Friday, January 31, 2014

TIZAMA AFANDE SELE ALIVYOJITAMBULISHA RASMI CHADEMA




 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro .
ENDELEA HAPO--------

PICHA NNE ZA MAISHA MAPYA YA BABU WA LOLIONDO BAADA YA KUWANYWESHA KIKOMBE




 
Hii ni nyumba aliyokuwa anaishi Babu Ambi kabla Dozi ya Kikombe haijachanganya

RATIBA KAMILI YA LIGI KUU BONGO WEAKIEND HII,SIMBA USO KWA USO NA JKT OLJORO



         Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaingia raundi ya 16 wikiendi hii kwa mechi nne ambapo kesho (Februari 1 mwaka huu) Simba itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
ENDELEA CHINI-------

Wednesday, January 29, 2014

breaking newzzzz---tafadhali kama hujiamini usifungue,TRNI YA MWAKEMBE YACHINJA MTU USIKU HUU HAPA MABIBO MWISHO,TIZAMA PICHA






BREAKING NEWS:. MAKUNGA, KIBANDA, MWIGAMBA WASHINDA KESI YA UCHOCHEZI

 
Theophil Makunga.

Absalom Kibanda.

Samson Mwigamba.

             MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam  imetoa hukumu ya kesi ya makala iliyodaiwa kuwa ya uchochezi iliyokuwa inawakabili Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga, Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima ambaye sasa ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Absalom Kibanda  ambapo wameibuka kidedea baada ya ushahidi upande wa mashitaka kutojitosheleza.

BREAKING NEWZZ----HAWA NDIO VIONGOZI WA CCM WANAOTAJWA KUANZISHA CCJ,MWENYEKITI WAO AWATAJA LIVE,ASEMA WANA KADI MBILI WARUDISHE MARA MOJA

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA JAMII CCJ BW RICHARD KIYABO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

        Mwanzilishi wa chama cha kisiasa cha CCJ ambaye kwa sasa amekikimbia chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM leo ametoa kali ya mwaka baada ya kuitaka CCM iwape adhabu wanachama wake ambao wanamiliki kadi mbili yani ya CCJ na CCM huku akiwataja kwa majina
       
        Bw RICHARD KIYABO ambaye ndiye aliyeanzisha chama cha CCJ leo amejitokeza mbela ya wanahabari jijini dar es salaam na kusema kuwa amemwandikia barua makamu mwenyekiti wa ccm mh PHILIPO MANGULA akimtaka achukue hatua kali kwa wanachama wake ambao sio waadilifu kwa chama chake na wamekisaliti chama chao na kwenda kuanzisha CCJ kwa lengo la kukiua CCM
  
         “nashangaa ndani ya chama bado kuna wanacham na viongozi waandamizi wana kadi mbili yani ya CCM na CCJ na wameshindwa hadi sasa kuzirudisha na kuomba radhi kwa wanachama kwa usaliti huo”alisema bw KIYABO.



MAJINA YA MICHANGO YA CCJ YA KUANDAA MAANDAMANO AMBAYO VIONGOZI WA CCM NAO WANATAJWA KUCHANGIA
           Bw KIYABO pia aliayaambatanisha majina ya wanachama wa ccm waliowahi kushiriki katika kuchanga hela kwa ajili ya kukisaidia chama cha CCJ kufanya maandamano ya amani nchi nzima huku orodha hiyo akiwa na majina ya viongozi wakubwa wa CCM kama mwakyembe, samweli sitta nape,anna kilango na wenginme wengi

KAZI 907 KUSHINDANISHWA KATIKA TUZO ZA WAANDISHI ZA AJAT MWAKA HUU

KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA MCT AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Braza la habari Tanzania MCT limetangaza kupokea jumla ya kazi 907 za waandishi wa habari ambazo zitashindaniwa katika tuzo za waandishi wa habari zitakazofanyika mwaka huu katika ukumbi wa mlimani city march 14
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini dar es salaam katibu mtendaji wa baraza hilo bw KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa idadi hiyo ni pungufu kidogo ya kazi zilizopelekwa mwaka jana ambapo kazi 946 zilikusanywa.
Amesema kuwa katika waandishi waliioongoza kupeleka kazi nyingi bado wanatoka makampuni ya mwananchi communication kama ilivyokuwa mwaka jana,huku akisisitiza waandishi kujifunza kushiriki katika tuzo hizo kwani zitaajengea uzoefu mkubwa.
Washindi wa tuzo hizo watakabidhia zawadi zao katika usiku wa march 14 mwaka huu katika ukumbi wa mlimani city ambapo mgenirasmi anatarajiwa kuwa raisi wa mahakama yay a jumuiya ya Africa mashariki mh jaji HAROLD NSEKELA

Tuesday, January 28, 2014

MANENO ALIYOYAANDIKA ZITTO KABWE KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK ,YAWALIZA WENGI YASOME,SASA AMERUDI KWA MUNGU WAKE


MUNGU WANGU TUSAMEHE,MWIZI WA BODABODA HUKO MAFINGA ACHOMWA ABANIKWA KAMA KUKU,samahani kwa picha hizi


Anavyoonekana majereha ya mgongoni
 
Sehemu ya miguu yake
        Ezekiel Kaganga (29) mkazi wa Mjimwema Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga baada ya kubanikwa kwenye moto kama kuku akituhumiwa kuiba pikipiki (bodaboda).
ENDELEA KUISOMA--------

HABARI ILIYOTIKISA NCHI LEO NI MSANII WA BONGO MOVIE KUJINYONGA LEO HUKO TANGA AKIWA KAZINI


           MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR  ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
ENDELEA HAPA----------

TANGAZO MUHIMU KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF



                       MADAKTARI VPL KUWASILISHA VYETI TFF

         Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kufikia Februari 8 mwaka huu.
ENDELEA--------

breaking newzzz---CCM YAFANYA MKUTANO MKUBWA TANDALE JIONI HII,IDDI AZANI NA MADABIDA WAFNIKA WASEMA HAKUNA CHA SERIKALI TATU HAPA NI MWENDO WA SEREKALI MBILI HADI MWISHO WA DUNIA

BURUDANI KAMA KAWA

         Chama cha mapinduzi ccm jioni hii kimefanya mkutano mkubwa jijini dar es salaam katika kata za tandalemkutano wa muendelezo wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa cham hicho  ambapo viongozi mbalimbali wa chama hicho wamehudhuria akiwemo mbunge wa kinondoni mh IDDI AZAN pamoja na mwenyekiti wa chama mkoa wa dare s salaam  hicho mh RAMADHANI MADABIDA ambapo wamezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo swala la katiba na serikali tatu.
MAMIA YA WAKAZI WA TANDALE WAKIWASILIZA VIONGOZI WAO

KARIBU UZUNGUMZE NA WANANCHI WAKO BABA

MBUNGE WA JIMBO LLA KINONDONI MH IDDI AZANIA KIWAHUTUBIA WAKAZI WA TANDALE MUDA MFUPI ULIOPITA
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la kinondoni mh IDDI AZAN amesema kuwa ccm imetekeleza mambo mengi tofauti na mambo ambayo wapinzani wamekuwa wakiyasema kuwa hayaendi na kuwabeza jambo ambalo amesema kuwa ni uongo kwani bila ccm mambo mengi hayawezi kwenda

MWENYEKITI WA CCM MKA WA DAR ES SALAM ALIKUWA MGENI RASM KATIKA MKUTANO HIO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM AMBAPO
Akizungumza mbele ya umati wa wakazi wa tendele jijini leo amesema kuwa serikali mbili ni msimamo wa chama cha mapinduzi na hakuna wa kuwababaisha katika hilo kwani wana sababu nyingi za kusimamia swala hilo na wanaotaka serikali tatu wana yao mambo na ni wasaliti wan chi yao.
“hatuwezi kuwa na serikali tatu bila ya kuvunja muungano hivyo kuvunja muungano ni usaliti kwa waasisi wa nchi hii na tutakuwa hatujawatendea haki watanzania na wapenda amani wanchi hii”amesema madabida
Ameongeza kuwa mtu anayetaka mfumo wa serikali yatu haitakii mema nchi ya Tanzania na ni msaliti mkubwa nahafai katika nchi hii,kwani Tanzania imepatikana kwa taabu hivyo haiwezi kuvunjwa kirahisi kama watu wanavyofikiria na huo ndio msimamo wa chama