Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na
maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi
ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere, Abuu Mvano.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa
Jeshi la Polisi, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere kukagua shughuli zinazofanywa na Idara za Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP
Martin Otieno.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watendaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani waliopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere na Waandishi wa Habari wakati wa ziara yake aliyoifanya
kutembelea Idara za Wizara hiyo zilizomo katika Uwanja huo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisalimiana na
Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro
alipotembelea Kituo cha Polisi Buguruni wakati wa ziara yake katika
Kituo hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (katikati),
akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea Uwanja
huo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin
Otieno.
Mkuu wa Ofisi ya Uhamiaji katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Abuu Mvano (kulia),
akiongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni (kulia), alipotembelea Idara za Wizara hiyo
zilizopo katika Uwanja huo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment