Thursday, September 3, 2015

Tizama kiingio cha mchezo wa Stars Jumamosi na sehemu ya kupata Tiketi


Maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria (Super Eagles) yamekamilika, ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa jumamosi kati huku kiingilio cha chini kabisa kikiwa shilingi elfu saba tu.

NGASA, ULIMWENGU, SAMATTA WAJIUNGA STARS


Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA WATAALAMU WA HAKI NA SHERIA, JIJINI ARUSHA.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu  Agustino Ramadhan. Picha na OMR

Wednesday, September 2, 2015

MAGAZETI YA LEO TZ,SEPT 3 Sep 3, 2015



Historia ya lowasa leo huko sumbawanga,Tizama hapa

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Ikuo Malila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015. 


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe, akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kizwitwe, Sumbawanja Mjini, leo Sepremba 2, 2015.

Kutoka manzese muda huu,uzinduzi wa kampeni CHAUMA

 Mwananchi aliyevalia nguo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiondolewa na askari polisi baada ya kujipenyeza kwenye uzinduzi wa kampeni za Chama cha Ukombozi Umma (Chauma), uliofanyika viwanja vya Bakhresa Manzese Dar es Salaam leo.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi (Chauma), Dk. Hashim Rungwe, akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika viwanja vya Bakhresa Manzese Dar es Salaam leo.

VIDEO--Mbatia Amlimpua tena DK SLAA leo,Tizama Kila Kitu Hapa

Baada ya jana aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha democrasia na maendeleo chadema Mh DK WILBROAD SLAA kumshambulia mgombea wa UKAWA ndugu EDWARD LOWASA na UKAWA kwa ujumla leo mwenyekiti mwenza wa umoja huo JAMES MBATIA ameibuka na kujibu mapigo ya tuhuma hizo.

Tamko Rasmi la CHADEMA kuhusu DK SLAA LEO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana na vyombo vya habari mbalimbali kutaka kauli yetu kuhusu mkutano wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Willbroad Slaa na waandishi wa habari uliofanyika jana Hoteli ya Serena na kutangazwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na radio, tunapenda kusema ifuatavyo;

MAGEUZI YA MIFUMO KANDAZIMIZI HAYAEPUKIKI-WANAHARAKATI WA TGNP

MWANAFEMINISTI KUTOKA NCHINI NIGERIA. PROF. AMINA MAMA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WANANCHI WALIOHUDHURIA TAMASHA LA JINSIA KWA MWAKA 2015 KATIKA VIWANJA VYA TGNP VILIVYOPO KATA YA MABIBO WILAYA YA KINONDONI JIJINI DARESALAAM,, PROF. AMINA MAMA ALISEMA KUTOKANA NA UCHAMBUZI  WA KIFEMINISTI AMBAO UMEFANYWA KUHUSU SERA ZA SOKO HURIA UMEONYESHA KUWA HAKUNA UHURU WOWOTE UNAOLETWA NA TAASISI ZA KIFEDHA.

Tuesday, September 1, 2015

Lowasa alivyowasili Ruvuma

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA anayeungwa mkono na vyama Vinne vya upinzani UKAWA leo ameendelea na harakati zake za kampeni kwa kuingia Ruvuma ambapo ameendelea kuzinadi sera zilizopo katika ilani ya umoja huo,Hapa zimenifikia picha kadhaa kuhusu matukio hayo

RAIS KIKWETE AAGWA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA

1x
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipowasili katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama leo.
[Picha na Ikulu.]
4x
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (wan ne kushoto) akiwa na Viongozi wengine wakisimama kupokea salamu ya heshma ya kwaride la Vikosi vya Ulinzi wakati wimbo wa Taifa ulipopigwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kuagwa rasmi leo.
2x
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi la Vikosi vya  Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  kumuaga kwa kumaliza muda wake wa Urais leo.
3x
Askari wa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  katika sherehe za kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete alipoagwa rasmi na Vikosi hivyo leo,

TWIGA STARS KUONDOKA KESHO


Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3, mwaka huu.

AMENGOKAA--Dk slaa achafua hali ya hewa upyaaaa,amfumua lowasa na Ukawa yake

KATIBU mkuu wa CHADEMA Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema aliamua kuachana na CHADEMA na siasa kwa ujumla tangu tarehe 28/08/2015 baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowasa kujiunga na CHADEMA, kwa kile alicho dai kuwa asingeweza kushiriki kumsafisha mtu mwenye madhambi na badala yake aliona ni vyema ajiengue kwakuwa yeye sio muumini wa siasa za ulaghai.
Kauli hiyo ameitoa katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, amabapo amesema ameamua kayasema hadharani  kwa kile alicho dai kuna upotoshwaji unao endelea  kuwa yuko likizo na kwamba atajiunga na shughuli za chama hicho mbele ya safari, huku akidai kuwa hakuwa likizo na wala hakupewa barua yoyote ya likizo
Hata hivyo amesema alijaribu mara kadhaa kuandika baraua za kujiuzuru lakini hakuweza kusikilizwa na mtu yoyote, na baadae aliamua kuchukua uamuzi wa kuchana shughuli za chama hicho,  na kwamba uvumi uliokuwa ukiendelea kuwa Slaa amezuiwa na mke wake Josephine
ameongeza kuwa kitendo cha kuwaruhusu baadhi ya wabunge waliotemwa na CCM baada ya kura ya maoni nacho kimechangia kumuondoa katika  chama hicho, huku akimtolea mfano Waziri mkuu wa wazamani Fredrick Sumaye kuwa ndiye mtu ambaye alikuwa na mgogoro nae baada ya kumuita fisadi katika bunge  la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, amabapo na yeye leo hii ameendelea kuwaita ni “MAKAPI” .
Naondoka leo huku nikisikitika kuwa sura ya CHADEMA imebadilika nakuwa kama CCM, sasa utawezaje kuleta mabadiliko nawatu wale wale wanaotuhumiwa na kashfa zinao umiza taifa hili? Alisema Dkt Slaa.
Aidha alimaliza kwa kusema amestaafu siasa ila hana chama chochote ila bado ataendelea kuwatumikia watanzania kwa njia nyingine kwakuwa ana vipawa alivyo barikiwa na mungu lakini amewataka wananchi kuto pumbazwa na shamra shamra zinazo endelea badala yake wananchi wanatakiwa kutambua kazi waliyo nayo kwa sasa.
KUHUSU LOWASA KUHUSIKA NA RICHMOND DKT SLAA AME ANIKA HAYA.
kifungu cha 152 cha katiba ya nchi hii kina sema jukumu kubwa la waziri ndio msimamizi wa shughuri za serikali sasa anawezaje kukataa kuwa yeye hakuhusika?
Na katika makampuni yaliyo omba zabuni ya Umeme mwaka 2006, kampuni ya Ricmhond ndiyo kampuni pekee iliyokuwa na sifa “sifuri” haya yoote anayajua na kama hajui basi alikuwa ni mzembe! na kama alikuwa mzembe basi hafai kuwa Rais. alisema Dkt Slaa.
Na aliagiza tenda ifanyike ndani ya siku 10, wakati sheria ya PPRA ina tamka tenda yoyote inatakiwa ifanyike ndani ya siku 45, ni kinyume na sheria.
Sasa hao wanao mtetea watoke hadharani kama mnaona sisi hatujui chochote, mbona mnata kutu pumbaza!?