini uwezo wa mbegu heka 3 na
kupalilia heka 3.
Eneo lingine muhimu ni masoko, lazima kiendelezwe katika
ukubwa wake. Wakulima watauza kwa bei ya hasara na bei ikiwa vizuri hawana tena
mazao. Leo viwanda vya sukari, hatuwezi kuingiza sukari kutoka nje bila kodi,
lazima tulinde viwanda vyetu vya ndani. Mazao yetu yote, kama tutakua na juhudi
za kusindika mazao, hili tatizo la ajira ambalo tunapiga nalo kelele sana,
litapungua. Pia pengo kati ya walionacho na wasio nacho litapungua.
Nimeona shule binafsi wanafanya vizuri, wanataka
wazipunguze nguvu, ongeza juhudi nawe umfikie. Katika miaka miwili au mitatu
tutapunguza kwa kiasi kikubwa wanaoenda nje.
Rushwa na ufisadi, hili jambo sina utani nalo. Ukituhumiwa
kwa rushwa ndani ya wiki moja unachunguzwa na wiki mbili mahakama imekuhukumu
na kama ni viboko unapokea kabisa.Kaulimbiu yake ya uongozi ni Komesha Rushwa,
Imarisha Uchumi.
No comments:
Post a Comment