Na Exaud Mtei (Msaka
Habari)
Umoja wa katiba ya
wananchi Tanzania UKAWA leo umeitaka taasisi inayijihisisha na maswala ya
midahalo na tafiti mbalimbali TWAWEZA kuandaa mdahalo wa wazi na umoja huo kwa
ajili ya kuichambua na kuitetea tafiti yao waliyoitoa hivi majuzi inayoonyesha
kuwa chama cha mapinduzi kina nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Akizungumza na
wanahabari kuhusu kile alichikiita kuwa ni utafiti wa kupikwa kwa maslahi ya
watu mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA amesema kuwa TWAWEZA kama Taasisi
inayojihusisha na uandaaji wa midahalo na kufadhili midahalo mbalimbali
inayohusiana na uchaguzi mkuu wanawataka kuitisha mdahalo baina yao na viongozi
wa umoja huo kwa ajili ya kuitetea taarifa yao hiyo.
Akizngumzia Taarifa
hiyo ya TWAWEZA mh MBATIA amesema kuwa ni jambo jema kwa taasisi hiyo kushiriki
katika maswala ya kukuza Democrasia ya Tanzania lakini wamepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa iliyotolewa na taaisis hiyo kutokana na kuonekana ina mapungufu
mengi ya wazi ambayo hata mtu ambaye hajasoma anaona wazi kuwa ni utafiti wa
kupikwa kwa ajili ya maslahi ya chama cha mapinduzi.huku akisema kuwa taaarifa
hiyo inaonyesha wazi jinsi gani taasisi hiyo inatumika vibaya na chama cha
mapinduzi kwa ajili ya kuwaahadaa wapiga kura na kawaaminisha kuwa chama cha
mapinduzi bado kina uwezo wa kushinda.
Mh mbatia amesema kuwa
pamoja na Taarifa zote lakini ni wazi kuwa taarifa hiyo imejaa
propaganda,ambazo moja kwa moja zimelenga kukisaidia chama cha mapinduzi ambapo
amesema kuwa jambo hilo limeidhalilisha sana taasisi hiyo.
Amesema kuwa kuna
kasoro nyingi ambazo zipo katika utafiti huo na kufanya watanzania kupuuza
utafiti huo huku akizitaja kadhaa kuwa ni –
1-Waliotafitiwa walipewa
simu za bure na watoa utafiti,ambapo katika taarifa hiyo imeandikwa kuwa simu za mkononi pamoja na chaja,zinazotumia chaji mwanga wa
jua ziligawiwa kwa kaya shiriki.
2-Watafiti wenyewe
wanaonekana kudhani kuwa UKAWA ni chama ambapo katika ukarasa wa kwanza wa
taarifa hiyo mgombea anayewakilisha ukawa ni EDWARD LOWASA.
3-Kutothamini kwa
usawa,michango,ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huu mkuu,vyama kama
ADC,CHAUMA,NLD,NRA,na UPDP havikuwekewa takwimu za moja kwa moja ambapo
vilihesabika kama vyama vingine.
4-Kuorodhesha vyama
visivyokuwa na wagombea Urais katika swali la kuchagua Rais kwa mfano
CUF,NCCR-MAGEUZI.
5-Maana ya UKAWA ni “Walinzi
wa katiba ya wananchi”ndivyo utafiti unavyoeleza katika uk 11 aya ya kwanza.
6-Jumla ya asilimia kwa
wima kutokuwa 100,katika kila jedwali kwenye ukurasa wa 8,9 na 10 kwa mfano
kwenye jedwali ukurasa wa 8,jumla nya asilimia chini ya mwaka 2013 ni 82badala
ya 100,kwenye jedwali la ukurasa 9,ujumla cjhini ya mwaka 2015 ni 102,kwenye
jedwali la ukurasa wa 10 jumla chini ya mwaka 2014 ni 85
7-Mtafiti hawezi
kutafiti kitu anachokijua ambapo katika ukurasa wa 10 imeandikwa ikumbukwe kuwa UKAWA
imejumuishwa katika kielelezo hiki ili kuonyesha kuwa wananchi wanadhani kwamba
UKAWA ni chama ,UKAWA haijasajiliwa kama chama cha siasa
8-Majumuisha ya Matokeo ya utafiti
hayaendani na maswali ya utafiti kwa mfano katika ukurasa wa 7 swali ni Je
uchaguzi ungefanyika leo ungempigia kura mgombea wa chama gani,wakati jumuisho
la tafiti huo linasema kuwa CCM ndio chama nkinachopendwa zaidi na wanaowaunga
mkono CHADEMA wamepungua kidogo tangu mwaka 2013.
9-Kauli
nyingi zinakinzana mfano\
(A)
Katika
ukurasa wa 12 imeandikwa kuwa utafitri huu sio utabiri
lakini katika majumuisho katika ukurasa wa 15 imeandikwa kuwa “karibu wananchi
wote 99% wanasema kuwa watapiga kura katika”
“Zaidi
ya 60% walisema kuwa wantamchaguz mgombea wa CCM wa Urais,ubunge na udiwani”
“26%
ya wananchi watamchagua kwa sababu hii..
“Chanzo cha takwimu wahojiwa hawakupatiwa orodha ya kuchagua
Mh
MBATIA amesema kuwa kutokana na maswala hayo yaliyojitokeza ni wazi kuwa
utafiti huo hauna nia njema kwa uchaguzi wa mwaka huu,huku akiwaomba watanzania
pamoja na wapenda maendeleo na mabadiliko kutoitilia maanani Taarifa hiyo na
kuwataka watanzania waendelee kuilinda na kuitunza amani kwani tafiti kama hizo
za kupikwa zinaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani kwa watanzania.
No comments:
Post a Comment