Vijana nchini
wametakiwa kuwajibika katika kukidhi maitaji yao ya kimaisha ili kutatua
changamoto zinazowakabili katika maisha yao na jamiii kwa ujumla.
Akizungumza
katika mkutanano wa maadhimisho ya miaka 71 ya UN ,Ndugu alvaro rodriguez
amesema ongezeko la vijana na mahitaji yao ni moja ya changamoto hapa nchini
wanawajibika katika kujiendeleza nakuendeleza taifa ilikupata maendeleo chanya
katika maisha yao, ilikufanikisha hayo vijana wanahitajika kuhakikisha kuwa na
ufahamu na taaluma ili kuwezesha mabadiliko ya uchumi nchini.
Pia vijana
wasisahau wao ndio chachu ya amani ha maendeleo ivyo wao kama umoja wa mataifa
watashirikiana na vijana kuhakikisha wanakuwa wadau wakanuni na taratibu
zilizosababisha kuwepo kwa umoja wa mataifa ili kuakikisha hakuna kijana
anayeachwa nyuma katika maendeleo.
Aidha wamechukua
hatua kuhakikisha vijana wanajua na kutambua malengo ya dunia uku ikiwa hivi
sasa vijana zaidi ya elfu kumi wanatambua malengo hayo ivyo umoja wa matiafa
unatengemea kuelimisha vijana wapatao elfu 50 ifikapo mwaka 2017 pia mashirika
ya umoja wa mataifa yametengeneza program maalumu zinazohakikisha vijana
hawaachwi nyuma katika kuendeleza fikra na utendaji utakao leta mabadilikiko
kiuchumi ifikapo mwaka 2030.
No comments:
Post a Comment