Saturday, November 26, 2016

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA KAMPALA JIJINI DAR ES SALAM

 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.

Mahafali yakiendelea
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

JUKWAA LA WASTAAFU WA TAALUMA YA ELIMU WATOA RAI MABADILIKO YA MITAALA


Jukwaa la wastaafu wa taaluma ya elimu limesema ni lazima kunapokuwepo kwa mabadiliko ya mitaala ya elimu mipya ni vyema ikatengenezwa kwa kufuata sheria ya elimu na sera ya elimu ili kuepuka mgogoro wa elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,mwenyewekiti wa Jukwaa la wastaafu wa Taaluma ya Elimu  profesa HERME MOSHA amesema  endapo kutakuwa na mkanganyiko wa mitaala ya elimu kuandaliwa bila kufuata sheria ya elimu na sera ,basi ni makosa katika maendeleo ya elimu.

Mwenyekiti huyo wa jukwaa la wastaafu  wa taaluma ya elimu profesa MOSHA ameongeza kuwa hakuna sheria inayosema elimu ni bure,ila ni vyema wakajua kuwa sasa hakuna malipo ya ada(karo) katika mashule.

Profesa MOSHA amefafanua kuwa elimu bure ni pale unapoona mwanafunzi anapopewa kila kitu anapoingia na anapotoka shule hasa uwepo wa chakula,usafiri pamoja na mambo mengine .

Hata hivyo Jukwaa la wastaafu wa taalumu ya elimu limeeleza kuwa lengo la kuanzishwa ni kuwakutanisha wastaafu wataalumu ya elimu ili waweze kubadilishana uzoefu wa hali ubora wa elimu nchini pamoja na kujitathimini wapi Walikosea .

SERIKALI KUENDELEA KUVIFUTIA USAJILI VYUO AMBAVYO HAVINA SIFA NCHINI

Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Dk. Magreth Shawa na Naibu Ktibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo (kulia), wakiteta jambo kabla ya maandamano ya kuelekea eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mahafali ya 11 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

Friday, November 25, 2016

MILIONI 10 ZA UJENZI WA CHOO ZAYEYUKA MANISPAA YA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM BILA CHOO KUKAMILIKA

 Choo cha Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kikiwa kimeng'olewa milango kutokana na kutokamilika ujenzi wake licha ya manispaa hiyo kutenga sh.milioni 10 za ujenzi. 
 Mkazi wa Temeke akipita mbele ya choo hicho.
Mwonekano wa moja ya tundu la choo hicho ambacho hakina miundombinu ya mifereji.

POPULAR GERMAN TV SERIE “TRAUM SCHIFF”FILMS EPISODES IN TANZANIA.

Some of the German film actors and actresses in discussion as shooting of the film is in progress in the West Kilimanjaro nearby Arusha National Park
 By: Geofrey Tengeneza
A German filming company called  PolyPhone Crew  accompanied by actors and actresses from Germany are in the country to film a renown German TV serie called "Traum Schiff" shown on a German TV channel namely ZDF which  is very popular in Germany, Switzerland and Austria, attracting more than 17 million viewers.

The team jet in Dar on November 9th and will be in Tanzania for a filming mission of 21 days until November 30th. . The lead actor in the serie which is being filmed in Tanzania is called Hardy Kruger Jr., son of famous actor Hardy Kruger who along with a very prominent US actor  John Wayne acted in the world famous "Hatari " film which was filmed  in Tanzania’s Arusha National Park.

The episodes which are being filmed in Tanzania will among other things feature some of Tanzania's leading tourist icons: Mt Kilimanjaro, Serengeti and Arusha National Park and is scheduled to start being aired in March 2017. So far the team has done most of their shooting at Shu’mata Lodge, located in West Kilimanjaro. They are also expected to visit and shoot in Zanzibar.

Speaking in West Kilimanjaro when she recently met the crew and film actors and actresses, the Managing Director of Tanzania Tourist Board Ms. Devoda Mdachi noted that the Tanzania Tourist Board (TTB) applauds the filming company for considering Tanzania as a proper and excellent location to shoot the film.  “We really acknowledge Polyphone Filming Company for choosing Tanzania as their filming location for this film. We believe that through this film many prospective tourists from Germany, Switzerland and Austria will be enticed to come to visit Tanzania's tourist attractions’ she noted.
Film actors and actresses and the PolyPhone crew from Germany pose for group photo with the Managing Director of Tanzania Tourist Board Ms. Devota Mdachi (in red dress) at Shi’mata lodge in West Kilimanjaro. The man in safari attire with cowboy hat (second left to Ms. Mdachi) is Mr. Hardy Kruger Jr, son of Hardy Kruger who starred the popular “Hatari” film.
Mdachi further said that the filming will also create more awareness to international film producers that Tanzania is a destination which has perfect locations for filming opportunities. She added that the filming industry brings in thousands of opportunities to destinations, including generating revenue, creating employment opportunities and compliment in the efforts to promote the destination.

Apart from Tanzania Tourist Board a number of Tanzania tourism stakeholders were involved in making the crew visit a success, this includes the Embassy of Tanzania to Germany, The Germany embassy in Dar-es-salaam, The Ministry of Natural Resources and Tourism and Marlies and Jorg Gabriel of Hatari Lodge Arusha. Others are The African Embassy Ltd, Tanzania National Parks, Abercrombie& Kent, Coastal Aviation, The Cultural Heritage Arusha and The Enduimet Wildlife Management Area (WMA).

CDEA WAZINDUA MRADI WA ATAMISHI YA KAZI ZA SANAA ‘IIDEA’ KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.
\
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika Mashariki kupitia Sanaa zao.

“Sanaa ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.
Pia alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika kuweza kubuni vazi la Taifa.
“Kwa kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu. Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa, Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza Habibu Msammy.

Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.
Katika uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu, maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.
dsc_1296
Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
dsc_1306
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo

VIJANA WAJASILIAMALI KUTOKA MIKOA MBALIMBALI YA TANZANIA WATEMBELEA SIDO DAR KUJIFUNZA UZALISHAJI



 Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.  Picha na Mafoto Blog
 Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya vijana wakiangalia jinsi Jora linavyotengenezwa.....
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 

Thursday, November 24, 2016

MAGARI MAPYA 25 YAKABIDHIWA BAADA YA KAMPENI YA WHITEDENT YA KUADHIMISHA MIAKA 25 KUISHA.

Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabishi Emannuel Sitta Mfano wa Funguo wa gari baada ya kuibuka mshindi wa Kwanza katika Promosheni ya Whitedent iliyoendeshwa nchi nzima.Hafla hiyo imefanyika leo Jijini Dar es salaam
 24 Novemba 2016. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza katika bidhaa za afya ya mdomo Whitedent imekabidhi magari 25 ya aina ya Suzuki Alto K10 kwa washindi kutoka mikoa mbali mbali nchini walioshiriki promosheni ya miezi mitatu iliyokuwa inasheherekea kuadhimisha miaka 25 ya biashara hiyo.
Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi HAMISI SAID  zawadi ya gari baada ya kuibuka mshyindi wa Tatu katika Promosheni hiyo 
Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi Julai mwaka huu ilitoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hilo kwa kukisia idadi ya pakiti za whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya aina ya Suzuki yaliyokuwa yakizunguka nchi nzima wakati wa promosheni. Washiriki walitakiwa kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha promosheni na kukisia jibu sahihi ili waweze kuingia katika droo kubwa ya kujishindia moja ya magari hayo ya Suzuki Alto 10 kabla ya mwisho wa Oktoba mwaka huu. 

Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi Ramadhani Khamis Ramadhani Zawadi yake baada ya kuibuka mshindi wa Nne katiika Promesheni ya whitedent ya kushindania Gari
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Uendeshaji wa Chemi & Cotex Raja Swaminathan alisema, “Nina furaha leo ya kuyakabidhi magari haya kama ishara ya kusheherekea miaka 25 ya mafanikio pamoja na jamii yetu. Tofauti na mashindano mengine yoyote, kila mshindi atapokea gari  lenye maili sifuri pamoja na kadi yake ya usajili, bima ya mwaka mmoja, likiwa limejazwa mafuta tenki nzima na gharama zote za kodi kulipwa. Hii haijawahi kufanyika nchini Tanzania.”

Shindano hilo lililokuwa chini ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania lilichukua miezi mitatu na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

"Tulitaka kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika shindano hili. Bidhaa ya Whitedent ni ya kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa na Watanzania. Safari ya promosheni ilipita sio mijini tu bali pia katika vijiji ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kushiriki,” aliongeza Raja Swaminathan, Afisa Mkuu Uendeshaji wa Chemi & Cotex.
Mkurugenzi wa Viwanda na biashara Mh OBADIA NYAGIRO ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi Abdul Feresh  zawadi ya Funguo baada ya kushinda Gari 
Inakadiriwa kuwa zaidi ya wana Afrika mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent. Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa Whitedent ina asilimia 79 ya soko nchini na hupatikana katika maduka makubwa ya bidhaa hadi kwenye vioski vidogo.

Whitedent, inajivunia kuwa na asili ya Tanzania na ni bidhaa inayotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu katika kiwanda chenye vifaa vya kisasa jijini Dar es Salaam. Vilevile dawa hii ya meno hutengenezwa kwa viwango vya kimataifa.
Washindi wanne wa zawadi ya magari waliokabidhiwa leo Jijini Dar es salaam
“Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa viwanda nchini kwetu ni mkubwa na tuna nafasi kubwa ya kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa Watanzania kwa bei nafuu na pia kuweza kuuza ulimwenguni kote. Tunajivunia kuwa katika viongozi wa mafanikio haya,”alimalizia Swaminathan.
Hafla ya makabidhiano ya magari imefanyika leo rasmi katika mikoa ya Dar es Salaam, Moshi, Mbeya na Mwanza. Miongoni mwa washindi hao kutoka Dar es Salaam ni Emmanuel Sitta, Hamisi Saidi Shabani, Abdu Idd Fereshi, na Ramadhan Khamis Ramadhan. Washindi kutoka Mtwara, Arusha, Dodoma, Iringa na Shinyanga wanatarajia kupata magari yao tarehe 26 Novemba na wale kutoka Kigoma, Tabora, Morogoro, Musoma na Zanzibar tarehe 29 Novemba 2016.

Azam FC kusaka vijana U-17 Mwanza J’MOSI

VIJANA wa Kanda ya Ziwa mpo tayariii? Hii ni habari njema kwenu kwani Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imepanga kuendesha msako wa vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘U-17’ Jumamosi ijayo Novemba 26, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza.
Mpango huo wa kitaifa wa mabingwa hao uliopita kwenye mikoa mingine mitano nchini, utafanyika kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi 9.00 Alasiri ndani ya jiji hilo lenye historia ya kutoa wachezaji wengi wenye vipaji waliowahi kutamba na wengine wakitamba hivi sasa nchini.
Mara ya mwisho zoezi hilo lilifanyika jijini Mbeya na kuhudhuriwa na vijana 433, ambapo Azam FC ilivuna vijana 10 pekee watakaoingia kwenye mchujo wa mwisho utakaofanyika mwezi ujao kwenye makao makuu ya Azam Complex, Chamazi.
Mpaka sasa kwenye mikoa yote hiyo mitano, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma, Visiwani Zanzibar na Mbeya, Azam FC imechagua jumla ya vijana 60 kati ya vijana 2,999 waliofanyiwa usajili.
Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.


BARAZA LA WAHITIMU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE LAKUTANA KUJADILI MUSTAKABARI WA CHUO


 Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), akihutubia wakati akifungua Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Dar es Salaam leo.
 Katibu wa Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Jumanne Muruga (kushoto), akihutubia katika baraza hilo.
 Mwenyekiti wa Baraza hilo, Simon Simalenga (katikati), akiongoza baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila na kushoto ni Katibu wa baraza hilo, Jumanne Muruga.

 Diwani wa Kata ya Mbezi, Humphrey Sambo ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya chuo hicho (MASO), akichokoza mada katika baraza hilo.

PUMA KUTANGAZA UTALII WA TANZANIA DUNIANI KWA KUTUMIA NDEGE 22 ZA ZAMANI

 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, moja ya picha ya ndege  22 za zamani zitakazotua nchini Novemba 28, mwaka huu, kwa mashindano ya 'Vintage Air Rally' yenye lengo la kutangaza utalii. Ndege hizo zilitengenezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.Kushoto ni  Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti akiwaonesha wanahabari  (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ambamo Mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitatua na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange.
 Meneja wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (katikati) akizungumza katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) Dar es Salaam leo, kuhusu  maandalizi wa mashindano ya Ndege 22 za zamani  'Vintage Air Rally' zilizotengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930 zitakazotua nchini Novemba 28 na kutangaza utalii pamoja na kukusanya fedha za misaada kwa jamii.  Kulia ni Meneja Rasirimali Watu wa kampuni hiyo, Loveness Hoyange na Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.
 Mkuu wa Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza.akijibu maswali ya wanahabari
 Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Mafuta ya Ndege ya kampuni hiyo, Andrew Lauwo (kulia)  akifafanua jambo katika mkutano huo
Mkutano ulivyokuwa


Wednesday, November 23, 2016

Mwenyekiti Aomba Kupigwa Risasi Mbele ya Makonda Baada ya Kubanwa na Wananchi


Mwenyekiti soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani ameomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.

mokio-hassan

Mwenyekiti akijitetea mbele ya Wananchi

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

miny3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
miny1
miny2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es  Salaam.lukub