Friday, February 3, 2017

BENK YA KCB WAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE MKOANI MOROGORO

Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, (aliyekaa katikati) na afisa biashara wa benki ya KCB tawi la morogoro, Lela Kisinda (aliyekaa kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Morogoro.

Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Benki ya KCB mkoani Morogoro.


Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hyo jijini Morogoro 
Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Allen Mhidze akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.

Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Grace Makoye akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.

Baada ya Rais Magufuli Kumsaidia Mjane Jana,leo yametokea haya Jijini Dar es salaam

Wanawake mbalimbali ambao ni wajane nchini Tanzania waliojitokeza Mbele ya wanahabari katika Ofisi za Cama cha wajane nchini tanzania TAWIA kumshukuru Rais Wa Tanzania Baada ya kuonyesha kuanza kuwasaidia Wajane nchini Baada ya Jana kumsaidia Mjane aliyemuomba msaada katika siku ya haki duniani
 Na Exaud Mtei Dar es salaam

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli jana kuagiza kusikilizwa na kusaidiwa kwa mwanamke mjane ambaye alileta malalamiko yake ya kudhulumiwa mali za Mumewe jana katika maadhimisho ya siku ya Haki Duniani,Hatimaye chama cha wanawake wajane nchini Tanzania TAWIA wameibuka na kutoa ya moyoni kuhusu swala hilo huku pia wakipongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Mh Rais.

Akizungumza na wanahabari Mapema leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Chama hicho Rose Sarwatt amesema kuwa chama hicho kimefarijika sana na hatua za Rais kuanza kuwajali wajane wa nchi hii jambo ambalo walilipigia kelele kwa muda Mrefu katika serikali zilizopita ambapo kwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha njia na matumaini mapya kwa wajane.
Aidha pamoja na Pongezi hizo Mkurugenzi huyo ametuma ombi maalum kwa Rais ambapo amesema kuwa kushughulika na Tatizo la mtu mmoja ni sahihi lakini Mh Rais akumbuke kuwa mjane huyo ni mmoja kati ya wajane Zaidi ya laki saba nchi nzima kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya mwaka 2012 hivyo kumtaka Rais kuanza kuwasikiliza wajane wote nchini ili kupunguza adha kubwa wanayoipata pindi tu ambapo wanaondokewa na wanaume zao ambapo hukumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzulumiwa mali zao.


Mkurugenzi wa Chama hicho Rose Sarwatt akizngumza na wanahabari mapema leo
Aidha wanawake hao wameiomba serikali kuanzisha mahakama ya familia itakayosimamia kesi zote za masuala ya familia ikiwemo kesi za mirathi jambo ambali wamesema kuwa litaondoa msongamano wa kesi za wajane zilizojaa katika mahakama mbalimbali nchini Tanzania ambazo pia zimedumu kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzi.

Hata hivyo wajane hao wameomba kufanyiwa kwa marekebisho sheria ya mirathi ya mwaka 1963 ambapo amesema kuwa kama ilivyo kwa sheria nyingine nchini zinazofanyiwa marekebisho kwa dharura na nyingine kutungwa kwa Dharura Kutokana na uhitaji uliopo basi wameomba Mh Rais ifanyike hivyo kwenye sheria hiyo ili kuwapatia haki wajane waliowengi ambao wanakosa haki zao nchini.

Jana katika siku ya maadhimisho ya Haki nchini Tanzania Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Mjane Kutokea tanga alijitokeza mbele ya Rais Magufuli na kufikisha kilio chake cha kudhulumiwa haki zake kutokana na kufariki kwa mume wake ambapo baada ya maelezo hayo Mh Rais aliagiza swala hilo kushughulikiwa mara moja na mwanamke huyo kupewa haki yake kisheria

Thursday, February 2, 2017

Mzee wa Miaka 75 aanza darasa la kwanza,Mbowe atikisa Bunge,Makonda ajitoa muhanga Vita dawa za kulevya,Rais Magufuli aacha Vumbi siku ya sheria,Simba watamba kurejea Kileleni,Magazeti ya leo Ijumaa Feb 3,2017 yapo hapa

HAWA NDIO WASANII WALIOTAJWA NA MH MAKONDA KUWA WANATUMIA MADAWA YA KULEVYA,WANAITWA POLISI KESHO

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametajwa kuwa ni kati ya wasanii ambao wanatumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kesho kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda katika kituo cha polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amewataja wasanii wengine akiwepo TID, Chid Benz, pamoja na Recho na kusema anahitaji kesho wafike makao makuu ya kituo cha polisi.
"Naomba tukutane kesho pale polisi Central akiwepo TID, akiwemo Wema Sepetu, wakiwepo wakina Junior Sniper, wakina Ditto, Titoo, kuna Ally Denya, kuna wakina Chacha, kuna kina Mecky wengine hawa wakina Petit Man tayari nishawatia mikononi mwa sheria, kuna watu kama kina Recho, Chid Benz wote hawa nawahitaji ni vijana wenzangu nafikiri tutaelewana vizuri" alisema Paul Makonda

KUSAFIRI KUSIKUNYIME FURSA YA KUFANYA MAZOEZI


Na Jumia Travel Tanzania


Je, unapenda mazoezi? Umeshawahi kujikuta ukiwa njia panda ukijiuliza aidha usafiri au la, kwa kuhofia kutopata fursa ya kufanya mazoezi? Basi ondoa shaka kwani Jumia Travel inakujulisha kuwa hoteli zifuatazo zina sehemu na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanyia mazoezi.    

MECHI ZA WIKIENDI HII LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo Februari 2, mwaka huu ambako Mwadui itaialika Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga.


Mchezo huo pekee Na. 201 utaanza saa 10,00 jioni na Ijumaa Januari 3, Young Africans ya Dar es Salaam, itaikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Jumamosi Februari 4, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili.

YOUNG AFRICANS YAAGIZWA KUMLIPA KOCHA BRANDTS



Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), limeitaka Klabu ya Young Africans ya Dar es Salaam kulipa mara moja deni la aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernst Wilhelmus Johannes Brandts - Raia wa Uholanzi waliyevunja naye mkataba miaka miwili iliyopita.

Klabu ya Young Africans imetakiwa kulipa dola 11,000 za Marekani kama ambavyo iliamriwa Juni 30, 2015 na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ya FIFA.

WANA USALAMA WA CUF YA PROFESA LIPUMBA WATOA ONYO KALI KWA WANAOTAKA KUKIHUJUMU CHAMA HICHO

 Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu madai ya hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama hicho. Kushoto ni Ofisa  Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Ofisa  Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe, akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Naibu Kamanda wa Blue Gurd, Wilaya ya Kinondoni,  Mohamed Kiotola, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Zainabu Mdolwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina na Mkurugenzi wa Blue Gurd wa Wilaya ya Temeke, Saidi Mtumbwe.
Wafuasi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.

TECNO MOBILE YASHINDA KAMPENI BORA



Kampuni  inayoongoza kwa mauzo ya simu nchini Tanzania, TECNO MOBILE imefanikiwa  kushinda tuzo za  Tanzania leadership Awards  zilizofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam. 

Katika mchakato wa tuzo hizo zilizoandaliwa na Purple  cow media Tecno   iliingia katika tatu bora ikiwa inashindana na kampuni mbili kubwa nchini Tanzania, kampuni ya mawasiliano ya simu TIGO na kampuni ya vinywaji  TBL , zote zikiwa katika  kitengo cha kampeni bora MITANDAO YA Kijamii ya  mwaka katika mitandao ya kijamii.
Tecno waliingia katika kinyang’anyiro kupitia kampeni yao ya simu  maarufu ya TECNO  CAMON  C9, katika kampeni iliyoshika hisia za  watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana na kuwapa nafasi watumiaji  wa simu kupiga picha kutokana na  maelekezo yaliyokua yanatolewa na account za mitandao ya kijamii  za kampuni,  washiriki washindi walipewa  zawadi  za aina mbalimbali   zikiwemo simu za TECNO CAMON C9.


 Tecno imekua kampuni ya kwanza ya simu kushinda katika kategori hiyo ya kampeni bora ya mwaka ya  mitandao ya kijamii kutokana na uwezo wake mkubwa uliojidhihirisha kwa kuwapa nafasi kubwa watumiaji wa mitandao na wateja wake kufikisha matzo yao na kusaidiwa lakini pia wateja kuongea na watu mbalimballi maarufu kama Salma Jabir, Hamisa Mobeto pamoja na Idriss Sultani huku zawadi kemkem zikitolewa kwenda kwa watumiaji wa mitandao waliofwata TECNO mobile katika mitandao.

Jamii ya Kitanzania itaendelea  kufaidika na mitandao ya kijamii kupitia kampuni kubwa ya  Tecno Mobile wakifanya matukio mbalimbali ikiwemo kampeni mpya  iliyopata umaarufu ya KAMA MBELE washindi wakipata nafasi ya kwenda kushudia mchezo wa mpira wa miguu katika jiji la Manchester wakiwa na mchekeshaji Idris Sultan, pamoja na Kampeni UPENDO inayowataka watumiaji kuweka picha au video mitandao wakisema upendo kwao ni nini na video/picha bora itampa nafasi mshiriki kuchaguliwa kwenda kusheherekea siku ya wapendao katika hotel kubwa Nchini.

Wednesday, February 1, 2017

Bombardier Yazua Balaa jana,Kubeti na Mitandao chanzo cha matokeo mabaya kidato cha nne,Simba waenda songea Kibabe,Soma magezeti yote ya leo Feb,2,2017 hapa

FAIDA ZA KUWAHI KAZINI MAPEMA


Na Jumia Travel Tanzania

Kuamka asubuhi ni mtihani mgumu ambao umewashinda watu wengi, si wafanyakazi, wanafunzi, wafanyabiashara au watu wa kawaida. Watu wengi hulazimika kuamka asubuhi kwa sababu inawalazimu kufanya hivyo vinginevyo wasingefanya hivyo.

Wataalamu mbalimbali wa afya, watu mashuhuri na waliofanikiwa katika shughuli zao, wametoa ushuhuda kuwa ukitaka kufanikiwa ni lazima ujijengee mazoea ya kuamka asubuhi na mapema. Jumia Travel inapenda kukushirikisha faida zifuatazo za kuwahi mapema kuelekea kwenye shughuli zako.

TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO

Mratibu wa Mafunzo ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni Dk.Lukwinyo na Dk.Mbaruku Mlinga.


 Madaktari mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.
Madaktari wa Tiba ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud, Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.

Diwani wa Kata ya Ndugumbi Mh Thadei Massawe akabidhi Vyeti kwa Madereva Pikipiki (Bodaboda ) waliokuwa katika mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo

Diwani wa kata ya Ndugumbi Mh Thadei Massawe(Katikati) Pamoja na Afisa Kata wa ndugumbi wakimkabisho mmoja kati ya madereva 27 wa pikipiki Maarufu kama Boda Boda cheti maalum cha kuashiria kumaliza mafunzo ya siku kumi yaliyokuwa yanatolewa na serikali kupitia Kata hiyo,Mafunzo yakiyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo madereva hao juu ya kazi yao na kuwakinga na ajali za barabari pamoja na Athari nyingine nyingi za kazi hiyo.

Picha ya Pili na ya tatu zikimuonyesha Mwenyekiti wa Madereva wa Madereva wa Pikipiki Mkoa wa Dar es salaam Bwana Michael Massawe ambaye katika shughuli Hiyo alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda.

Ambapo akizungumza kwa Niaba yake amesema kuwa Mkoa wa Dar es salaam umejipanga kuhakikisha kuwa unawapa uwezo mkubwa madereva wa pikipiki ili waweze kufanya kazi zao kwa ustadi zaidi na kuepuka ajali na majanga ambayo yanaweza kuzuilika kwa urahisi,Amesema kuwa mafunzo kama hayo ambayo yamehitimishwa leo Katika kata ya Ndugumbi ni Mpango wa Serikali kupitia Trafic kikosi cha usalama Barabarani kuhakikisha kuwa madereva wanapatiwa elimu na kuwa na leseni zinazowafanya kuendesha Vyombo Hivyo bila madhara yoyote

Diwani wa kata ya Ndugumbi Mh Thadei Massawe akizungumza na madereva hao 27 waliohitimu mafunzo hayo ambapo amewata kuhakikisha kuwa wanazingatia kile ambacho wamejifunza kwa siku hizo kumi huku akisisitiza kuwa endapo watafwata waliyofundishwa ana uhakika kuwa kutakuwa na kupungua kwa Ajali za bodaboda na matatizo ya ujambazi wa piki piki katika kata yake
Baadhi ya Madereva waliohitimu mafunzo hayo leo Jijini Dar es salaam katika kata ya Ndgumbi