Viongozi wakuu wa umoja
wa katiba ya wananachi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Democrasia
na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE pamoja na makamu mwenyekiti wa CHADEMA
Profesa SAFARI na kaimu mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni
mbunge wa bunge la Africa mashariki Mh TWALHA TASLIMA leo jioni wamehudhuria
Baraza la kuu la idd lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam Tanzania shughuli
iliyofanyika katika hotel ya LAMADA Jijini Dar es salaam.
Katika shughuli hiyo
ambayo iliambatana na dua mbalimbali pamoja na hotuba za viongozi mbalimbali
pia walialikwa wagombea urais wa vyama vyote Tanzania lakini hakuna hata mmoja
aliyeweza kufika huku mgombea wa UKAWA akiwakilishwa na Mh FREMAN MBOWE.
Mh mbowe alipata nafasi
ya kutoa Hotuba fupi ambayo iliwagusa mamia ya waislam ambao walikuwa katika
shughuli hiyo na hapa nimekunukulia baadhi ya mambo ambayo mbowe aliyazungumza
na kushtua wengi
1-Nashukuru sana kwa
ukaribisho wa shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD LOWASA alitamani kuwa nasi
jioni hii lakini kutokana na ratiba ya kampeni kubana imebidi aunganishe kwenda
kwenye kampeni za kesho huko manyara--MH MBOWE
2-Swala la mashekh
ambao wapo jela bila hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi wa kampeni na
tunaendelea kusema kuwa tumewaagiza wanasheria wa chama chetu kufwatilia kwa
makini na kuona nini hasa kimetokea kwao kama kuna mahali kunahitajika msaada
wa kisheria tupo tayari kulishuhulikia hilo kwani sisi lengo letu ni kurudisha
umoja na mshikamano Tanzania. --MH MBOWE
3-Zimebaki siku
takribani 30 sasa kabla ya watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda wa maamuzi
ndugu watanzania. --MH MBOWE
4-TANESCO imefilisika
na watanzania wengi hawajui hili,sasa shirika la umeme halina hata sent na
wameamua kufanya mgao wa kimya kimya lakini ukweli ni kwamba huu mgao ni mkubwa
sana huko tuendako kwa sababu hawana hela na wanaficha ukweli,kuna mgao mkali
sana sasa wa kimya kimya na utaendelea kuwa mkali kadiri siku zinavyokwenda. --MH MBOWE
5-Kuna wizi mkubwa sana
wa mafuta Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa wanauratibu wizi huo,Tanzania
ina akiba ya mafuta hadi mwezi wa 11 lakini serikali imetoa hati ya kuingiza
mafuta nchini ambapo baadhi ya wahusika ni familia ya Rais KIKWETE. --MH MBOWE
6-Serikali yetu ya
awamu ya tano sio serikali ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni serikali ya
kuwarudisha watanzania pamoja kwa maridhiano,na maelewano,ila kuna watu itabidi
washughulikiwe kwa mijibu wa sheria kutokana na kuligharimu taifa hao tutafanya
hivyo. --MH MBOWE
7-Tume ya uchaguzi ya
miezi miwili iliyopita sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo ila watendaji wengi
wameondolewa bila sababu za msingi. --MH MBOWE
8-Mtendaji mmoja mkuu
wa tume juzi tumepata taarifa kuwa ameondolewa na kupelekwa kusikojulikana na
amerudhishwa na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja. --MH
MBOWE
9-Tume ya sasa
inaongozwa na wanajeshi na usalama wa taifa,mimi mbowe ndio nasema kama kuna
mtu anabisha waje wanikamate leo,hatuwezi kuvumiliana kiasi hiki ni wakati wa
kuwekana wazi ili watanzania wafanye jambo wanalolitaka. --MH MBOWE
10-Nasema hivi
hatutakubai hujuma hizi ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi mwisho. --MH MBOWE
11-Mwisho kabisa nasema
hivi ni wajibu wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda kura hivyo ndugu zangu
waislam nawaomba tushirikiane katika hili,ASANTENI KWA KUNISIKILIZA--MH MBOWE
|
No comments:
Post a Comment