Wednesday, March 15, 2017

NAIBU WAZIRI JAFFO AKAGUA MAANDALIZI YA UJENZI WA DARAJA LA KIJICHI-TOANGOMA TEMEKE

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo (katikati) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Issa Mangungu alipokwenda kukagua ujenzi wa daraja linalounganisha Kata za Toangoma na Kijichi, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Toangoma, Mohamed Mketo. (PICHA NA DALILA SHARIF)

HII NI NYIMBO KALI MPYA KUTOKA KWA BIG WHIPY,FURAHIA MCHANA WAKO

Kampuni ya Quality Group LTD yaelezea mipango mipya ya miradi yake nchini



Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Quality Group Limited, Bwana. Nicholas Ralph leo Machi 15.2017, amekutana na vyombo  vya habari na kuelezea mipango mbalimbali ya kampuni hiyo ikiwemo miradi yake inayoendeshwa karibu nchi nzima Tanzania Bara na Visiwani.

Akizungumza na vyombo mbalimbali  katika tukio lililofanyika majira ya Alasiri ya leo Machi 15, Mkurugenzi huyo ameweza kuweka bayana miradi yao hiyo pamoja na muelekeo wa kampuni katika kufikia malengo yake  huku akibainisha kuwa, wataendelea kufanya kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kuwafikia wananchi kama sera ya makampuni hayo na ile ya Taifa huku wakiungana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli  ya kupiga vita rushwa na kuifanya Tanzania ya Viwanda.

Akielezea muelekeo wa kampuni hiyo amebainisha kuwa watanzania wanaimani nao hivyo wataendelea kujikita zaidi kwenye miradi na kuwafikia watanzania sehemu mbalimbali kama dira yao ya kuiletea Tanzania maendeleo yaani 2016/2021 na ile ya mpaka 2025 
“Quality Group imeweza na inaendelea kushirikiana na makampuni yenye majina makubwa Duniani kwa kufanya nao kazi pamoja na uwakala kwa hapa Tanzania ikiwemo kampuni za GM, Hoda,Isuzu, Bridgestone pamoja na  Chevrolet  huku yakizalisha faida maradufu hii ni pamoja na kutoa ajira kwa watanzania” amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha, akitaja baadhi ya miradi ambayo inasimamiwa na kampuni hiyo hapa nchini ni pamoja na mradi wa shamba la mpunga lililopo Mkoani Morogoro ambalo litakuwa likipanda mazao hayo sambamba na kununua kwa wakulima wadogowadogo ili kupata mchele.
Quality Group pia inasimamia miradi Visiwani Zanzibar ikiwemo ule wa Stone Town Village huku pia mirad mingine ni ule wa  Matrekta ambao ni wa Sonalika.
Kampuni hiyo kwa hapa nchini ni ya miaka mingi zaidi ya miaka 30 huku ikiwa imeweza kuajili wafanyakazi zaidi ya 667,300 huku ikitengeneza zaidi ya  faida  Bilioni 348.6 huku wa miongoni mwa makampuni bora na yenye majina makubwa kwa kujijengea heshima ndani na nje ya nchi.

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA KUFANYIKA KESHO, SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA WAFIWA

 Marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
 Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sofia Simba akimpa pole mjane wa marehemu, Janeth Kahama.


Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina Lowassa (wa pili kulia), akiwa kwenye msiba huo.
 Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.
 Pole zikiendelea kutolewa kwa mjane wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa msibani.

Na Dotto Mwaibale

MAZISHI ya aliyekuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe Sir George Kahama yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili  wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Kesho mwili wa marehemu  utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia  saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Ibada ya mazishi  itafanyika  katika  makaburi  ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu  9.30 alasiri.

Tuesday, March 14, 2017

WAZIRI NAPE ATISHIA KUWATUMBUA MAAFISA HABARI WASIO WAJIBIKA IPASAVYO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amemtaka Mkurugenzi wa Habari maelezo kufuatilia utendaji kazi wa maafisa habari na mawasilano wote ili kuona utendaji kazi wao kama unaleta maendeleo kwa jamii.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na maafisa habari na mawasiliano wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo Mkoani Dodoma.

Amesema kuwa wao ndiyo chanzo cha kuwafanya viongozi wao kukimbia vyombo vya habari kutokana na maafisa hao kushindwa kuwaandaa vyema badala ya kutoa habari zinazotakiwa kwa jamii.

MVUA DAR YAUA MTOTO AKIJARIBU KUVUKA MTO MSIMBAZI


Na Regina Mkonde
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jumanne ya Machi 13, 2017 katika eneo la Mongo la Ndege, limeokota mwili wa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Imelda Ngonyani (13) aliyekufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Msimbazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 14, 2017, Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema marehemu huyo kabla ya kufa maji alikuwa pamoja na wenzake watano walionusurika kifo wakielekea shule ya Msingi ya Mongo la Ndege.

TAARIFA ZA JK KUZINDUA TAASISI YAKE,ZILIMFIKIA ZITTO KABWE,HAYA NDIYO MANENO YAKE

Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete leo amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu
Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia akaunti yake ya Facebook:
“Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri

Monday, March 13, 2017

HABARI ZOTE MPYA KUTOKA TFF ZIPO HAPA LEO

MALINZI AMLILIA SIR GEORGE KAHAMA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu Sir George Kahama aliyefariki dunia Jumapili akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Rais Malinzi amesema taifa limepoteza mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa katika kupigania maendeleo ya mpira wa miguu baada ya kupigania Uhuru ambao Watanzania leo wanajivunia amani.

Pamoja na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, Rais Malinzi Dkt Magufuli amewapa pole wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi, akisema ni kielelezo cha kiongozi aliyetukuka.

COCA - COLA YAKAMILISHA SHANGWE JIJINI MBEYA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia), akigongesha soda ya Coca-Cola na viongozi wengine wa kampuni hiyo kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho mkoani Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni David Karamagi - Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi – Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Mbeya. Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo - MMG-MBEYA.

Mgodi wa GGM na Wanawake wa Geita

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyankumbu wakijisomea library. Shule hii ya wasichana ni ya mfumo wa sayansi na inawanafunzi zaidi ya 900, imesheheni vifaa vya maabara, nyumba za kisasa 36 kwa ajili ya waalimu, madarasa 21 na viwanja mbalimbali vya michezo. Pamoja na miradi mingine ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, GGM imewekeza shilingi Bilioni 10 katika ujenzi wa shule hii kubwa na ya kisasa. 
Wanawake wakiwa wanashona na kutaririzi katika mradi chini ya mradi mkubwa uitwao Geita Economic Development Project (GEDP) mradi huu umelenga kuwawezesha wanawake na jamii ya Geita katika kujiinua kiuchumi na unahusisha miradi ya kilimo cha mpunga na alizeti, Kushona na kutarizi, ufyatuaji matofali, Welding na ushonaji na kutengeneza viatu .

Sunday, March 12, 2017

Video: ASKOFU GWAJIMA AMSHAMBULIA TENA MAKONDA...ATAJA SABABU ZA KUKIMBILIA AFRIKA KUSINI

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametaja makosa ya kisheria yaliyomfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda kukimbilia Afrika Kusini.

Akizungumza leo kanisani kwake, Ubungo, jijini Dar es salaam, Gwajima alidai kosa la kwanza la Makonda ni kughushi cheti ambacho kinaonyesha yeye ni Paul Makonda wakati akifahamu kuwa yeye ni Daudi Bashite.

“Kosa hilo kwa mujibu wa Gwajima ni kifungo cha miaka saba.Kosa jingine ni kula kiapo cha ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa akisema yeye ni Makonda wakati akijua yeye ni Bashite,” alisema

Gwajima alisema kosa la hilo la kula kiapo na cheti feki ni kifungo cha miaka mitatu.

Kosa jingine alisema ni kupokea mshahara na posho kwa jina la Makonda wakati akifahamu si yeye na kuongeza kuwa kosa hilo likithibitika atatakiwa kurudisha mishahara na posho zote alizochukua.

==>Tazama Video ya Mahubiri yake hapo chini




LOWASA AANDIKA WARAKA MZITO JUU YA WALIOTIMULIWA CCM,USOME HAPA


lowassaNafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.

Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa kutoka CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwa tajwa huko katika vikao vyao.
Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala Bora nchini.
Hawa walikuwa mashujaa wa kutetea haki,demokrasia na taratibu na kupinga dhulma ndani ya chama chao na nchini.Kwa kusimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.
Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa. Nawakaribisha Chadema na UKAWA kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa kisiasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.
Waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta Demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu,safari hii inahitaji umoja na mshikamano ili kufikia malengo.
Huko wanajinasibu kuwa CCM ikiyumba, nchi itayumba lakini mimi nasema kinachotokea ni kwamba, kwa jinsi CCM inavyoyumba, ndivyo wananchi wanazidi kukomaa kisiasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.
Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala. Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora.
Edward Lowassa
Mjumbe kamati Kuu Chadema

Saturday, March 11, 2017

News Alert !! BASI LA ALLY'S STAR LAGONGANA NA LORI LA AZAM MISUNGWI MWANZA

Basi la ALLY'S STAR GULF AIR lenye namba za usajiri 514 ANW likitoka Mwanza kwenda Tabora, limepata ajali asubuhi ya leo majira saa moja katika kijiji cha MWAZENZE wilayani Misungwi Mwanza mara baada ya kugongana uso kwa uso na lori la mizigo na kuacha njia.

Kwa mujibu wa maelezo ya abiria waliokuwa wamepanda kwenye basi hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva alipokuwa akijaribu kuovateki gari iliyokuwa mbele yake pasipokujua mbele yake zaidi kuna nini, ndipo basi hilo likagongana ghafla na lori la AZAM lililokuwa limebeba unga wa ngano.

Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyefariki wala kuumia zaidi ya mtu mmoja kupata mshituko wa mguu. Dereva alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo kutokea.

Mwandishi wa MASENGWA BLOG Isaac Luhende, alifika eneo la tukioametuletea picha kadhaa za tukio hilo.
Lori la mizigo lililogongana na basi hilo likiwa limeharibika baada ya ajali