Saturday, September 2, 2017

BI. HINDU KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KISUTU

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda.
Hindu alifariki dunia ghafla jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza, leo Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.

‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.
“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.

WANAFUNZI 8 WA SEKONDARI NA 7 WA SHULE ZA MSINGI WAMEBAINIKA KUWA NA MIMBA RUFIJI MKOANI PWANI

Jumla ya wanafunzi wa kike nane wa shule za sekondari na saba wa shule za msingi wilayani Rufiji mkoani Pwani ,wamebainika kuwa wana mimba ,mwaka huu .

Kutokana na taarifa hiyo ,mkuu wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo ,amewaasa wanafunzi wa kike kuacha kukimbilia mambo ya ovyo badala yake wajidhatiti katika elimu ili kupata maarifa na ufahamu .
 
Akizungumza baada ya kukamilisha ziara yake ya mwezi mmoja ,ya kutembelea shule 43 ,kuzungumza na wazazi na walezi ,alisema mimba za utotoni zinakwamisha jitihada za kumkomboa mtoto wa kike kitaaluma.
 
Njwayo alieleza ,kati ya mimba zilizobainika mwanafunzi mmoja ni wa shule ya sekondari Ngorongo ,Nambunju saba na wengine saba ni wa shule za msingi.
 
Alifafanua ,zipo hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa waliohusishwa kuwatia mimba wanafunzi hao,; ambapo watendaji wa kata wameshawashtaki kwenye vyombo vya sheria .
 
Alisema ,pia wanatengeneza mazingira mazuri kwa watoto mashuleni kwa kuwataka walimu wakae nao mara kwa mara kuwaelimisha wajiepushe na wanaume wadanganyifu .
 
Kwa mujibu wa Njwayo ,kilichomsukuma kufanya ziara hiyo ilikuwa baada ya kupata taarifa kuwa kuna wanafunzi watoro wa kudumu 190 kati ya wanafunzi 2,442 wanaotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu .
 
Aidha katika ziara hiyo amefanikiwa kuwarejesha shule wanafunzi hao 54 wa shule ya Ikwiriri ,shule ya msingi Utete tisa na shule ya msingi Mapinduzi tisa.
 
Njwayo alielezea,alichogundua ipo changamoto ya wazazi kutokuwa na ushirikiano na walimu na kutofuatilia mwenendo wa watoto wao kila siku .
 “Elimu ni muhimu ,ni nguzo na msingi wa maisha yetu ,na kwa watoto wetu ,itaweza kuwasaidia kupata ufahamu wa kujiajiri na kuwa mwanakilimo bora wa kisasa na kuwa na upeo kuliko kukosa elimu ” alisisitiza Njwayo.
 
Njwayo ,alisema kwasasa kuna watendaji wa vijiji na kata wamefukuzwa kutokana na kukatwa kwani hawakuwa na cheti cha kidato cha nne hivyo wanaajiriwa wapya kuziba mapengo .
 
“Hapo ndipo inapoonekana thamani ya elimu ,hivyo wanafunzi waache michezo na vishawishi ,;wasome kwa bidii ” alisema Njwayo.

SIKILIZA ALICHOKISEMA B DOZEN KWENYE MVUTANO WA ALLY KIBA NA DIAMOND

Host wa show ya XXL ya Clouds Fm, B Dozen amefunguka mambo machache kuhusu mvutano wa Diamond na Alikiba pamoja na team zao katika mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano na Times Fm kwenye kwenye uzinduzi wa viatu ‘SultanXforemen’ vya msanii wa filamu na mchekeshaji, Idris Sultan. B Dozen alisema ni kitu kizuri iwapo kitawaletea fedha.
“Ni game inasonga mbele, unaona kama kwenye wiki hizi mbili pamechangamka kweli, kumekuwa na team hii na team hii as long as hakuna ambacho kitatokea baada ya mabishano yanayondelea kwenye social media, radio station na Tv kwenye interview zao,” amesema.
“Ni kitu kizuri ilimradi kiwe kinawatengenezea hela isiwe ni tuwe na namba kubwa ya followers na like kwenye page zao na views kwenye YouTube bila ku-make money it won’t make sense lakini kama inatengeneza hela it very goog thing,” ameongeza.
Siku za hivi karibuni Diamond na Alikiba pamoja na mashabiki wao walikuwa na mchuano mkali katika mitandao ya kijamiii baaada ya kutoka ngoma ‘Seduce Me’ ya Alikiba na ‘Zilipendwa’ ya Diamond/WCB.

SHAKA AZUNGUMZIA MAENDELEO YA UCHAGUZI WA NDANI WA UVCCM

April Mwaka 2017 Chama Cha Mapinduzi kilianza mchakato wa Uchaguzi ndani ya Chama na Jumuiya zake. Kufuatia mabadiliko ya Kanuni ya UVCCM yaliyofanyika mwezi Machi, 2017 tulianza Uchaguzi katika ngazi za Matawi ambapo hadi leo jumla ya Matawi 23,529  sawa na Asilimia 99.4% kati ya Matawi  23,670 sawa na Asilimia 0.59% yamekamilisha uchaguzi.


Ngazi za   Kata  3,913 sawa na Asilimia 96.59% kati ya Kata 4,051 sawa na asilimia 3.4% zimekamilisha uchaguzi .Kwa upande wa majimbo ya  Zanzibar majimbo 54 sawa na Asilimia 100%, wamekamilisha uchaguzi.  

Ngazi ya Wilaya na Mkoa  mchakato wa uchujaji wa  majina kwa Vijana waliomba nafasi mbali mbali ndani ya Jumuiya yetu , umeanza na  unaendelea vizuri huku jumla ya Vijana 7,606 wamejitokeza kuchuka fomu za kugombea nafasi mbali mbali katka Jumuiya yetu, hali inayoonyesha kumekupo kwa mabadiliko  na msisimko wa kisiasa ukilinganisha na chaguzi zilizopita.

Kwa upande wa ngazi ya Taifa Vijana 350 wamejitokeza kuomba nafasi za uongozi ndani ya UVCCM kama ifuatavyo:-

(i)
Nafasi ya Mwenyekiti
113
Walioomba
(ii)
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa
24
Walioomba
(iii)
Nafasi 5 za Wajumbe wa H/Kuu
103
Walioomba
(iv)
Nafasi  5 za Wajumbe wa B/Kuu Taifa
81
Walioomba
(v)
Nafasi 1 Wawakilishi UWT
14
Walioomba
(vi)
Nafasi 1 Wawakilishi Wazazi
15
Walioomba

Maandalizi kwa ajili ya Mikutano Mikuu ya Wilaya hadi Taifa yanaendelea vyema ambapo chaguzi zote ndani ya UVCCM zinategemewa kukamilika Novemba 2017.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tunaendelea kusisitiza kuwa sifa na wasifu wa kila mgombea aliyeomba kuteuliwa kwa kadri alivyojaza kwenye fomu yake, utaandaliwa na kuandikwa vizuri katika kitabu maalum cha wagombea wote ambacho watapatiwa wajumbe wa Mkutano siku ya uchaguzi husika.
Kila mgombea atapata nafasi ya kujieleza na kutoa wasifu wake, kutaja dhamira na malengo yake mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu husika baada ya taratibu za vikao vya uteuzi kukamilika si kinyume na hivyo.

Tunaendelea kuwakumbusha kuwa ni mwiko kwa mgombea kuanza kampeni mapema  au wapambe wake kufanya ushabiki wa kisiasa kumnadi, kumpigia debe, au kujipitisha na kuelezea nafasi anayogombea. Ukiukaji huo wa Kanuni na taratibu utampotezea sifa za kuteuliwa.

Aidha tunaendelea kuwasisitiza kuwa ni marufuku na hairuhusiwi kabisa walioomba nafasi mbali mbali kuanza kufanya kampeni za kihuni , kutumia lugha chafu, siasa za maji taka kuchafuana, matusi, dharau kinyume na ubinadamu.

Kuyaacha hayo yote yafanyike bila ya kuyadhibiti, kuyaasa na kuyakemea ni mwanzo wa kukaribisha mvurugano, mgawanyiko hatimaye  kujipenyeza kwa adui rushwa. Hivyo basi  tunaendelea kuwaagiza watendaji wote wa ngazi husika kusimamia matakwa ya Kimaadili, Kikanuni na Kikatiba.

Aidha  tunaendelea kuviomba vyombo vinavyohusika katika ngazi zote hasa TAKUKURU kuendelea na  kufuatilia kwa karibu nyendo za wagombea na wapiga kura ili kubaini kuwadhibiti na kuwachukulia hatua za kisheria. Mgombea au mpiga kura yoyote atakayethibitika kutoa au kupokea Rushwa, hatua za kimaadili na kisheria tunaelekeza zichukuliwe ili kulinda heshima ya taasisi yetu.

Tunaendelea kusisitiza kuwa uchaguzi wa UVCCM katika ngazi zilizobakia zitafanyika kwa misingi ile ile ya uhuru na uwazi huku kila mgombea akipitishwa na vikao vya kikanuni na kikatiba baada ya kukidhi mashariti ya uchaguzi kwa mujiba kanuni na katiba.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na malumbano yenye kupandikiza chuki na kupalilia mifarakano isio na ulazima huku baadhi wa watu wakiwachafua wenzao kwenye mitandao ya kijamii na wakati mwingine wapo wanaothubutu kuwatukana wenzao matusi ya nguoni kinyume na ustaarabu, ubinadamu na misingi na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi.

Wapo baadhi yao hujivika kofia ya Jumuiya wakitumia  njia hatari na batili, wamekuwa wakikebehi, kutuhumu wenzao kinyume na utaratibu huku baadhi yao hata kufikia kutoa madai  yanayovuka mipaka na   kubeba taswira ya  Jinai au  madai. 

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umestushwa na  hali hiyo inayoonekana kutaka kuibua migogoro na kujenga mazingira yanayotaka kuonyesha kana kwamba ndani ya Jumuiya kuna mvurugano au  kuporomoka kwa mshikamano wetu wakati mambo nayo  hayapo. 

Kimsingi  yote yanayofanyika ni kinyume na utamaduni wa Chama Cha Mapinduzi Kikatiba na Kikanuni na Kimaadili. CCM si genge la wahuni bali ni Chama makini  cha Siasa kinacho heshimu  utu wa mtu, taratibu na miongozo iliyojiwekea katika kushughulikia mambo yake.

Kwa miaka yote wanajumuiya na viongozi wamekuwa wakiishi kwa kuzingatia misingi ya Umoja, Upendo, mashauriano na kudumisha Maelewano.


Jumuiya yetu imekuwa ikifanya kazi zake kwa uwazi na umakini mkubwa. Tusingependa kuona ikitiwa nyufa au kukumbwa na athari za kutengenezwa na watu wachache. Nasema tena hatutasita kuchukua hatua stahili kwa mujibu wa kanuni Katiba ya Chama na ikibidi hata kisheria ili kukomesha vitendo hivyo vyenye nia ya kuondosha haiba nzuri ya Chama na Jumuiya katika kufanya mambo yake ya msingi.

Tumeanza kuwafatilia kwa karibu mno na kuanza kuwatambua wote ambao wanafanya au kushiriki vitendo hivyo vya aibu aidha iwe kwenye Jumuiya au ndani ya Chama chetu  

Chama Cha Mapinduzi na  Jumuiya zake  hujadili mambo yake aidha yakiwa magumu au mepesi kwa mujibu  wa ajenda na njia za majadiliano kupitia vikao halali hatimaye  maamuzi hutolewa baada ya kujiridhisha.  

Kimsingi utaratibu wa kushughulikia mambo mbali mbali ndani ya chama na Jumuiya zake uko wazi.

Yeyote mwenye madai, tuhuma au shutuma anatakiwa atumie vikao halali vya kikanuni na kikatiba   ama kuyafikisha kwa viongozi husika kwa kufuata utaratibu si kinyume na hivyo. 

Kwa kila mwana jumuiya muadilifu, msemakweli, mpenda Umoja na Mshikamano, siku zote huheshimu kanuni, taratibu, katiba na maelekezo yanayotolewa na viongozi wetu. 

LOWASSA KUMPIGIA KAMPENI UHURU KENYATTA

Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amesema atarudi nchini Kenya kumpigia debe Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta katika kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kurudiwa baada ya kufutwa na Mahakama.

Lowassa aliyekuwa mgombea wa urais nchini mwaka 2015 kupitia vyama vinavyounda Ukawa, August mwaka huu alikwenda nchini Kenya kushawishi raia wa nchi hiyo kumchagua Kenyatta kwa mara nyingine kuwa Rais wao katika uchaguzi uliofanyika August 8 mwaka huu.
Katika mahojiano na kituo cha Runinga cha Azam Lowassa amesema atafanya hivyo na ni kitu ambacho atakifurahia kukifanya.
Katika hatua nyingine Lowassa ameeleza sababu ya kumuunga mkono Kenyatta ingali yeye ni mpinzani nchini Tanzania.
“Kuwa upinzani ni barabara tu, nyenzo ya kufika sehemu fulani, nilipendezwa na Rais Kenyatta kwa anavyokubali mambo ya ushirikiano wa kimataifa, lakini la pili namuheshimu anavyoheshimu demokrasia na katika uongozi wake inalindwa, wabunge wana haki, vyama vina haki, kila mtu ana haki,” amesema Lowassa.
“La tatu uongozi wake ni wenye malengo, amerithi nchi imetoka katika migogoro ya kivita lakini kaingoza katika miaka mitano kimya wakijenga maendelea na wanatupita, kwa hiyo ni  Rais mwenye upeo, makini na mahiri ,” ameongeza.
Hiyo jana Mahakama ya Juu nchini Kenya ilifutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa Urais uliofanyika Agosti 8 mwaka huu, ambapo Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo, hivyo kurudiwa siku 60 zijazo.
Maamuzi hayo ya mahakama ni baada ya vyama vinavyounda umoja wa Upinzani (NASA), kupeleka malalamiko yao Mahakamani wakishutumu kudukuliwa kwa matokeo ya uchaguzi huo huku wakidai kuwa haukuwa wa huru na wa haki.

Friday, September 1, 2017

RUNGWE AZIDI KUCHOCHEA MOTO KUHUSU SWALA LA BOMBERDIER

Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ameibuka na kumtetea Tundu Lissu kwa kile alichofanya kutoa taarifa juu ya ndege ya Tanzania kuwekwa kizuizini Canada na kusema ametumia haki yake ya kikatiba ya kutoa habari kuhusu sakata hilo.     

Rungwe amezidi kuwashangaa watu ambao wanasema Tundu Lissu siyo mzalendo kwa kuwa alitoa taarifa hiyo na kusema uzalendo siyo kuficha  au kufanya siri ya mambo yanayohusu maisha ya Watanzania na kudai ni bora watu wajue ili mwisho wa siku hata maisha yanapokuwa magumu wajue kuwa zile fedha za Umma zimechukuliwa kwenda kulipa deni hivyo watu wafunge mkanda. 
Aidha Rungwe ameitaka serikali kufanya mazungumzo na watu hao japo waweze kuwapunguzia au hata kama kulipa kwa awamu ili mwisho wa siku ndege hiyo iweze kuja Tanzania na kuanza kufanya safari zake.

"Kesi ile imefikia katika hatua ya mwisho kabisa ya utekelezaji, wanasheria wana mbinu nyingi wanaweza kufanya jambo wale watu ambao ni wadai wakaelewa angalau kutupunguzia tukapata kanafuu fulani au tukalipa hata kwa awamu ni nafuu ndege yetu ikaja ikaanza kufanya daladala yake hapa na kupeleka watu hapa na pale kuokoteza hata hizo senti inaweza kujilipa yenyewe ila ukitumia utemi utemi si kila kitu unaweza kutumia utemi" alisema Rungwe. 

OFFICIAL VIDEO PATORANKING FT. DIAMOND PLATNUMZ - LOVE YOU DIE


Msanii wa muziki toka nchini Nigeria anayefahamika kama Patoranking aliyefanya vizuri na vibao vyake vingi vizuri kama My Woman My everthing pamoja na Girlie "O" na kwa sasa amekuja na wimbo wake mpya aliyomshirikisha Diamond Platnumz toka Tanzania.


Wimbo huu hapa unaitwa Love you die Patoranking ft Diamond Platnumz kwa kutazama au kudawnload bonyeza kwa chini hapa...
   

MAHAKAMA KUU NCHINI KENYA YAFUTA MATOKEO YA URAIS

Orengo: Tume ya uchaguzi imo mashtakani

Wakili mkuu wa Bw Odinga, James Orengo, amesema mahakama imefuata katiba kubatilisha uchaguzi wa urais.

Amesema anatumai tume itaandaa uchaguzi wa marudio kwa njia huru na ya haki.
"Desturi ya kutoheshimu sheria lazima ikomeshwe na wahusika waadhibiwe. Mwaka 2013, maafisa wa tume ilibainika kwamba walifanya makosa. Tume imo mashtakani. Kabla tufanye uchaguzi mwingine, tume lazima ichunguzwe. Sidhani tutakuwa na tume hiyo ikiandaa uchaguzi tena."

WAKIMBIZI 12000 WA BURUNDI KUREJEA NCHINI KWAO


WAKIMBIZI 12,000 kutoka nchini Burundi walioonesha nia ya kurejea nchini kwao na kujiandikisha, wanatarajia kuanza kurudi kuanzia Septemba 7, mwaka huu.
Aidha, serikali imesema atakayesema Tanzania inafukuza wakimbizi nchini, itabidi kukaa naye meza moja ili aeleze kuhusu kauli hiyo kwani kufanya hivyo ni kuchafua jina la nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema hayo jana katika mkutano wa Kamisheni ya Utatu inayoshughulikia kuwarudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao kwa hiari yao.
Mwigulu alisema kuwarejesha kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ni haki ya mkimbizi yeyote kuondoka na kurejea katika nchi yake. Alisema kwa kuwa kazi ya kuwarejesha itaanza Alhamisi ijayo, inawezekana kukawepo idadi kubwa ya wakimbizi wenye kuonesha nia ya kutaka kuondoka kwa hiari, lakini pia kazi ya kuwarejesha ni endelevu ambayo inaweza kuwa na ongezeko kubwa la wanaotaka kurudi.
Mwigulu alisema kwa maana hiyo ni wajibu wa mashirika ya kimataifa kusaidia na kuwezesha kazi ya kuwarejesha makwao pamoja na maeneo watakayoishi nchini Burundi ili kazi ya kuwarejesha iwe endelevu zaidi. “Ili kufikia lengo ni muhimu kupanga kwa umakini kwa kuangalia malengo ya mbeleni ya wakimbizi ili kuepuka kurudi kwa ghafla,” alieleza Mwigulu na kuongeza kuwa sheria za kimataifa zinahitaji kuona utayari wa nchi husika katika kutoa ulinzi kwa wakimbizi watakaorudi.
Alisema Serikali ya Tanzania inatambua hali ya Burundi imetulia na inaruhusu wakimbizi walio tayari kurejea nchini kwao kwani Agosti 22, mwaka huu, Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza alipokutana na Rais John Magufuli, alikiri hali kuwa shwari nchini humo na kwamba warudi wakajenge nchi yao.
Kuhusu Tanzania kufukuza wakimbizi, alisema vipo vyombo vya nje vilivyodhani kuwa Tanzania inafukuza wakimbizi, wakiongeza zaidi kuwa inatumia jeshi na kuwatoa kwa nguvu, jambo ambalo siyo la kweli.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Burundi, Pascal Barandagiye alisema ni muhimu kwa kamisheni hiyo kujiunga ili wakimbizi hao wanaoomba warudi mapema na isichukue muda mrefu sana. Alisema wako tayari kuwapokea warudi ili waende kusaidia kujenga nchi yao. 
Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya alisema ni muhimu kwao kuwa na imani na kule wakimbizi wanakokwenda kuwe na usalama kwa kuwa ni kazi inayokubalika kimataifa.



MAANDALIZI YA TAMASHA LA JINSIA YAPAMBA MOTO ANGALIA KITAKACHOJIRI KWENYE TAMASHA HILO

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa tamasha kubwa la jinsia linalotarajiwa kufanyika siku ya jumanne tarehe 5 mpaka 8 ya mwezi wa 9 katika viwanja vya mtandao wa jinsia TGNP.

Maandalizi yakiwa bado yanaendelea kwa upande wa wanaharakati wa semina za jinsia GDSS wameendelea kujipanga ipasavyo kuhakikisha wanaonyesha vitu vikubwa Zaidi kwa kuwa wao ndio wenyeji wa tamasha hili, na kusema kuwa hawatakubali kuja kufunikwa na wageni watakao kuja kwenye tamasha hilo.
Afisa Program na nguvu za pamoja wa TGNP Bi. Anna Sangai akiendesha semina ya GDSS kwa kuchukua maoni na kuangalia nini kifanyike kwenye Tamasha la Jinsia ili lizidi kuwa zuri zaid kwa mwaka huu.
Akiongoza semina hiyo afisa program wa nguvu ya pamoja Bi. Anna Sangai alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwa mwaka huu tamasha hilo litachukua Zaidi ya wanafunzi 150 wa shule za sekondari na msingi.

Miongoni mwa shule hizo ni shule ya msingi umoja na mabibo sekondari zilizopo kata ya mabibo kwa idadi ya 25 msingi na 25 sekondari ambazo zitakuja siku ya kwanza ambayo ni tarehe 5, na kundi la pili litakuwa kata ya mwananyamara ambalo pia ni wanafunzi 50, 25 shule ya msingi mchangani na shule ya sekondari makumbusho wanafunzi 25, na kundi la mwisho litakuwa shule ya msingi kilimani wanafuzni 25 na kipunguni sekondari wanafunzi 25 hizi toka kata ya kipunguni.

Aidha dada anna alipenda kuwasisitiza wanaGDSS kuwa wakarimu kwa wageni wote lakini pia kuwa na upendo ili wageni wajione wako nyumbani na kama ukiokota kitu cha mtu mwingine basi kipelekwe mahali husika ili kitangazwe na kupewa mwenye kitu chake ili wageni wafurahie tamasha na kuona TGNP ni sehemu nzuri na salama kwao.

Lakini sambamba na hilo wanaGDSS wametakiwa kuhakiki majina yao ili waweze kujua wamapangwa vitengo gani vya kutoa huduma na pia kwa ajiri ya kupewa vitendea kazi kama mabegi na Tshirt za tamasha hilo pamoja na huduma nyinginezo kama chakula nk.


Na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa kwanza wa rais mwanamke kwa Tanzania mama samia suluhu hassani na kusema kuwa amashapelekewa barua hivyo wanatarajia kama hatokuwa na shughuli nyingi za kiserikali ataungana na jopo kubwa la wageni katika tamasha hilo.


baadhi ya washiriki wa semina ya GDSS ya wiki hii wakisikiliza kwa umakini muongozo unaotolewa na kiongozi wao.
Bi. Heriet Kabende akichangia mada katika semina ya jinsia na maendeleo GDSS ilifanyika jumatano hii ikiwa semina ya mwisho kabla ya siku ya tamasha la jinsia linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Bw. Innocent Siriwa akitoa maoni kuhusiana na Tamasha la Jinsia linalotarajiwa kuanzia jumanne ya tarehe 5 mpaka ijumaa 9 katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Mabibo jijini Dar es salaam

Bi. Subira Kibiga akiendelea kuwafua wanafunzi wake kwa upande wa mashairi ili waweze kutoa kitu kizuri siku ya Tamasha la Jinsia linarotarajiwa kufanyika hivi karibuni.