Saturday, December 3, 2016

LISU--TUMEBADILISHA MBINU YA KUMKABILI MAGUFULI


Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema kuwa vyama vya  upinzani vimejipanga vizuri kwaajili ya kukabiliana na Rais Dkt. John Magufuli .

Amesema hayo katika Semina iliyowashirikisha viongozi wa vyama vya upinzani kutoka Mataifa 16 iliyofanyika  Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni Jijini Dar es salaam, amesema  wanapambana kuhakikisha  uwanja wa siasa unakuwa sawa lazima wabadili staili ya kumkabili Rais Magufuli.

Jarida la New African lamtaja Rais Magufuli ‘Person of the Year’


magazineHarakati na uongozi wake madhubuti hasa katika kupambana na rushwa, ufisadi na kuhakikisha uwajibikaji mkubwa wa viongozi na wafanyakazi, vimempa sifa kubwa Rais Dkt John Magufuli.

WAMILIKI WA BLOG TANZANIA KUKUTANA WIKI IJAYO,NMB YADHAMINI MKUTANO HUO

Chama cha  Wamiliki/Waendeshaji mitandao ya kijamii nchini (Tanzania Bloggrs Network-TBN) mapema leo Disemba, 2 imekabidhiwa  cheki maalum ya kiasi cha Tsh. Milioni 10, fedha zilizotolewa na  benki ya NMB kama wadhamini wakuu wa Mkusanyiko wa ‘Bloggers’ kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Friday, December 2, 2016

Maneno ya Zitto Kabwe Baada ya kumtembelea Mbunge lema Mahabusu,Sasa anakaa mahabusu hadi mwakani


Leo Ijumaa disemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati Za kutafuta na kulinda Haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa Sana na ukiukwaji mkubwa wa Haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona Ni bora akae ndani Mpaka hapo Dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana.

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka Mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.
Amemshukuru Mungu Kwa kumpa Mke jasiri anayempa moyo na Ndio ngome yake Kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka Haki kutendeka Katika uendeshaji wa Nchi yetu. Siku zote Haki hushinda


Leo December 2 2016 Mahakama kuu kanda ya Arusha imetupa rufaa ya kupinga maamuzi ya kumnyima dhamana iliyoamuliwa na mahakama ya hakimu mkazi dhidi ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema.
Naibu msajili wa Mahakama kuu kanda ya Arusha, Anjelo Rumisha amesema kwamba rufaa hiyo ilikuwa imekatwa nje muda uliopangwa.
Akizungumza baada ya maamuzi hayo, wakili wa Lema, John Malya amesema wameongea na mteja wao na kuwaambia wasishughulike tena na kesi hiyo hadi pale upande wa Jamhuri utakapoamua lakini wao wataendelea kukutana na jopo la mawakili ili kuja na njia mbadala

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM


POLISI DAR YAWAKAMATA WATUHUMIWA SUGU 586


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam limefanya msako mkali kuanzia tarehe 22.11.2016  hadi 02.12.2016 na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 586 wa makosa mbalimbali. Watuhumiwa hao wamekamatwa maeneo mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Wamekamatwa kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu,kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi kutoka maungoni, kucheza kamari, kubughudhi abiria, wizi wa magari, wizi kutoka maungoni, shambulio la aibu na la kawaida, kutengeneza,kuuza na kunywa pombe haramu ya Gongo, uvutaji bhangi nk

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AENDESHA HARAMBEE YA SH.BILIONI 1 KUSAIDIA MFUKO WA UKIMWI NCHIN

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF)  Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akihutubia kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

 Meza kuu.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Salum Mussa (kulia), akishiriki uzinduzi wa mfuko huo na wadau wengine.

Thursday, December 1, 2016

Green Sports Africa Academy kufanya ziara Azam FC


KITUO cha kukuza vipaji cha Green Sports Academy kutoka jijini Nairobi, Kenya kinatarajia kufanya ziara maalumu kwenye makao makuu ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC.

Ziara hiyo ya siku sita itakayoambatana na mechi za kirafiki, itaaanza rasmi Desemba 20 jioni watakapowasili nchini hadi Desemba 25 mwaka huu watakaporejea nchini kwao.
Green Sports itakuja nchini ikiwa na timu zake nne za umri tofauti chini ya miaka 13, 15, 18 na 21, ambapo itacheza mechi tatu za kirafiki kuanzia Desemba 22, 23 na 24 dhidi ya timu za vijana za Azam FC.
Uongozi wa kituo hicho kupitia kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Stephen Ochiel Otieno, umetoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Azam FC kwa kuwakubalia ziara hiyo ya kuja hapa nchini.
Otieno amesema kuwa hiyo itawahamasisha sana vijana wadogo wenye vipaji kuelekea kuwa nyota wa kimataifa katika siku za usoni, huku pia kwa upande wao wakiangalia mbele kuendeleza ushirikiano wa kudumu na Azam FC, ambayo kwa sasa ndio klabu bora iliyowekeza kwa vijana katika ukanda huu.
Huu ni ugeni mkubwa wa pili kwa mwaka huu kwa Azam FC ikihusisha kituo cha kukuza vipaji, wa mara ya kwanza ulikuwa ni mwezi Juni ilipozialika timu mbili za Afrika Mashariki, Football For Good Academy ya Uganda na Ligi Ndogo Academy ya Kenya kwenye michuano ya Azam Youth Cup 2016, ambayo pia iliishirikisha Future Stars Academy ya Arusha na kushuhudiwa wenyeji Azam FC Academy ikitwaa ubingwa wa michuano hiyo

Kama Ulimsahau Scopion Kesi imeendelea leo,Haya ndiyo yaliyojiri


MSHITAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete (34) ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya kareti kutoka chuo cha mafunzo cha Ifakara aliyoyafanya mwaka 1989 hadi 1995.



Aidha, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umemuongezea mashitaka ya shambulio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashitaka.

HII NDIYO IDADI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene amesema kuwa wanafunzi 526,653 kati ya 555,291 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka huu wamechaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwakani katika shule za sekondari za Serikali.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ni sawa na asilimia 94.85 ya wanafunzi wote waliofaulu.

Akizungumza na Waandishi wa habari tarehe 28 Novemba 2016 mjini Dodoma Waziri Simbachawene ameeleza kuwa wanafunzi 28,638 wakiwemo wavulana 12,937 na wasichana 15,701 hawakuchaguliwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi.

MAJALIWA AWASILI ARUSHA

arusha
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Richard Kwitega baada ya kuwasili jijini Arusha kuanza ziara ya kazi mkoani humo Desemba1, 2016.

JK KUZUIWA UWANJA WA NDEGE--SERIKALI YALIPA ONYO KALI GAZETI LA MTANZANIA

Jakaya Kikwete

Kufuatia gazeti la Mtanzania la Novemba, 20 na 22 kuandika habari ambazo zinamhusu Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuwa alizuiliwa kuondoka katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Serikali imetoa taarifa kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Kaimu Msajili wa Magazeti, Patrick Kipangula imesema kuwa taaarifa hiyo haina ukweli na ina nia ya kumdhalilisha Kikwete ambaye aliondoka madarakani mwaka jana 2015 na nafasi yake kuchukuliwa na Rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli.
Hivyo kutokana na kuchapishwa kwa habari hizo, Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Magazeti imetoa onyo kwa gazeti la Mtanzania na kuvikumbusha vyombo vya habari kuzingatia maadili ya uandishi ya habari.
1e504b16-a8c4-4f31-985f-d3bd4f01e8aa

Azam FC kusaka vijana U-17 Kigoma J’mosi hii

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, itakuwa mkoani Kigoma wikiendi hii Jumamosi (Desemba 3, 2016) kusaka vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17).

Huo ni mwendelezo wa mpango wa Kitaifa wa timu hiyo wa kutengeneza kikosi imara cha timu ya vijana wa umri huo, ambapo inakwenda Kigoma kutokana na mkoa huo kuwa historia ya kisoka nchini ya kutoa wanasoka wengi waliotamba.
Majaribio hayo ya pili kuelekea mwisho wa kufungwa zoezi hilo, yatafanyika ndani ya Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Jumamosi hii kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana na vijana wanaotakiwa ni wale waliozaliwa kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.
Mpaka sasa zoezi hilo limeshahusisha mikoa sita, ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma, Visiwani Zanzibar, Mbeya na Mwanza, ambapo kiujumla Azam FC imewafanyia usaili jumla ya vijana 3, 265 na kuvuna 70 pekee kati ya hao waliochaguliwa, huku 151 wakiwekwa akiba kwenye kumbukumbu za mradi huo.
Vijana hao wote waliochaguliwa kwenye mikoa mbalimbali, wanasubiria kuitwa kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika ndani ya Uwanja wa Azam Complex baadaye mwezi huu Desemba, ambao ndio utatoa vijana bora watakaounda timu hiyo.

PUMA YANG'ARISHA UTALII ZANZIBAR KWA MASHINDANO YA NDEGE KONGWE 22

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rubani wa kike mdogo kuliko marubani wote wa ndege ya zamani, Sara Meehan (18), jinsi injini ya ndege hiyo kutoka Botswana inavyofanya kazi, wakati wa mapokezi  ya ndege hizo 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Ndege hizo zilitengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), akisalimiana na rubani wa ndege ya zamani Pedro Langton kutoka Canada, wakati wa mapokezi ya mashindano ya ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), na Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi wakiangalia ndege ya zamani kutoka Canada, wakati wa mapokezi ya mashindano ya ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana.