Saturday, January 6, 2018

ANGALIA HAPA MAJINA YALIYOPITISHWA NA CCM YA WABUNGE WALIOTOKA UPINZANI NA KUGOMBEA TENA KATIKA MAJIMBO YAO.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kimewarudisha waliokuwa wabunge wa upinzani kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya wabunge hao kuijiunga na chama hicho.
 Picha inayohusiana
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole imesema kuwa baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Imesema kuwa wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo siku ya Jumanne, Januari 9 bila kukosa.

LISSU ASAFIRISHWA KUPELEKWA UBELGIJI KWA MATIBABU SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubeljiji kwa matibabu zaidi ya kuurejesha mwili wake katika hali yake ya kawaida.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kwenye makazi yake Dodoma.

Mwanasiasa huyo amesindikizwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na watoto wake pacha, Augustino na Edward, ndugu zake, viongozi na wanachama wa Chadema.

"Nawashukuru sana madaktari wa hapa Nairobi na wale wa Dodoma wakiongozwa na Katibu Mkuu (wa wizara ya afya Profesa Mpoki Ulisubisya waliookoa maisha yangu," amesema Lissu kabla ya kupandishwa gari la wagonjwa

"Nakwenda Ubelgiji kwa matibabu, nikirudi mapambano yanaendelea, nawashukuruni nyote mlioniombea, nawashukuru Wakenya na serikali yao ambao kwa miezi minne nikiwa hapa walinipa ulinzi wakati wote."

Akizungumza kwa msisitizo  mbele ya wabunge na wanachama wa Chadema waliokuwapo amesema "Chapeni kazi, mimi nitarudi kuendeleza mapambano haya."

Kuhusu gharama, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema gharama za safari na matibabu zimegharamikiwa na Chadema na TLS.

Baadhi ya waliokuwapo hospitalini kumsindikiza Lissu uwanja wa ndege ni kaka yake Alute Mghwai, mdogo wake, Vinceti Mghwai na ndugu wengine.

Pia, Dk Mashinji, Naibu Makatibu Wakuu, John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar).

Wengine walikuwapo ni wabuge wa Chadema, Susan Kiwanga (Mlimba) na Godbless Lema(Arusha Mjini), John Heche (Tarime Vijijini), Rose Kamili (Viti Maalum), Anna Gideria (Viti Maalum).

Kwa niaba ya familia, Alute amesema "Tunamwomba Mungu ajalie huko anakokwenda akapate matibabu, kwani alivyokuja hapa sivyo anavyoondoka na tunawashukuru wananchi wa Tanzania na Kenya kwa ushirikiano wao."

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akitolewa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

RAIS MAGUFULI AMTEMBELEA KINGUNGE HOSPITALINI MUHIMBILI

Rais  Magufuli akimjulia hali mzee Kingunge Ngombale Mwiru, katika wodi ya Mwaisela, Muhimbili. Mzee Kingunge amelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake



Ziara ya msemaji wa Jeshi la Polisi BBC

   Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP)  Barnabasi Mwakalukwa  akiagana na  meneja wa ushirikiano wa BBC Media Action, Agnes Kayuni  mara baada ya kumaliza mazungumzo na watendaji wa  BBC Media  Action leo  alipo watembelea ofisini  kwao kwa lengo la kuimarisha ushirikiano.  (Picha  na Jeshi la Polisi.
    Studio Meneja wa  shirika la utangazaji la BBC, Peter Mfalila akimuonesha Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP)  Barnabasi Mwakalukwa  namna studio ya BBC Dar es salaam inavyofanya kazi. (Picha  na Jeshi la Polisi


MBUNGE MGIMWA:WATENDAJI KAMATENI WAZAZI WOTE AMBAO HAWAWAPELEKI WATOTO WAO SHULE

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
  Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini

Na Fredy Mgunda,Mufindi.

 Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari.

Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu  viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.

“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ilogombe Pastor Haonga alisema kuwa wazazi wengi wa kata ya Kibengu wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Haonga

Haonga alimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kata ya Kibengu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Haonga.

Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu


Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu  alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi

Nao watendaji wa vijiji vitano vya kata ya Kibengu ambao ni Dominicus Nyaulingo,Saifod Mwengwa,Haruna Kalenga, Richard Mandili na Demetus Kanyika walisema kuwa wamepokea agizo la mbunge na watalifanyia kazi kwa ukamilifu kwa kufuata sheria ili kuhakikisha watoto wa kata hiyo wanapata elimu kama inavyotakiwa.

Na kata ya Kibengu inajumuisha vijiji vitano ambavyo ni kijiji cha Kibengu,kijiji cha Igereke,kijiji cha Ilogombe,kijiji cha Usokami na kijiji cha Kipanga

Friday, January 5, 2018

Tigo Yapata Mamilionea Wapya wa Mwaka Mpya 2018

Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kulia) akiongea kwa njia ya simu na moja wa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika usiku wa kuamkia mwaka mpya katika ofisi za Tigo ambapo Lugano Thomas Mlimi wa Dar es salaam, Kulthum Salim Ally wa Ruvuma na Maria Josef Maligisa wa Lindi walijinyakulia shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 katika promosheni hiyo. Katikati ni Meneja wa Mapato wa Tigo, Arnold Ngakashi na kushooto ni Mwakilisi wa Bodi ya Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Ally Abdallah.


Wateja watatu wajishindia TSH 15 milioni, 10 milioni na 5 milioni!
 Wengine 150 wajinyakulia zawadi za TSH 1 milioni na 500,000 kila mmoja!
                             Dar es Salaam, 31 Desemba, 2017

 ‘Nimeanza mwaka mpya nikiwa milionea!’ alisema Lugano Thomas Mlini, ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam alipotaarifiwa kuwa amejishindia shilingi milioni 15 kutoka Tigo.  

Kupitia huduma yake ya Tigo Pesa, kampuni ya simu inayoongoza ya Tigo imewageuza Watanzania watatu kuwa matajiri wapya kwa mwaka 2018.  

‘Ndoto zangu za kuanzisha biashara sasa zimetimia! Ahsanteni sana Tigo’ alisema Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma ambaye naye alijinyakulia kitita cha shilinigi 10 milioni katika drooo kabambe ya promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika siku ya mkesha wa kuamkia mwaka mpya, katika ofisi ya makao makuu ya Tigo jijijni Dar es Salaam.

‘Nilienda kulala nikiwa maskini na sasa nimeamka nikiwa tajiri’ alisema Mariam Josef maligisa, Mkulima na mkaazi wa Nagangu, Lindi aliyeamka kutoka usingizini ili kupokea simu yake na kutaarifiwa kuwa naye amejishindia  TSH 5 milioni kutoka Tigo.

Akitangaza washindi katika droo hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema, ‘Tigo pesa ni zaidi ya huduma ya kufanya malipo. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo leo tumewawezesha wateja wetu kutumiza ndoto zao za msimu wa sikukuu na Mwaka Mpya kupitia huduma ya Tigo Pesa.

Alibainisha kuwa Tigo imetoa jumla ya shilingi 120 milioni kwa watu 153 kutoka maeneo mbali mbali ya nchi. Wateja walishinda zawadi nono za kila siku baada ya kutumia huduma ya Tigo Pesa.

‘Pia tunajivunia mchango wetu katika kufanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Kupitia Tigo Pesa, tunawawezesha mamilioni ya Watanzania kutuma na kupokea zaidi ya TSH 1.7 bilioni kila mwezi. Hii inawawezesha wateja wenyewe pamoja na jamii, huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa nchi,’ aliongeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Willima Mpinga alisema kuwa,’Tigo inawatakia Watanzania wote Mwaka Mpya wenye furaha na mafanikio. Tigo ni mtandao unaowaelewa zaidi wateja na kujibu mahitaji ya soko.  Tulizindua promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde kwa dhumuni kuu la kuwawezesha wateja wetu kushinda pesa zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ya mwisho mwaka.’

Tigo Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu ya pili kwa ukubwa nchini.  Tigo Pesa ina mtandao mpana zaidi wa wakala na watoa huduma zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.  Tigo Pesa pia ilikuwa ndio huduma ya kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kutuma fedha kwenda nchi nyingine kwa kutumia viwango na fedha za nchi husika.

Tigo ndio kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ikijivunia huduma bora za sauti, SMS, intaneti yenye kasi ya juu zaidi ya 4G iliyosambaa katika miji 24 nchini, pamoja na huduma za kifedha. Mtandao wa Tigo pia ni maarufu kwa promosheni na ofa zake bunifu kwa wateja.

Tigo ilianza kutoa huduma zake Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu sasa ndio kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 11.6 milioni.


Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde

Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tigo, Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde. Amezingirwa na baadhi ya washindi 153 wa promosheni hiyo waliojinyakulia vitita vya shilingi milioni 15, TZS milioni 10, TZS milioni 5, TZS milioni moja na TZS 500,000 kila mmoja.



Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 5 milioni kwa Mariam Maligisa, mkulima kutoka Nagangu mkoani Lindi, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 





Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 10 milioni kwa Kulthum Salim , mkulima kutoka Tunduru mkoani Ruvuma, aliyekuwa moja wa washindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) pamoja na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Hussein Sayed (katikati) wakikabidhi mfano wa hundi ya TZS 15 milioni kwa Lugano Thomas , ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde aliyekuwa mshindi katika promosheni ya 'Tumia Tigo  Pesa na Ushinde'. Jumla ya washindi 153 kutoka maeneo mbali mbali nchini walijinyakulia zawadi za TZS 500,000 hadi TZS 15 milioni katika promosheni hiyo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari (aliyeketi wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi washindi wa promosheni ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde' ambapo jumla ya wateja 153 walijishindia zawadi tofauti za  TZS 15 milioni, TZS 10 milioni, TZS tano milioni na zawadi za kila siku za TZS milioni moja na TZS  500,000 kila mmoja.

Thursday, January 4, 2018

SIMU NYINGINE KALI IKIWA YA KWANZA KUTOKA TECNO.

TECNO kampuni ya simu za mkononi iliyojizolea umaarufu barani Africa na Mashariki ya kati kupitia uzalishaji wake wa simu janja (smart phone) imeendelea kushika chati katika masoko mbalimbali barani Afrika.


Kama ilivyo kwa kila mwaka, kampuni ya TECNO huzindua simu mpya na hua ni muendelezo wa matoleo yaliopita. Kwa mwaka huu TECNO wanaachilia simu ikiwa ni muendelezo wa simu aina ya CAMON. Camon imekua moja wapo ya simu janja (smartphone) pendwa sana kwa wadau kwa mwaka 2017!
Wanatarajia kuachilia simu hio ndani ya miezi ya kwanza (Januari – March) mwaka huu na itakua ni simu ya kipekee kwani itakua na vigezo maalumu kulinganisha na simu zingine zilizopita kabla!

Kadri miaka inavyosogea na kuendelea teknolojia ya simu, miundo ya simu, vigezo, mahitaji na matumizi ya simu hubadilika na kuongezeka, hivyo kama kampuni imekua ni jambo muhimu kuweza kutoa simu zinazokidhi mahitaji ya wadau na watumiaji wa bidha zake hivyo kutoa toleo jipya kabisa!
Je, ni simu gani na itakua na vigezo/muundo gani?
Fuatilia kurasa za TECNO katika mitandao ya kijamii na tovuti yao kujua zaidi!

WANANCHI WA VIJIJI 11 WAITAKA SERIKALI KUMALIZA KAMATA KAMATA YA WANANCHI INAYOFANYWA NA ASKARI WA MKUNGUNERO



Na Woinde Shizza,Kondoa

Wananchi wa vijiji 11 kwenye kata sita wilayani Kondoa wameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kumaliza migogoro inayotokea kati yao na Askari wa Pori la Akiba la mkungunero kwani wananchi hao wamekuwa wakibambikiwa kesi za  mara kwa mara na Askari hao na kugeuzwa miradi kwa madai ya mifugo.
Tokeo la picha la AKARI WA WANYAMA POLI
Licha ya mda mrefu kupita na kutulia kwa migogoro pembezoni mwa pori la akiba la Mkungunero na Wananchi wa vijiji 11 bado kumekuwa na kamata kamata ya wananchi na kujikuta wanafunguliwa kesi ambapo mifugo zaidi ya 146 inashikiliwa na Askari wa wanyapori ndani ya hifadhi hiyo huku wananchi watatu wakishikiliwa tokea demember 26 mwaka jana na kesi yao ipo mahakamani hadi december  5 mwezi huu.


Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi hao Diwani wa Kata ya Itaswi Issa Chobu alisema kuwa licha ya mgororo huo kuwepo kwa mda mrefu lakini Tatizo kubwa ni Serikali kushindwa kufuatilia ripoti ya tume iliyoundwa waziri mkuu ya mwaka 2012 ili wananchi waliohamishwa ndani ya hifadhi wakati huo walipwe fidia zao.


Alisema kuwa licha ya wananchi kukaa na viongozi wa Pori hilo la Akiba na kuona wanatatatuaje matatizo ya unyweshaji wa maji mifugo na wananchi kutumia maji hayo kwa matumizi yao bado tatizo kubwa kwenye mgogoro huo ni huduma bora ya maji na hilo litaondoa tatizo la mifugo na wananchi kuingia ndani ya hifadhi .

“Mimi kama mwakilishi wa wananchi naiomba serikali kuangalia upya ripoti ya tume iliyoundwa na waziri mkuu pinda wakati huo naona hii itasaidia kuondoa dhana nzima ya migogoro na kurudisha uhifadhi shirikishi kwa maendeleo ya taifa na uhifadhi.”alisema Chobu
Nae Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kutish Adamu Ally amesema kuwa wao kama majirani wema wa hifadhi waliomba kunywesha mifugo kwenye mto unaoanzia milima ya haubi na kupita mita 120 ndani ya hifadhi karibu na kitongoji changu katika kikao chao na viongozi wa pori hilo la Akiba mwezi wa Tano mwaka jana na kukubaliwa lakini kwa kipindi cha kiangazi lakini cha kushangaza kila wakipeleka mifugo kunyesha wamekuwa wakikamatwa na kutozwa kiasi cha 50,000  kwa kichwa cha mfugo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa malalamiko yao mara kwa mara lakini wananchi wameendelea kukamatwa na kufunguliwa kesi kama wenzao watatu wamekamatwa toka desember 26 na kufikishwa mahakamani licha ya wao kutokuwepo  wakati mifugo inakamatwa.

Juhudi za kumpata Meneja wa Pori hilo la Akiba kwa njia ya Simu zinaendelea licha ya kuwa alikuwa hapatikani hewani ili aweze kujibu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwenye uongozi na watumishi wa Poti hilo la Akiba la Mkungunero

Gazeti hili limefika kwenye eneo la tukio na kujionea na kusikiliza pande mbali mbali za serikali za vijiji hiyo na kata na kugundua kama serikali itafuata ushauri huu basi mgogoro huo utakuwa Historia,Moja Kuanzisha(WMA) Uhifadhi shirikishi,Pili uwepo wa Ujirani Mwema,na Tatu  kuisaidia huduma za kijamii kwa mapato inayotokana na uwindaji kwenye hifadhi hizo za Akiba.

MKE WA KINGUNGE AFARIKI DUNIA HUKU MUMEWE AKIWA AMELAZWA

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

IGP AKAGUA MIRADI KINONDONI

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza OCD wa  Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni, Salim Marcuse, wakati alipotembelea moja kati ya miradi ya maendeleo ya  Jeshi hilo inayotekelezwa katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar es salaam. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akikagua mradi wa maendeleo ya Jeshi hilo unaotekelezwa katika Wilaya ya Kipolisi ya Magomeni jijini Dar es salaam, mradi ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za Kipolisi hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi.

Wananchi wa Kigogo Mburahati jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, ambaye alifika eneo hilo kwa ajili ya kukagua moja kati ya miradi ya Jeshi la Polisi, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi hao kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kuwafichua wahalifu katika maeneo yao. Picha na jeshi la polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro, akimsikiliza Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, wakati alipofanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Jeshi hilo Mbweni jijini Dar es salaam katika wilaya ya kipolisi ya Kawe. Picha na Jeshi la Polisi.