Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limeweka mikakati madhubuti ya kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya
jiji la Dar es Salaam ili kuwawezesha wananchi kusherehekea Sikukuu Kuu ya IDD
EL-HAJI itakayosherehekewa leo 25/09/2014 kwa amani na utulivu.
Katika kuhakikisha haya yanafanyika kwa
weledi mkubwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kutekeleza yafuatayo:
·
Kutakuwa na
ulinzi wa kutosha kwenye nyumba zote za ibada hususani katika misikiti na
maeneo mengine yenye mikusanyiko inayohisiana na siku kuu hiyo.
·
Kushirikiana na
vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi cha Zimamoto
na uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya uokoaji wakati wa majanga, na
vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya
uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.
·
Limepanga
kutumia kikosi maalum cha intelijensia ili kukusanya taarifa zote muhimu ambazo
zitasaidia kuzuia matukio au mipango ya kufanya matukio ya uvunjifu wa amani.
·
Tumejipanga
kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya
washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho
kitakuwepo. Pia askari wa kawaida (GD), askari wa Usalama Barabarani, n.k
watakuwepo kila mahali. Wote hawa wamepewa maagizo maalum ya kuchukua hatua
kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na sio kungoja tukio lifanyike. Kwa
mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani litashughulikiwa bila
kuchelewa.
·
Zitakuwepo doria
za Miguu na doria za pikipiki katika
barabara zote muhimu.
·
Wananchi wanashauriwa
kusherehekiea siku ya IDD EL-HAJI katika ngazi ya familia au kukusanyika katika
mitaa wakisherehekea kwa amani na utulivu.
·
Aidha kutokana na sababu za kiusalama na matishio
mbalimbali katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jeshi la Polisi limepiga marufuku
disko toto katika kumbi mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi
viwango vya kiusalama.
·
Wananchi
wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe taarifa mapema
iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili hatua zichukuliwe kwa
haraka.
·
Aidha, madereva
wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na
kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, kutoendesha vyombo hivyo wakiwa
wamelewa, magari au pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo ni
marufuku.
·
Aidha, Kikosi
cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria kwenye fukwe za Bahari na
maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam.
·
Polisi watatoa
ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya Polisi vya muda
vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa msaada wa haraka pindi
unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi
wanasherehekea kwa amani.
“TII SHERIA BILA SHURUTI”
NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL-HAJI - 2015
No comments:
Post a Comment