Sunday, January 1, 2017

NAIBU SPIKA AONGOZA MKESHA MKUBWA WA KITAIFA 2017 KWA NIABA YA RAIS DK.JOHN MAGUFULI UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAM

Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
Maombi yakiendelea.
Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.
Shamrashamra za kuupokea mwaka mpya.
Mwaka mpya wa 2017 ukipokelewa.
Wananchi wakiwa wamelala wakisubiri kuupokea mwaka mpya.


Na Dotto Mwaibale

NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amesema Tanzania mpya na yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo akamataka kila mmoja wetu kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.

Dk.Akson aliyasema hayo kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

"Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana" alisema Akson

Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha huo mkubwa ulioandaliwa na makanisa mbalimbali ya kiroho.

Akinukuu baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu ataiponya nchi iwapo kila mtu atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha na kuomba na kuziacha njia mbaya.

"Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu" alisema Akson.

Mratibi wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi mikoa 17 hapa nchini imekuwa ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa ajili ya kuwaombea viongozi wa nchi na taifa kwa ujumla.

"Mungu amekuwa akijibu maombi yetu tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu tulipoanza jijini Dar es Salaam mwaka 1997" alisema Malesi.

Alisema tangu wakati huo wamekuwa wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na ufisadi na kumpata Rais atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo amepatikana Rais Dk.John Magufuli ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo mpya.

Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.

Mkesha huo uliopambwa na nyimbo kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam na Brass Band ya Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka nchi za jirani za Rwanda na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa nchi kuwa na amani.



No comments: