MATOKEO ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Siha yameanza kubandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel akiongoza kwa mbali katika baadhi ya vituo.
Katika matokeo hayo, Dk Mollel anafuatiwa kwa mbali na mgombea wa Chadema, Alvis Mossi huku wa CUF, Tumsifuel Mwanri akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.
Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo.
Kituo cha Kirua–Kawate Kata ya Siha
Wilaya ya Siha mgombea wa CCM kura 208
Alvis wa Chadema akipata kura 42
Mwanri wa CUF kura 10.
Katika kituo cha Lawate namba 2 Kata ya Siha
CCM kura 300
Chadema 21
CUF 0.
Kituo cha Lomakaa,
CCM ilipata kura 190,
Chadema 10 na CUF haikupata chochote.
Pia kituo cha Ofisi ya Kijiji Sanya Juu,
CCM ilipata kura 284,
Chadema 54 na CUF 1.
Kwa upande wa kituo cha Sanya Juu
CCM ilipata kura 93,
Chadema 50,
CUF 0,
Huku kituo cha Kaboko Kusini 2
CCM 403
Chadema 68
CUF na Sau zikiwa hazijapata kitu.
Pia Kituo kingine cha Kaboko B;
CCM 106
CUF 76,
Sau 0 na kituo cha Ofisi ya VEO Merali Juu1;
Chadema 33,
CCM 64
CUF na Sau vikiwa havijapata kitu.
Ofisi ya VEO Merali Juu2:
Chadema 22
CCM 87.
Endelea kufuatilia matokeo zaidi hapa.
No comments:
Post a Comment