Monday, April 6, 2015

MAGAZETINI LEO JUMANNE APRIL 7,2015 YAKO HAPA YOTE KWA UNDANI

MATOKEO YA SIMBA NA KAGERA SUGAR YAKO HAPA




Timu ya Simba SC klabu imeibamiza bao 2-1 timu ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Mtanange huo ulitarajia kufanyika siku ya Jumamosi iliyopita lakini kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya baada ya maji kujaa uwanjani mchezo uliahirishwa.

Simba SC imejipatia bao la kwanza kipindi cha pili katika dakika ya 52 kupitia kwa mchezaji wake Ramadhani Singano,dakika ya 64 Kagera Sugar wakasawazisha bao kupitia kwa mchezaji wake Rashid Mandawa lakini dakika ya 71 Emmanuel Okwi akaipatia Simba bao la pili kwa njia ya penati.

Mchezo umeisha Kagera Sugar wanaonesha kutoridhika na matokeo vurugu za aina yake zimejitokeza lakini hali imetulia

PICHA 40-KAMA ULIKOSA UHONDO WA TAMASHA LA PASAKA JANA HIZI HAPA ZOTE-MEMBE NAYE ALITOA NENO

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.
…….
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akiwapungia watu waliohudhuria katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe. Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Mkewe.
Watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akitoa vyeti vya shukrani kwa vyombo mbali mbali  vya habari vilivyoshiriki kwa miaka kumi na tano katika kulitangaza tamasha la Pasaka.

Sunday, April 5, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRIL 6,2015,YAKO HAPA YOTE KWA UNDANI


DSC00984


DSC00965

VIJANA WA CCM WALIVYOAMUA KUISHAFISHA KAWE

Wanafunzi kutoka Shirikisho la elimu ya vyuo vikuu ambao ni makada wa chama cha Mapinduzi(CCM) mwishoni mwa juma hili  wamejitokeza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Kawe  jijini Dar es salaam.

Akizungumzia operesheni hiyo Mwenyekiti wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu  Iman Matabula amesema kuwa wamefanikiwa kupanda miti takribani 500, kufanya usafi katika zahanati ya  Kawe pamoja na shuke ya msingi ya tumaini ambayo kuhistoria nidio shule ya mwisho ya mama salma kikwete kufundisha kabla ya kuwa first lady wa tanzania,na kufanya usafi katika maeneo ya masoko yaliyopo kawe  pamoja na kuzungumza na wananchi.
Kwa upande wa  mambo waliyozungumza na wananchi ni kuhimiza wajitokeze katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja kuwahimiza kuhakikisha kuwa  wanalirejesha jimbo la Kawe lililokuwepo mikononi mwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo Chadema.
Vijana hao pia walitoa misaada mbalimbali ikiwemo sabuni na vitu kama hivyo katika zahanati ya kawe na katika shule ya msingi tumaini waliahidi kuchangia tofali 500 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika shule hiyo..
TIZAMA PICHA ZA TUKIO NZIMA HAPO CHINI

DIWANI WA CCM HUKO KIJICHI AWAKUNA VIJANA,ADHAMINI LIGI YENYE DHAMANI YA MILLION 35

Diwani wa kata ya mtoni kijichi CCM mh ANDERSON CHALE kulia akimkabidhi jezi mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM katika kata hiyo bwana ABDALAH LIMBANGA ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ligi ya mpira wa miguu katika kata hiyo ligi itakayojulikana kama UVCCM KIJICHI CUP ambayo yanatarajiwa kuanza takribani wiki mbili zijazo,picha ya chini inaonyesha akimkabidhi mipira ambayo imetolewa kwa kila timu kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ligi hiyo

  Diwani wa kata ya mtoni kijichi mh ANDERSON CHALE leo amekabidhi vifaa vya michezo mbalimbali kwa timu 50 katika kata hiyo kama maandalizi ya ligi itakayoendeshwa katika kata hiyo na kujulikana kama UVCCM KIJICHI CUP.
Vifaa ambavyo vimekjabidhiwa kwa timu hizo ni jezi,ambapo kila tiku moja imepoatiwa jezi pamoja na mpira mmoja ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza baada ya wiki mbili na kuendeshwa na kata ya mtoni kijichi kwa kudhaminiwa na diwani huyo.
Mh diwani ANDERSON CHALE akionyesha pikipiki ambazo ni moja katika zawadi za washindi wa ligi hiyo,ambapo picha za chini zinaonyesha akimkabidhi pikipiki hizo mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM kwa ajili kabisha ya kushindaniwa katika ligi hiyo.
 Akizungumza na washiriki wa mashindano hayo ya mpira wa mguu mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM katika kata hiyo ndugu ABDALAH LIMBANGA amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu hamsini ambapo kila mtaa katika kata hiyo umetoa timu kumi kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo.
Amesema kuwa katika ligi hiyo ambayo inakadiriwa kutumia jumla  ya million 35 hadi kukamilika kwake washindi watapewa zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza ataondoka na pikipiki,jezi pea mbili pamoja na kombe ambapo mshindi wa pili na watatu watapata zawadi kemkem ikiwemo pikipiki moja kwa kila timu.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo diwani huyo amesema kuwa amesukumwa kudhamini mashindano hayo baada ya kugundua kuwa katika kata yake kuna vijana wengi na wanahitaji umoja ili waweze kujiletea maendeo na njia aliyoona ya kuwaunganisha kwa pamoja ni pamoja na kuanzisha mashindano kama hayo kwa lengo la kuwakutanisha vijana hao.


WAIRI MKUU PINDA AFIWA NA BABA MKWE WAKE

Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa pole kwa familia ya Marehemu akiwemo mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) ambaye alifiwa na baba yake Mzazi, Mzee Abdallah Rehani , Nyumbani kwa marehemu,Tabata jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015 . Wengine pichani ni ndugu wa karibu wa Mama Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mazishi ya babamkwe wake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015. Kushoto ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad.

Saturday, April 4, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA PASAKA

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SIMBA SC


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia vifo vya mashabiki wa klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani eneo la Makunganya mkoani Morogoro.



Katika salamu zake Rais Malinzi amesema, TFF imezipokea kwa masikitiko taarifa hizo za ajali na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wanawapa pole wafiwa wote na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze kupata nafuu na kupona kwa uharaka zaidi.

Aidha Rais  Malinzi ameagiza michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itakayochezwa  wikiendi hii nchini, kusimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

LIVE TOKA UWANJA WA NDEGE DAR-REBECCA MALOPE AWASILI KWA AJILI YA TAMASHA LA PASAKA KESHO

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini Africa ya kusini REBECCA MALOPE  usiku huu amewasili katika uwanja wa ndege wa mwalimu nyeere kwa ajili ya kutumbuiza katika onyesho la miaka 15 ya tamasha la pasaka linalotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa Dar es salaam mchana.
akizngumza na mtandao huu MALOPE amesema kuwa amefurahi sana kiuwa nchini tanzania kwa mara ya tatu sasa kutumbuiza katika tamasha hilo na anawaahidi watanzania watakao fika kesho kupata burudani isiyo na kiifani

Naye mkurugenzi wa MSAMA PROMOTION ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo ALEX MSAMA amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi kwani watapatiwa burudani ya aina yeke katika tamasha hilo.Kwa mujibu wa Alex Msama, sambamba na Malope, Afrika Kusini wanatarajia kutoka waimbaji wengine wawili ambao ni Solly Mahlangu na Sipho Makabane.
Msama alisema waimbaji wengine waliokubali kutumbuiza kwenye tamasha hilo ni pamoja na Ephraim Sekeleti, Solomon Mukubwa, Upendo Nkone na Bonny Mwaitege,

Friday, April 3, 2015

TBN WAMWANGUKIA RAIS SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO ILIYOPITA BUNGENI

Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni.
Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

KWA MUJIBU WA TCRA ASILIMIA 100 YA TANZANIA SASA IMEKUWA NI DIJITALI

 
 Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa Televisheni kwa mfumo wa Analojia kwenda Dijitali ambapo asilimia 100 ya nchi sasa imekuwa Dijitali. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala na Ofisa wa Masafa, Christopher Asenga.
  Ofisa wa Masafa wa TCRA, Christopher Asenga (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TCRA, Semu Mwakyanjala
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano ukiendelea.  

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

FAHAMU KWANINI GWAJIMA HAKUHOJIWA JANA NA POLISI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum halikuweza kumhoji Askofu Josephat Gwajima ili kumpa fursa afya yake iimarike zaidi. Askofu Gwajima alifika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati yalipo Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum akisindikizwa na wasaidizi wake ikiwa ni pamoja na wakili wake majira ya saa mbili na nusu asubuhi.

Alifika kituoni akiwa bado anatumia kiti cha magurudumu matatu (wheel chair) na alikubaliana na wapelelezi kwamba akaendelee na matibabu na anatakiwa arudi kuripoti tarehe 09/04/2015 ili aweze kuendelea na mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu na kumtukana Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM