Saturday, March 11, 2017

SERIKALI IZUIE UINGIZWAJI WA NYANYA NA PILIPILI KUTOKA NJE ILI KULINDA VIWANDA VYA NDANI

 SERIKALI imetakiwa kuzuia uingizaji wa bidhaa za Nyanya za kutengeneza pamoja na Pilipili za kutengeneza ili kuweza kuviokoa viwanda vya ndani ambazo zinatengeneza bidhaa hizo.

Pia,Serikali imeombwa kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya masoko pamoja na miundombinu ambayo itasaidia viwanda hivyo kuinuka na kuweza kuzalisha bidhaa nyingi.

Ombi hili kwa serikali limetolewa leo Jijini Dar es Salaam,na Dominicus Ulikaye ambaye ni Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya kiwanda Darsh  ambao ni wazalishaji wa bidhaa za RedGold wakati wa mkutano wa waadau wa Kilimo.

Amesema ili serikali ya viwanda iweze kufanikiwa hakuna budi serikali kuangalia na ikiwezekana kuzuia uingizaji wa bidhaa kutoka nje ili kuweza kuinua bidhaa za ndani.


“Yaani sisi tunazilisha (Tomatos na Chill sause) kwa wingi ila tukakosa masoko ya uhakika kutokana na kupata ushindani kutokana na bidhaa kama hizi ambazo zinatoka nje.ambazo zinapelekea bidhaa zetu kushindwa kutanuka”amesema Ulikaye.

Ulikaye amesema sasa ni wakati wa serikali kutilia mkazo bidhaa hizo kutoka nje kwa kuweza kuziachia bidhaa za ndani kuweza kuuzika vizuri na kusaidia viwanda hivyo ambavyo amedai zimetoa ajira nyingi kwa watanzania.

‘Kiwanda hiki leo kimetoa ajira zaidi ya elfu sitini za wakulima wa nyanya ambao tumekuwa tukizinunua nyanya hizo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu,kwahiyo kwa serikali ikishindwa kuzuia uingizaji wa bidhaa basi watanzania hawa ambao ni wakulima watakosa masoko yetu”ameelekeza Ulikaye.

WANAWAKE WANACHAMA WA CHA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAWI LA MIEMBENI MANZESE WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUFANYA USAFI.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese,Fatuma Mohamed (kulia) akishirikiana na wanachama wa chama hicho kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mtaa wao kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam.
 Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)Tawi la Miembeni lililopo Kata ya Manzese wakishirikiana na wafanyakazi wa hospitali ya Mtakatifu Monica kuweka taka kwenye sehemu ya kuwekea uchafu kama ishara ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam. 

Friday, March 10, 2017

WATAMBUE WANAWAKE 10 MASHUHURI NCHINI TANZANIA

Na Jumia Travel Tanzania

Kila ifikapo Machi 8 dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambapo nchi na taasisi mbalimbali huwa na shughuli kadha wa kadha katika kusherehekea siku hii. Kwa kawaida shirika la Umoja wa Kimataifa Duniani, UN, huwa na kauli mbiu kwa kila mwaka katika kuadhimisha siku hii, kwa mfano mwaka huu inasema, “Wanawake Katika Ulimwengu wa Mabadiliko ya Kazi: Kufikia usawa wa 50 - 50 ifikapo 2030.”   

Tofauti na awali, sasa hivi wanawake wamekuwa na muamko mkubwa katika kuisherehekea siku hii kwani wanaitumia vilivyo kupaza sauti zao juu ya masuala yanayowahusu. Hivyo basi, Jumia Travel inakuletea majina ya wanawake hawa 10 wa kitanzania waliojipatia umaarufu mkubwa kupitia shughuli tofauti za kijamii wanazozifanya. 

Mama Samia Suluhu

Unapozungumzia miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kupata nyadhifa za juu kabisa za uongozi nchini Tanzania basi huwezi kuacha kumtaja Mama Samia Suluhu Hassan. Huyu ni Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke kuwahi kutokea nchini ambapo aliupata wadhifa huo kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 uliomuweka Rais John Pombe Magufuli madarakani. Tanzania kama nchi zingine za kiafrika kwa kiasi fulani imekuwa na kasumba ya kutomwamini mwanamke katika kushika nyadhifa za juu za kiuongozi. Lakini kuchaguliwa kwa Mh. Samia Suluhu kumedhihirisha kuwa hakuna lisiloshindikana endapo wanawake wakiwezeshwa, kuaminiwa na kupewa fursa.

Maria Sarungi Tsehai

Miongoni mwa wanawake wanaofanya shughuli nyingi katika harakati za kuiona jamii ya watanzania ikisonga mbele ni Maria Sarungi Tsehai. Kumchambua Maria kwa kila shughuli anayoifanya ni vigumu kwani itachukua muda mrefu ingawa kitaaluma yeye ni mtaalamu wa masuala ya mawasiliano. Kati ya shughuli kadha wa kadha anazozifanya, jina la Maria Sarungi Tsehai lilikuja kujulikana na watanzania wengi baada ya kuteuliwa kuwakilisha kwenye Bunge la kujadili mchakato wa katiba mpya na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2014. Maria alichaguliwa kufuatia hamasa yake ya kuibua mijadala ya kimaendeleo nchini Tanzania kupitia mitandao ya kijamii kama vile ‘Facebook na Twitter’ kupitia #ChangeTanzania, na kufanikiwa kuungwa mkono na wafuasi zaidi ya 50,000. 

Dr. Helen Kijo Bisimba

Kwa muda mrefu Dr. Bisimba yupo kwenye tasnia ya sheria ambapo amekuwa kipaumbele katika kutetea maslahi na kutoa msaada kwa watanzania wanyonge wanaonewa na kunyimwa haki zao katika masuala mbalimbali. Ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) nafasi ambayo yupo kwa zaidi ya miongo miwili. Mama huyu msomi aliyebobea katika masuala ya sheria amekuwa na mchango mkubwa juu ya harakati za kutetea haki na usawa katika nyanja mbalimbali. Kupitia shughuli za kituo hicho, Dr. Helen Bisimba amekuwa ni alama na nguzo muhimu ya mapambano dhidi ya unyonge na ukandamizwaji wa haki dhidi ya wananchi wa kipato cha chini.    

Faraja Nyalandu

Watanzania wengi walilifahamu jina la Faraja Nyalandu baada ya kuwa mshindi wa kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka 2004. Lakini kipindi hicho alikuwa akijulikana kama Faraja Kota kabla ya kuolewa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini kwa sasa, Mh. Lazaro Nyalandu. Faraja ni mwanamke mjasiriamali katika masuala ya kijamii ambaye amejikita zaidi katika shughuli za kielimu ili kuwajengea uwezo watoto na vijana kuipata huduma hiyo. Kupitia dhamira hiyo ameweza kuzindua programu mbili za kuwawezesha wanafunzi kupata masomo kwa njia ya maswali na majibu pamoja na maelezo ya kutosha. Huduma hizi mbili ambazo ni ‘Makini SMS na Shule Direct,’ huwawezesha wanafunzi na walimu kuweza kusoma na kufundisha kupitia njia za simu na mtandao na hivyo kuepuka changamoto kama vile za uhaba wa walimu, vitabu na muda wa kujisomea.

Jokate Mwegelo

Jokate Mwegelo si jina geni miongoni mwa watanzania wengi na hii ilitokana na ushiriki wake katika mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2006 na kuibuka nafasi ya pili. Mbali na shughuli za urembo pia anajihusisha na muziki, ujasiriamali, uanamitindo na mavazi, uigizaji wa filamu, utangazaji wa luninga, ushereheshaji, na shughuli za kielimu. Jina lake ni kubwa na hamasa kwa mabinti wanaokua kutokana na mafanikio aliyonayo. Mpaka hivi sasa amefanikiwa kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya masuala ya urembo na mavazi inayojulikana kama ‘Kidoti.’ Mbali na hapo anaendesha shughuli za kusaidia jamii yake kwenye nyanja ya elimu kupitia kampeni inayokwenda kwa jina la ‘Be Kidotified.’ Mpaka sasa amekwishajenga viwanja vya netiboli na kikapu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani.  


Doris Mollel

Jina la Dorris Mollel limeanza kusikika na kujulikana baada ya kushinda taji la mashindano ya Miss Singida mnamo mwaka 2014. Baada ya hapo alianzisha harakati za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au miezi 9 yaani njiti ambapo alianzisha taasisi yake aliyoipa jina la Doris Mollel Foundation mwezi Februari mwaka 2015. Lengo kuu la kuanzisha taasisi hiyo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa njiti. Pia ameazimia kuielemisha jamii kwani tafiti zinaonyesha kwamba idadi ya watoto hao ni ndogo kutokana na wazazi wengi kutokuwa na tamaduni ya kwenda kujifungulia hospitali. 

Mercy Kitomari 

Huyu ni Afisa Mtendaji Mkuu na Muasisi wa kampuni inayojihusisha na utengenezaji wa ‘Ice Cream’ inayokwenda kwa jina la Nelwa’s Gelato. Mercy alishawishika kwa kiasi kikubwa kuanzisha biashara hii baada ya kuwa masomoni London nchini Uingereza ambapo alikuwa akivutiwa na vibanda vinavyouza ‘ice cream.’ Alikuwa anajiuliza endapo kama akirudi nchini atafanya kitu kama hiko kwani havikuwepo. Ametimiza ndoto hiyo na kwenda mbele zaidi kwa kuwawezesha watanzania wengine na kuwapataia mafunzo ya namna ya kuendesha biashara hiyo. Katika biashara hiyo Mercy hutumia viungo vya hapa nyumbani kutengenezea ‘ice cream’ zake kama vile matunda na karanga, hivyo kutoa ajira pia kwa wakulima. 

Joyce Kiria

Ongezeko la vituo vya luninga nchini Tanzania limekuja na fursa ya kuibuka kwa wazalishaji wa vipindi lukuki vinavyohusu masuala tofauti ya kijamii. Joyce Kiria ni miongoni mwa watangazaji wachache wanaovuma kwa kuwa na kipindi cha luninga kinachoivutia hadhira kubwa nchini. Kipindi chake cha ‘Wanawake Live’ kinachorushwa kwenye kituo cha luninga cha East African Television (EATV) kimejipatia umaarufu mkubwa hususani kwa kujikita zaidi katika kujadili na kuibua masuala mbalimbali yanayowakabili wanawake na kuwasaidia. Kipindi chake kimekuwa ni chanzo kizuri na msaada mkubwa kwa wanawake wanaokumbwa na changamoto mbalimbali na hatimaye kupatiwa msaada na serikali, taasisi au viongozi kuchukua hatua.

Wakonta Kapunda

Inawezekana kuwa habari ya huyu binti ndiyo iliyowagusa watanzania wengi zaidi nchini Tanzania kwa mwaka 2016. Maisha ya Wakonta Kapunda yalibadilika baada ya kupata ya kugongwa na gari na mwanafunzi mwenzao siku ya mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Korogwe, Tanga mwaka 2012. Ajali hiyo ilipelekea kupooza mwili mzima na kumlazimu kufanya shughuli zake kwa kutumia kichwa tu. 

Kilichowagusa wengi ni ari ya kutokata tamaa kwake ambapo aliweza kushiriki shindano la kuandika mswada wa filamu (script) lililodhaminiwa na kampuni ya Filamu ya Maisha ya nchini Uganda. Kwa kutumia ulimi wake aliweza kuandika na kufanikiwa kuchaguliwa kuingia hatua ya kwanza. Alijitokeza hadharani kuomba msaada baada ya kutakiwa kwenda visiwani Zanzibar kushiriki mafunzo ya siku 10 ambayo yalikuwa yanagharimu takribani kiasi cha shilingi milioni 4 za kitanzania. Wakonta alikuwa anaishi na familia yake mkoaniRukwa na haikuwa na uwezo wa kumsafirisha mpaka Zanzibar kwenda kujumuika na wenzake. Kupitia ushujaa wake, kutoka tamaa na kuamini kwamba ulemavu sio mwisho wa maisha, habari za Wakonta ziliwagusa watanzania na taasisi nyingi ambapo kampeni mbalimbali zilianzishwa kumsaidia kutimiza azma yake.   

Thursday, March 9, 2017

TAMKO KWA UMMA JUU YA SIKU YA AFRIKA YA MFUMO WA NCHI KUTATHMINIWA NA NCHI NYINGINE (APRM)


MKUU WA WILAYA YA KISARAWE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOA WA PWANI


 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda (katikati), akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Shule ya Msingi Chanzige wilayani  Kisarawe jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile, akipima shinikizo la damu katika maadhimisho hayo.
 Diwani wa Kata ya Kisarawe, Abel Mudo akipima afya.

 Ofisa Mikopo wa Benki ya Equity, Nelifyage Mbwilo (kulia), akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness Seneda (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali katika maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Germana Mnga'alo na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Kisarawe, Khamis Dikupatile.

EfG YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na shirika hilo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Mjumbe wa Bodi ya EfG, akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris akitoa hutuba 
yake kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Chang'ombe, Mkaguzi wa Polisi, Meshack Mpwage, akihutubia kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa muda wa wanawake wajasiriamali masokoni, Betty Mtewele na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi kikitoa burudani.
 Waananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea. wanawake wakiwa na mabango yenye maneno ya nafaa kuwa kiongozi.
 Meza kuu.
 Wafanyabiashara katika soko la Temeke Sterio wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Burudani za sarakasi zikiendelea.

 Nifuraha tupu katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele 'kweli ni wanawake na maendeleo'
 Vipeperushi juu.


Wasaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim jijini Dar es Salaam, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Wednesday, March 8, 2017

Skuli ya Kijini na Mbuyu Tendee Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,Wafaidika na Mradi wa Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Cha PennyRoyal kwa Kutoa Elimu ya Afya na Mazingira

Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA anayetowa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.
Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitowa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli hya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe  Pennyroyal.  

TIZAMA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE KUTOKA LHRC HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu Mama Hellen Kijo Bisimba akizungumza na wanawake mbalimbali waliokuwa wanashiriki katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Jana ambapo Kituo hicho kilifanya maadhimisho hayo Jijini Dar es salaam na kuwakutanisha wanawake mbalimbali na mashirika Tofauti kuhakikisha kuwa wanajadili kwa Pamoja changamoto zinazowakabili na jinsi gani wanaweza Kuzitatua.


Mwenyekiti wa chama cha ACT WAZALENDO Mama Anna Mgwira akisikiliza kwa makini Hotuba mbalimbali katika maadhimisho hayo ambayo na yeye alishiriki kama mmoja kati ya wanawake waliodhubutu na kuweza kugombea nafasi kubwa ya Urais nchini akiwa ni mwanamke pekee kufanya hivyo katika uchaguzi Uliopita

Naemy Silayo akitoa Tamko la wanawake katika Shughuli hiyo.


Rebecca Jummy moja kati ya wanadada mashughuri wa sheria nchini ambaye amejizolea Umaarifu mkubwa katika kesi aliyoifungua dhidi ya sheria ya ndoa nchini akitoa mada katika Mkutano huo

Rais wa Vikoba,Devotha Likokola ambaye alikuwa Mgeni Rasmi ambapo amesema kuwa Wanawake wanatakiwa kuzitumia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali zitakazowasaidia kuondokana na utegemezi ili kuifikia Tanzania ya Viwanda

Tuesday, March 7, 2017

MAADHIMISHO YA GIRL GUIDES TEMEKE YA KUMUENZI MWASISI WA TGGA DUNIANI

 Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania (TGGA) ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho Duniami, Roden Barden Powell yaliyofanyika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TGGA Tanzania, Profesa Martha Qorro na Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi . 

Mashirika ya TGNP Mtandao ,Oxfam na Care International yaungana katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani

Mkurungezi wa TGNP  Lilian Liundi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza uzinduzi wa kauli mbiu ya ya mwaka huu "Kuwa Jasiri, PingaUkatili Dhidi ya Wanawake” Katika kuadhamisha siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi ambapo  maadhimisho hayo yatafanyika kimkoa  katika viwanja vya MwembeYanga Temeke Jijini Dar es salaam, Pembeni yake kushoto ni Mkuu wa kitengo cha ushawishi Oxfam Eluka Kibona ,na kulia ni  Mkurungezi wa  wanawake wa Basketball Dar es salaam Bainasi Wamunza na mwishoni ni Makamu mwenyekiti wa Chaneta Bi Zainab Mbiro 


Mkuu wa kitengo cha ushawishi Oxfam  Eluka Kibona akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati wa kutangaza uzinduzi wa kauli mbiu ya ya mwaka huu "Kuwa Jasiri, PingaUkatili Dhidi ya Wanawake” Katika kuadhamisha siku ya wanawake duniani tarehe 8 Machi ambapo  maadhimisho hayo yatafanyika kimkoa  katika viwanja vya MwembeYanga Temeke Jijini Dar es salaam,Kulia kwake ni Mkurungezi wa TGNP  Lilian Liundi.

Tigo yashirikiana na Milvik kutoa huduma za bima ya afya wanazomudu wateja


Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin(kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi kwa kutumia Tigopesa ijulikanayo kama Bima Mkononi, Pembeni yake ni Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.

Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara , akitoa ushuhuda

Mteja aliyenufaika na huduma ya Bima Mkononi kwa kutumia Tigo pesa , Hawa Ramadhani mkazi wa Kibaha Maili Moja akiongea na waandishi wa jijini Dar Es Salaam leo, kwenye uzinduzi wa huduma iliyoboreshwa ya bima kwa simu za mkononi. Wengine kutoka kushoto Meneja mkazi wa Milvik Tanzania, Tom Chaplin, Mteja aliyenufaika Melikizedeki Nyalufujo mkazi wa kimara na Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa Simu wa Tigo, Ruan Swanepoel.