Sunday, December 11, 2016

WAFANYABIASHARA SOKO LA MADENGE TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM WA JENGA KISIMA KWA NGUVU ZAO

 Fundi Martin Justine akitengeneza paa la kisima cha maji safi kinacho jengwa Soko la Madenge Temeke jijini Dar es Salaam kwa nguvu za wafanyabiashara. Ujenzi wa kisima hicho umegharimu sh.milioni 5.6.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala' akimuonesha mwandishi wa mtandao huu (hayupo pichani), kisima hicho.
 Katibu Mkuu wa Soko hilo, Shaban Jabir Malonji 'maarufu kama Wailala'  akinawa maji yanayotoka katika kisima hicho ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia kubwa.

Azam FC yatoka sare na Mtibwa Sugar


KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex usiku huu.
Azam FC imeutumia mchezo huo kama maandalizi tosha ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), ambapo itaanza kufungua dimba Desemba 18 mwaka huu kwa kuvaana na African Lyon katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, alitumia vikosi viwili tofauti kwenye mchezo huo cha kwanza kikianza kipindi cha kwanza na kingine kikimalizia kipindi cha pili.
Alikuwa ni Enock Atta Agyei, aliyeweza kuipatia bao la uongozi Azam FC kwa mkwaju wa penalti dakika ya 14, kufuatia kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed, kumwangusha ndani ya eneo la hatari mshambuliaji wa mabingwa hao, Francisco Zekumbawira.

Azam FC iliyoonekana kucheza vema kwa soka la kasi kipindi cha kwanza, ilijikuta ikiwaruhusu Mtibwa Sugar kusawazisha dakika ya 28 kupitia kwa nahodha wao, Shaban Nditi na hivyo kufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1.
Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Yahaya Mohammed, aliyeingia dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Agyei, naye alifungua akaunti ya mabao kama mtangulizi wake huyo kwa kuipatia bao la pili timu hiyo kwa shuti la kiufundi.

Kinda wa zamani wa timu ya vijana ya Azam FC, Ibrahim Rajab ‘Jeba’, aliisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 90 kwa njia ya mkwaju wa penalti na kufanya mpira kumalizika kwa sare hiyo.
Tukio la kuvutia kwenye mchezo huo ni mashabiki waliokuwa uwanjani kumpigia makofi ya shukrani winga wa Azam FC, Enock Atta Agyei, wakati akitolewa na kuingia Mohammed dakika ya 61, na hii ni kufuatia konyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo.

Benchi la ufundi la Azam FC, pia liliutumia mchezo huo kuwafanyia majaribio wachezaji wawili kiungo mkabaji Stephane Kingue na beki wa kati, Yakubu Mohamed aliyetokea Aduana Stars ya Ghana.

Kikosi cha Azam FC leo:
Mwadini Ally/Aishi Manula dk 46, Abdallah Kheri/Shomari Kapombe dk 46, Erasto Nyoni/Bruce Kangwa dk 46, Aggrey Morris/Daniel Amoah dk 46, David Mwantika/Yakubu Mohammed dk 46, Jean Mugiraneza/Himid Mao dk 46, Frank Domayo/ Stephane Kingue dk 46, Ramadhan Singano/Salum Abubakar dk 46, Francisco Zekumbawira/John Bocco dk 46, Enock Atta/Yahaya Mohammed dk 61, Joseph Mahundi/Samuel Afful dk 46

Saturday, December 10, 2016

PICHA--ALICHOKIFANYA MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWAN KIKWETE




Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete na mhandisi,Elias anayesimamia uunganishwaji wa mabomba na kufukia mitaro katika mradi wa maji wa Wami-Chalinze wakiukagua

Tizama maadhimisho ya siku ya akimataifa ya Haki za binadamu ilivyoadhimishwa na LHRC Jijini Da es salaam


Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi Hellen Kijo Bisimba , akiwa na  Balozi wa uingereza nchini Tanzania  mh Sarah Cooke wakiwa katika  maadhimisho ya siku ya haki za binadamu yaliyofanyika Makumbusho Jijini Dar es salaam Jana.Picha na Exaud Mtei











Mgeni Rasmi ambaye ni Balozi wa uingereza nchini Tanzania  mh Sarah Cooke akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya haki za Binadamu Duniani yaliyofanyika Jijini Dar es salaam na kuadhimishwa na kituo cha sheria na hakii za Binadamu nchini.
Picha Ya pamoja wakati wa maadhimisho hayo

Viongozi mbalimbali wa Club za LHRC kutoka mashule na Vyuo mbalimbali nchini wakishiriki kwa pamoja kuzindua Report mpya ya hali za Haki za binadamu nchini Report ambayo imeandaliwa na Kituo cha sheria na Haki za binadamu nchini Tanzania LHRC 

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu bi Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanaharakati mbalimbali wa haki za binadamu na wanafunzi  waliojitokeza katika Maadhimisho hayo yaliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Report Mpya ya haki za binadamu nchini

Wanafunzi wakisikiliza kwa makini

Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano nas Mazingira Mhe Luhaga Mpina Zanzibar.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Tume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar Bi Afua Mohammed akitowa maelezo ya utendaji wa Tume hiyo wakati akiwasilisha Ripoti ya Utafiti iliofanywa na Tume hiyo wakati wa ziara ya Mhe Luhaga, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Tume hiyo maruhubi Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akipitia Ripoti ya Tume ya Sayansi na Teknolijia Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tume hiyo ilioko Zanzibar.

UKINYIMWA UNYUMBA NDANI YA NDOA NENDA KASHITAKI DAWATI LA JINSIA POLISI

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Felix Lyaniva (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Felix Lyaniva (Wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho wa  maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha. 
 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Wadau na wananchi wakifuatilia hutuba za mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.

SHEIKH JALALA ATOA NENO KUELEKEA MAADHIMISHO YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD


Ikiwa zimebaki siku chache kufikia maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad Kiongozi wa waislam wa madhebu ya shia Ithnashariya  Tanzania  Shekhe Hemed  Jalala amewataka  watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana hasa wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.


Akizungumza na waandishi wahabari Leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es salaam amesema Mtume Mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza Upendo na amani hivyo nivyema waTanzania  kuishi kwa Upendo bila kujali utofauti wa dini zao.

"Mtu kupenda nchi ni katika amani na pia dini imekuja kutunza upando na amani watanzania tusibaguane kutokana na dini zetu" amesema Jalala.

Hata Hivyo Sheikh Hemed amebainisha kuwa ni vyema jamii kuyaishi maisha aliyoishi Mtume Mohammad ikiwa ni pamoja na sifa kuumbili alizokuwa nazo Mtume ambazo  nikuwa mkweli na mwaminifu.

Sambamba na hayo ameongeza kuwa Kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na watanzania hasa kwa kipindi hiki chakukumbukwa kwa kuzaliwa kwa Mtume ni kuishi kwa amani na ushirikiano kwa kuwa vitabu vyote vya dini vimekuja kuunganisha watu.

Friday, December 9, 2016

Tigo Fiesta Supa Nyota ni Moto na Wasanii watembelea Tigo Shop Songea

Meza ya Majaji wakiongozwa na Chief Judge, Adam Mchomvu (wapili kushoto) wengine toka kushoto ni Chege,Man C na Joh Makini

Wasanii waliongia mchujo wa mwisho utaofanyika jioni ya leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Majimaji, kushoto ni Single Baba na Yatosha.

Msanii Chipukizi aliyeingia Mbili Bora almaarufu, Single Baba akinyanyua mikono juu mara baada ya kutangazwa kupanda jukwaa la Tigo Fiesta jioni ya leo uwanja wa Majimaji Songea, jumla ya wasanii wawili watachuana kumpata mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma.

Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na  washindi wawili nyuma waliosimama na chini toka kushoto ni jaji Man C toka Jogoo Fm, Adam Mchomvu, Chege na Joh Makini.



Baadhi ya wateja wa Tigo wakipokea zawadi toka kwa wasanii mbalimbali

Msanii Ruby akimkabidhi zawadi mteja wa Tigo, Fatuma Komba leo


Wasani watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Majimaji Songea jioni ya leo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Duka la Tigo lililopo mtaa Itundu Songea

Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote Lafana Mjini Songea

Msanii Elias Barnaba akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana


Mr Blue akitoa Burudani kwenye Jukwaa la Tigo Fiesta Songea

Kutoka Temeke Chege Chigunda akiwapa burudani mashabiki wa Tigo Fiesta waliojitokeza uwanja wa Majimaji Songea




Luli Diva Jukwaani

Mkali wa Nyimbo ya Kinanda Messen Selecta  akitoa Burudani

Wasanii waliopanda jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji Songea usiku wa kuamkia jana kwa pamoja wakiweka mishumaa juu kumkumbuka Mtayarishaji wa muziki Joshua Magawa a.k.a Pancho Latino aliyefariki hivi karibu kwenye kisiwa cha Mbudya jijini Dar Es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe.Pololite Mgema akiongea na wanachi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana. Pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme ns Mratibu wa Tamasha hilo Shafii Dauda.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme akiongea na wananchi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.


Mkali wa Wowowo Zaiid akitoa Burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta  Songea.


Likiwa limeingia mkoa wanne Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote limefana na kuacha alama kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani  Ruvuma usiku wa kuamkia jana, Kabla ya kuingia mkoani humo Tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro limepita  mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea na kuelekea Mtwara jumapili hii.

Akifungua Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololite  Mgema alisema Tunawashukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kutuletea tamasha hili kubwa mkoani kwetu. “ Hii si kwa burudani pekee bali ni fursa kwa wakaazi wa mkoa huu kwa kuwawezesha kwa kuwaongezea kipato kwa kipindi hiki chote cha wiki nzima”. Niendelee kuwapongeza tena Tigo  na Clouds Media na kuwaomba mwakani msiache kuja tena kwenye mkoa wetu.

Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumpata mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota kwa kumuibua Msanii Single Baba atakayeiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar Es Salaam mwezi ujao.

Shoo rasmi ilianza kwa Msanii Mesen Selekta kufuatiwa na Rubby huyu ni msanii aliyeibuliwa kwenye Supa Nyota miaka kadhaa iliyopita, kwa kweli ni msanii wa aina yake aliweza kuteka hisia za mashabiki kwa kuimba nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze,Ntade, Na Yule,Forever na nyingine.

Jumla ya wasanii kumi na mbili walipanda jukwaani wakiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid Q, Masen Selekta,  Lulu Diva,Chege, Foby ambao wasanii hao ndio watapanda kwenye jukwaa jumapili uwanja wa Nangw’anda Mtwara.

Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.


Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

RAIS MAGUFULI AWAONGOZA WATANZANIA MAADHIMISHO YA UHURU.

reqNa Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu Dkt. John Magufuli amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara.
Sherehe hizo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es saalam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Sherehe hizo zilipambwa na gwaride, ngoma za asili, wimbo maalumu kutoka vikosi vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jeshi la Magereza na Jeshi la Polisi.
Katika hatua hiyo, kikosi maalumu cha wanamaji kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania walionesha umahiri wao kwa kupita mbele ya Rais huku wakibeba mabegi yenye uzito wa kilo 65 za vifaa vinavyowawezesha kuhimili maisha ndani ya siku saba wawapo katika uwanja wa medani bila kuhitaji msaada wowote.

VIJANA U15 WAMALIZA ZIARA MOROGORO, SASA KUIVAA BURUNDI

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mazoezi  yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
 Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 15, imemaliza ziara Morogoro kwa mafanikio baada ya jana Alhamsi Desemba 8, kuifunga Moro Kids mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa siku ya jana Ijumaa Desemba 9, mwaka huu timu hiyo ilijifua kwa mazoezi kwa mujibu wa programu ya Kocha Oscar Mirambo baada ya Morogoro kuleta timu ya wakubwa tofauti na vijana wenye umri wa chini ya miaka 15. Hivyo, mchezo huo wa pili haukufanyika.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
Kiungo Alphonce Mabula (kushoto), akichuana na Jonathan Kombo wakati mazoezi  yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Mazoezi na michezo hiyo ya kirafiki ambayo mingine wataifanya Zanzibar juma lijalo, ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi mchezo unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, mwaka huu kwenye Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Awali ilipangwa icheze na Shelisheli ambayo imetoa taarifa ya kuwa haijajiandaa.
Mara baada ya Morogoro, timu hiyo imerejea Dar es Salaam leo kujiandaa na safari ya kwenda Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.
Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, Edson Mashirakandi (Katikati) akimtoka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Oscar Milambo (Kulia) kwenye mazoezi  yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.  Kushoto ni beki Rashid Hamis (Picha na Alfred Lucas wa TFF)
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana weeny umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.
Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.
Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma  Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15, Edson Mashirakandi akikokota mpira baada ya kumtoka beki Dastan Matheo kwenye mazoezi  yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Alfred Lucas wa TFF)Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.

Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.

YANGA YAULA WA CHUYA KWA HASSAN KESSY,SASA KUWALIPA SIMBA MAMILIONI HAYA


SUALA LA MCHEZAJI HASSAN RAMADHANI KESSY


Baada ya kupitia mawasilisho ya pande zote kwa njia ya mahojiano, na vielelezo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji imebaini mambo yafuatayo ambayo yanapaswa kuchukuliwa hatua za haraka:

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini