Saturday, January 28, 2017
HUU NDIO UJUMBE WALIOTUMA WACHIMBAJI WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA,WADAI WAPO HAI,WATAKA CHAKULA NA SIGARA
RAIS MAGUFULI AVUNJA MWIKO...AKWEA PIPA KWENDA ETHIOPIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 28 Januari, 2017 ameondoka nchini na kuelekea Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia ambako atahudhuria mkutano kilele wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.
Friday, January 27, 2017
TAMKO KUTOKA LHRC KUKEMEA MAUAJI YA RAIA NA UKIUKWAJI WA MISINGI YA HAKI ZA BINADAMU

Ndugu
Wanahabari,
Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu ni shirika lisilo la kiserikali ambalo si la kisiasa wala kibiashara
lenye kujibidiisha katika kutetea, kulinda na kuendeleza haki za binadamu na
utawala bora nchini. Kimekuwa kikifuatilia na kukusanya taarifa mbalimbali za
matukio ya ukiukwaji wa haki za Binadamu na mwenendo wa serikali na taasisi
zake ili kuhakikisha ulinzi wa haki hizo na utendaji wa serikali unafuata misingi ya
sheria na haki za Binadamu.
ZIARA YA NAIBU WAZIRI MASAUNI MKOANI RUKWA ATEMBELEA IDARA ZILIZOPO CHINI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen akitoa taarifa
ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(kulia), wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea idara zilizopo chini
ya wizara yake.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
UWANJA WA TAIFA MPYA RUKSA KUTUMIKA,TFF WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufunguliwa tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kadhalika, TFF inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa juhudi zake na kwamba namna aliyoonesha ushirikiano kufanikisha suala la kufunguliwa uwanja huo uliofungiwa matumizi yake na Serikali, Oktoba mwaka uliopita.
TFF inachukua nafasi hii kuahidi kuwa itasimamia matumizi mazuri ya uwanja huo kwa kutoa elimu kwa wadau ili kuutumia uwanja huo vema ikitambua kuwa ni hazina ambayo imetokana na nguvu na gharama kubwa za Serikali kuujenga uwanja huo.
TFF inatahadharisha mashabiki wa mpira wa miguu kwamba uwanja huo umejengwa kwa gharama kubwa hivyo ni jukumu letu kuutuza na kuutumia vema kwa sababu ni hazina kubwa tuliyonayo na ni miongoni mwa urithi bora kwa vizazi vijavyo.
Kwa sasa tumetuma maombi yetu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutumia uwanja huo kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Januari 28, mwaka huu kati Simba na Azam utapigwa kwenye uwanja huo wa Taifa, Dar es Salaam kadhalika keshokutwa katika mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam na Mwadui ya Shinyanga.
Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inaonesha kuwa ligi hiyo huko Mbeya kutakuwa na ‘derby’ kwa maana ya mchezo wa upinzani baina ya timu zinazotoka mkoa mmoja wa Mbeya ambazo ni Tanzania Prisons na Mbeya City utakaochezwa na Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Keshokutwa Jumapili Januari 29, mwaka huu kutakuwa na mchezo mwingine ambao Young Africans itacheza na Mwadui jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Majimaji ya Songea itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Jumatatu Januari 30, 2017 kutakuwa na mchezo mwingine kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wakati JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
..………………………………………………………………………… ........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
TIZAMA HII KUTOKA KWA FREMAN MBOWE LEO
Thursday, January 26, 2017
CHADEMA WAPATA MSIBA KANDA YA VICTORIA
Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri.
Huyu ndiye Mkuu wa Wilaya mteuliwa wa Mh Magufuli aliyeamua kuachia Ngazi leo
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw. Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-Picha kwa hisani ya Kapipij blog
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka waandishi wa habari waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi wa habari
RUFAA YA POLISI DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Posts (Atom)






