Saturday, November 29, 2014

FILAMU YA ESCROW YAMALIZIKA,HAYA NDIO MAAZIMIO MAPYA NANE YA BUNGE

Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe amesoma maazimio mapya ya Bunge kwa mujibu wa kamati maalumu iliyoundwa leo na kuhusisha CCM, PAC na UKAWA

Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nyumba, ardhi na makazi Prof Tibaijuka, Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa serikali Jaji Werema, na Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Maswi

Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge

Azimio: Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic, Mkombozi na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji wa fedha haramu

Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa

HIVI NDIVYO PROFESA KIKWETE ALIVYOWASILI TANZANIA AKIWA NA AFYA NJEMA KABISA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mmoja wa abiria wakati ndege aliyopanda ilipotua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Rais Bw. Morris Mbena baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea
Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo 
Novemba 29, 2014

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wafanyakazi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuwasili akitokea Marekani kwenye matibabu leo Novemba 29, 2014

KINANA KWENYE UBORA WAKE,ZIARA ZAKE ZAWEKA HISTORIA KUBWA,TIZAMA ANACHOKIFANYA

Mnara wa Kumbukumbu ya Mwanajeshi wa Tanzania , Hamad Mzee aliyeuawa na ndege ya kivita ya wareno baada ya kuzitungua ndege mbili za kivita mwaka  1972 katika Kijiji cha Kitaya mpakani mwa Msumbiji na Tanzania wakati wa mapambano ya kuikomboa Msumbiji


 Kinana akipanda katika moja ya pikipiki 10 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwa makatibu Kata wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini katika mkutano wa hadhara wa katika Kata ya Kitaya

HII NDIO AJALI MBAYA YA NDEGE IL;IYOTOKEA DAR LEO PICHA ZOTE ZIKO HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAipIhlI8ex3lyJ-mPk1Kix3q57jRXW0raBvX4xz2sUm1erwxAOiUs0plcK-NjYz3Jn1N7BMGyoqvv_i9mOoUTv4t12pylH-Ayz17d68nKP4k_DsdYpr0puerX9W5qIKRmSHu_uYjK7-Y/s1600/1794591_10205373005827007_6204134194784841380_n.jpg
Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuangukaAjali
ya Helicopter ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani
3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse,
Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt.
Khalfan,Ajali  hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala
jijini Dar es
Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikaa mpaka sasa.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnkYKfN-ZYp79MR92smsNSn59V5bHfFhzupS5pWRO-gzDhTZqrqiaAhy4b3h3dEP7OCaY0UGnO8n6pyG9YMA3BAV9v6RxD3ylhfI8cyRSgf62Vo92qwno4SGgdjZTzaqjaeFUdZ4ahfSk/s1600/unnamed.jpg
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akifafanua
jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea
kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEftmSFx69EFX3tvHHZhczxVi21TklBFb9dKJmOPtkbeXwjLHjnf2wrxAjXXWeHbZxUtxtJVk0o5Ospeff46jH_w4S1s8ZApO3F4BnROGg7omLTozIZsmpm8Sizh01ToUOoCZaSvaQeEQ/s1600/unnamed.jpgj.jpg
 Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya
Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo
iliyopelekea vifo vya watu wanne
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYRroRI9l3fAd1f2kaXkNsaTooabukaZ_wvTRUS5XviTSYwshrBqsESGk8rQKQvcFXoox_sjR3YljDqux4FoUh-Uu2-zXGhBDHoYHMGvAm8VZ9Xznz3zP1KG0AwqUj3xAaOiSVgsu8U2o/s1600/unnamed.jpgm.jpg
 Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEir-eyPz4wy_hdR2eW2IYsqBHMyyopr9XH-jzsDPik_feVDl2m_m_9qROyFa3wHSJP3HVXkIONvXGhSxJMyUhfNsqagNsQ7wz0T20wImjXN6HhrYWGDGK_kFIT5OMF1Us109FUIyDlajBM/s1600/10802069_862315180487994_1289925175792270593_n.jpg
 Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es
Salaam.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGcsoRANe3su00TAseZh6Tn2Mpz65u7fVZm5IaubI92E4cW540Z3a-PjHWHtx7wpgeit1-8muCsOaKte707-EIdPe1FNVvmewsaEgEL8M2aCNTDkkqrfS1qVto7Qapyo1cq1S0CTgll4g/s1600/10360388_862315213821324_570599580791994756_n.jpg

TAZAMA MALUMBANO MAKALI YANAYOENDELEA KWENYE FACEBOOK BAADA YA ZITTO KABWE KUKUBALI MAPENDEKEZO YA CHENGE


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiP1k7NG9pjcAVLRiqhaL4UrH6EO39kD5wXZAFIpELs3o2tcwiyTfLn9aTw7ERo4BWWpCKH-MNviReke5mJ73wsPmb-578D9tWJWYNzKm0qHT2LcaF8erRfiGaqh4CShPBMtcAXhRQNcoA/s1600/Zitto+Kabwe.jpg Mhe  Zitto  Kabwe

ZITTO KABWE PAMOJA NA KUONESHA UNA UCHUNGU NA TAIFA NIMESHITUSHWA NA WEWE KUUNGA PENDEKEZO LA ANDREW CHENGE AMBAYE NI MTUHUMIWA.
Mara zote watu hudhani nina chuki binafsi na Zitto Kabwe ,Lahasha,Ninampenda sana Zitto Kabwe kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kijenga hoja Pamoja na kuwa na ushawishi mkubwa kwa umma.Lakini Pamoja na hilo,Zitto Kabwe ameliingiza taifa katika kunusuru mafisadi.
Kitendo cha Zitto Kabwe kuunga mkono hoja ya Andrew Chenge kwamba eti mamlaka zilizowateua Mafisadi kama Prof Muhongo,Pinda,Prof Tibaijuka na wenzake ndizo ziwawajibishe hivyo kukiuka kabisa mapendekezo ya PAC namba 8,9 10,11,12 ni kubariki mafisadi kujipa adhabu wenyewe.
Zitto katika pendekezo la Chenge ameunga mkono na kukubaliana huku akijua Chenge naye ni mtuhumiwa wa scandal hii ya uchotaji wa fedha katika account ya ESCROW kiasi cha Bilioni 1.6 sawa na milioni 1600 ni kulinda mafisadi.
Hivi mwizi anaweza kushauri ama kupendekeza adhabu ya kupewa??.Je ni kweli mtuhumiwa anaweza kushauri adhabu kali dhidi yake??
Ona sasa Wabunge wanasema Emmanuel Nchimbi,Hamis Kagasheki,Lowasa nk waombwe radhi kwa kuwa waliwajibishwa kwa kashfa mbalimbali iweje hawa walindwe??.Lowasa na wenzake waombwe radhi??
Zitto Kabwe Pamoja na kueleza kwa kina na kwa ufasaha mkubwa,Lakini kitendo cha kuunga mkono pendekezo la Chenge ni kutuachia maswali mengi sana yaliyokosa majibu.
Any way,ngoja tukubaliane na wengine pengine ni kutimiza PRINCIPLE OF NATURAL JUSTICE(NEMO JUDEX IN CAUSA SUA) yaani RIGHT OF RULE OF NO BIAS..

Thursday, November 27, 2014

UMESKIA JUU YA ZITTO KABWE KUSHIRIKI KULA HELA ZA ESCROW,SOMA JIBU LA WAKILI WAKE HAPA




Baada ya tuhuma zilizoibuka jioni hii juu ya hela za escrow kuwa hadi mwenyekiti wa PAC ZITTO KABWE KUSHIRIKI KULA HELA ZA ESCROW wakili wake ameibuka na kujibu yafuatayo.tuhuma hizi zimeibuliwa katika kipindi cha kuchangia ambapo mbunge lusinde amemtaja wakili wa zitto bwana msando kama mmoja wa watu waliomchukulia zitto kabwe million kumi za escrow,baada ya tuhuma hizo  wakili msando amesema haya

2 hrs · Msasani ·
1. Sijapokea hela yoyote kutoka kwa IPTL/PAP kumpa Mh. Zitto Kabwe. 2. Ni habari za kuzusha na kupotosha kusema Mh. Zitto alipokea hela. 3. IPTL/PAP wajitokeze na waseme hizo fedha kama walinipa walinipa ili Mh. Zitto afanye nini? Kwa nini walizitoa kama kweli walizitoa? 4. Kwa nini basi hawakuomba nihojiwe kuhusu hizo fedha?
Hoja inabaki; fedha ni za nani? Je tumeibiwa au hatujaibiwa?
LikeLike ·  · 

TIZAMA ALICHOKIFANYA SALUM MWALIMU WA CHADEMA KATIKA ILE OPERATION YAO


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu akisaini daftari la wageni kwenye ofisi ya chama hicho, Kijiji cha Laela, Jimbo la  Nkwera, mkoani Rukwa wakati alipowasilini kijijni hapo  kuanza ziara ya siku 5 katika vijiji mbalimbali vya mkoani Rukwa, ukiwa mwendelezo wa  ziara iliyopewa jina la Operesheni Delete CCM kuanzia uchaguzi ujao wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.



Naibu Katibu Mkuu akiwahutubia wananchi wa Laela

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar, Salum Mwalimu i akihutubia wananchi wa Kijiji cha Kaoze, kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika, mkoani Rukwa wakati alipowasilini kijijni hapo kuendelea na ziara ya siku 5 katika vijiji mbalimbali mkoani humo ukiwa ni mwendelezo wa  ziara iliyopewa jina la Operesheni Delete CCM




MBOWE ALIPOMTAKA PINDA AACHIE NGAZI LEO SIKILIZA NA SOMA ALICHOJIBIWA





Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.
Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?– Mbowe.
Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…

ESCROW BUNGENI--HUU NDIO UTETEZI WA WAZIRI MUHONGO.


Ameanza kwa kuomba radhi kama jana kulikuwa na usumbufu wa umeme na anawaagiza mameneja wote wa TANESCO wasikate umeme.

Anatoa pongezi juu ya mjadala wa Escrow, mengi yamesemwa na niwakati wa kuanza mjadala kujua ukweli, Shukraan kwa CAG, TAKUKURU kwa uchunguzi. Pia nawashukuru PAC, jana tulitulia kuwasikiliza PAC na leo tutulie tusikilize utetezi wangu

Miaka ya 90 tulikuwa tuna upungufu wa umeme kutokana na maji, 1994 serikali ilitoa kazi ya uwekezaji kwa IPTL ilikuwa inamiliwa na VIP ya Tanzania iliyokuwa na 30% na Mechmar ya Malaysia 70%.

Wednesday, November 26, 2014

MPYAAA---WATAMBUE KWA PICHA ZAO VIGOGO WALIOTAFUNA MABILION YA ESCROW

 Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe.
Andrew Chenge (Mb)






 Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4. 


 Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa                                         shilingi milioni 80.8. 

 Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4 
 Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4 

 Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga
alipewa shilingi milioni 40.4

 Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7. 

 kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa
shilingi milioni 40.4

 Viongozi wa Madhehebu ya
Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63
Methodius Kilaini shilingi 80.9 

 Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4 

 Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.
Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4. 
Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4

 Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi,
mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow

 Bilioni 73.5
zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha
Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006 
Taarifa
ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote
zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa. 

 Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
NA HAYA NDIO MAPENDEKEZO YA KAMATI

Tuesday, November 25, 2014

MPYAAA--SAKATA LA ESCROW LATINGA MAHAKAMA KUU KUZUILIWA UJADILIWA KESHO

Maafisa wanaojitambulisha kuwakilisha  Kampuni ya  Pan Africa Power-PAP wapo mahakama kuu ya Dar es salaam kufungua shauri la kuzuia suala la Escrow kujadiliwa na Bunge.
 
PAP wamefungua shauri hilo kwenye mahakama kuu kanda ya Dar es salaam  wakimshitaki waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG na katibu wa bunge kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa jambo lililokwisha kutolewa hukumu na mahakama na kukaguliwa na hivyo kutaka kuzuia mjadala wowote wa suala hilo hadi ufafanuzi wa mahakama utakapotolewa.
 

JESHI LA POLISI LATOA TAHADHALI KWA WANAWAKE KUTOSHIRIKI KIMAPENZI NA WATU WASIOWAJUA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM LATOA TAHADHALI KWA WANAWAKE KUTOSHIRIKI KIMAPENZI NA WATU WASIOWAJUA
         
       Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaa hususani wasichana kuwa makini na wanaume wanaowataka kimapenzi na baadaye kuwauwa na kutelekeza miili yao.

ESCROW--MAMA MARIA NYERERE AIBUKA MCHANA HUU,SOMA ALICHOWAAMBIA WANAHABARI NYUMBANI KWAKE

Mama  MARIA NYERERE ambaye ni mke wa baba wa taifa hili mwalimu NYERERE akizungumza na wanahabari muda huu nyumbani kwake jijini DAR ES SALAAM
Na karoli Vinsent

        SAKATA la Ufisadi wa zaidi ya Bilioni 400 kwenye Akaunti Tegeka Escrow iliyoko Benki kuu,lazidi kuwaibua watu mbalimbali Kupinga wizi huo ,baada ya leo Mama  Maria Nyerere kuibuka na kuzivaa mahakama pamoja na Bunge kwa kitendo chake cha kutumia kipengele cha sheria walizotunga wao kuwalinda wezi wanaliibia taifa mabilioni ya mapesa.

             Kauli hiyo ya mama Maria Nyerere ameitoa mda huu jijini Dar Es Salaam,wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini kutaka kufahamu kuhusu mwenendo wa nchi,ambapo Mama Nyerere alisema inashangaza sana viongozi wa leo ambao wanashindwa kumuenzi baba wa taifa kwa kuzidisha wizi wa mali za umma huku wakilindwa na sheria walizozitunga.
   
          “Yaani inasikitisha sana leo watu wanasogeza mali za umma kwenda kwenye mifuko yao huku tukishuhudia wengine hawana dawa kwenye hospitali,harafu tunaambiwa wezi hawa wanaofanya unyama huu wanalindwa na sheria,wakati leo unapita kwenye mitaa huku unamkuta mwizi ameiba kuku anachomwa moto,halafu anayeiba mali za umma analindwa na sheria sasa hii sheria ikoje jamani kwa sababu wtu wanakufa kwa kukosa dawa sheria haiwalindi hii ni vipi “ alihoji Mama Nyerere
    
             Mama Nyerere alizidi kuongea kwa uchungu huku akitaka hata kulia  alisema kwa sasa Viongozi wamekosa  maadili na kujikita kwenye wizi wa mali za umma kutokana na mifumo ya kimaadili ambayo imeanzia kwenye Familia na kupelekea hadi kwa watendaji wa serikali.
 Kuhusu Katiba iliyopendekezwa

TIGO PESA YAREJESHA TENA FAIDA YA SHILING BILION 3 KWA WATEJA WAKE

         Tigo imetangaza leo kwamba imetoa malipo yake ya kwanza ya kila robo mwaka ya kiasi cha shilingi bilioni 3 (dola milioni 1.8) kwa wateja wake wa Tigo Pesa. Mgao huu ni wa kwanza kati ya awamu nne za malipo zinazotarajiwa kufanyika kila mwaka.


      Malipo haya yanafanyka miezi mitatu baada ya kampuni hiyo kulipa kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (dola milioni 8.64) ambacho kilikuwa kimelimbikizwa katika mfuko wa fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, malipo yaliyoifanya Tigo kuwa kampuni ya simu ya kwanza duniani kuwagawia faida watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa simu za mkononi. Tigo Pesa ina jumla ya watumiaji milioni 3.6.

TANGAZO MAALUM TOKA TFF MCHANA HUU


WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA
Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wawww.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.

TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.

Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)