Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP siku ya jana tarehe 30 mwezi
juni umefanya semina fupi iliyofanyika maeneo ya Kimara kibo iliyokutanisha
baadhi ya wakazi wa kata hiyo lengo likiwa ni kujadili ukatili wa kijinsia uliopo
kwenye kata hiyo.
Bi. Agness Lukani akiongoza semina ya ukatili wa kijinsia kwa wakazi wa Kimara Kibo iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam |
Akiongoza semina hiyo iliyodumu kwa takribani masaa mawili dada
Agness Lukani aliweza kuibua changamoto mablimbali zinazowakabiri watoto wa
kike pamoja wanawake kwa ujumla kutokana na ukatili wa kijinsia. Baadhi ya
vijana waliweza kuainisha baadhi ya vitendo vya ukatili vinavyopatikana katika
eneo hilo na miongoni mwake ni.
Baadhi ya vijana walioudhuria semina ya ukatili wa kijinsia wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa kwa njia ya Televisheni mapema jana Kimara Kibo jijini Dar es salaam |
Vijana wengi kutelekeza familia zao hii inaonyesha ni sababu
kubwa kwa wakazi wa eneo la kibo kwa kuwa unakuta kijana anampa mimba binti na
hatimaye kukimbia hivyo kumuacha binti huyo kuishi na mimba hiyo kwa tabu mpaka
anapojifungua na baadae akiona mtoto kamekua anakuja kudai mtoto wake.
Kupigwa kwa wanawake pia ni miongoni mwa aina nyingine ya
ukatili ambayo inapatikana kwenye eneo hilo na mara nyingi unakuta ni wivu wa
kimapenzi hii inasababisha mtoto wa kike kupigwa kwa maana nakuwa hana uwezo wa
kupigana na mwanaume na mwisho binti anakaa kimya pasipo kutoa taarifa popote hali
inyofanya kitendo hicho kuwa endelevu cha yeye kupigwa kila siku.
Tatizo la mimba za utotoni pia limeendelea kuwepo kwa
wanafunzi na wasiwanafunzi kutokanana maeneo waliyopo kuwa ni mjini lakini pia
shule kuwepo mbali, na uwepo vijiwe vya vijana wasio na maadili mazuri kuendelea
kuwarubuni watoto hao kwa kigezo cha kutojua kuwa ni wanafunzi.
Tatizo lingine ni kupiga watoto kupita kiasi hii nayo imeelezwa
kuwa ni miongoni mwa ukatili unaopatikana eneo hilo, pale ambapo unakuta mtoto anakosea
mzazi anashindwa kumkanya au kutafuta njia mbadala ya kumrekebisha na kuona
suruhu kwake ni kumpiga hali inayofanya kumuumiza mtoto na sio kumrekebisha
kama anavyodhani.
Baadhi ya mabinti walipaza sauti zao na kusema kuwa wanaume
wao huwa wanashindwa kuweka usawa na kuwanyanyasa wao kwa kigezo cha kuwa na
hali ni ngumu na kuwaomba wenzi wao wavumilie, Lakini inapotokea wamepata pesa
nyumbani hawaonekani, na ikitokea wamerudi nyumbani wakiwa wamelewa hali
inayowanfanya kushindwa kuwaelewa wakati wanakuwa pamoja kwenye shida ila raha
wanakula na wengine.
Baada ya kupata mafunzo yaliyotolewa kwa kupitia Televisheni ilifikia muda wa majadiliano, kujadili walichojifunza kupitia kipindi walichokiangalia kwenye Televisheni |
Na mwisho wakazi hao wa kibo waliweza kuafikiana kuwa
waadilifu kwa familia zao na kumchukulia mtoto wa mwenzako ni wakwako kuweza
kumkanya endapo atakosea ili kuweza kupunguza mimba za utotoni na aina nyingine
za ukatili wa kijinsia. Na kuendelea kupongeza jitihada zinazofanywa na mtandao
wa jinsia TGNP kuwapa elimu ya kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia.