Sunday, January 31, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 1,2016.YAPO HAPA KWA UNDANI

Bomoa Bomoa ya TANROAD yaendelea kuwaliza wakazi wa Dar es salaam--Tizama hii

 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana.  na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.
 Wakazi wa Buza Sigara wakiondoa mabaki ya mbao baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad), kubomoa nyumba hizo.
 Kijana akipita jirani na nyumba iliyobomolewa.

Bomoa Bomoa KIWALANI DAR ES SALAAM yamkumba mtanzania huyu,aomba msaada kwa Rais Magufuli

 Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi  KIWALANI Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA SALUM MAWAMBA ameilalamikia TANROAD kubomoa moja ya GODAUNI lake la vifaa vya ujenzi   bila kufuata sheria hivyo kumsababishia hasara ya BILLION MOJA.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini DAR-ES-SALAAM,MAWAMBA amesema anasikitishwa  sana na kitendo hicho walichokifanya Tanroad kwa madai ya mmiliki huyo kujenga godauni hilo mpaka eneo la barabara,ambapo mmiliki huyo amekanusha kuwa sababu hizo sio za kwel,bali wamefanya hivyo kwa makusudi baada ya kukataa kuwapa rushwa


“maofisa hawa wa TANROAD wamekuwa wakinifwatilia mara kwa mara nakuhitaji rushwa lakini sikutishika na sikuwa tayari kwani navyojua eneo langu lipo mbali na barabara hivyo leo wamebomoa sehemu ya Godown langu na baadhi ya vifaa vyta ujenzi”.amesema mmiliki huyo.

Pia amesema kuwa maofisa hao wa TANROAD hawakupita katika ngazi zinazohusika ikiwemo kwa vongozi wa serikali za mtaa huo kwa mjumbe wala kwa diwani wa eneo hilo hivyo amemuomba Rais Magufuli kuweza kumsaidia kupata haki yake kwani anaamini Rais ni msikivu na mtetezi wa wanyonge.
Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi  KIWALANI Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA SALUM MAWAMBA akiwaonyesha wanahabari baadhi ya nyaraka zinazompa uhalali wa kuwa katika eneo hilo lililobomolewa na TANROAD 
Akizungumza Diwani wa kata ya Kiwalani MUSA KAFANA amesema kuwa kwa sasa anakusanya matatizo ya wananchi waliobomolewa kwa mmoja mmoja na ujumla kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria ili Kushughulikiwa kwa wakati huku diwani huyo akikiri kutofwatwa na maofisa kwa ajili ya zoezi la ubomoaji na kusema zoezi hili la ubomoaji ni Batili na uonevu kwa wananchi.

Aidha mmoja wa wananchi katika eneo hilo Mzee HERRY NDELELE amesema kuwa serikali siku zote inapokuja kubomo huwa inatoa taarifa kwa mmiliki wa jengo na uongozi wa mtaa hivyo anashangaa kuona zoezi hilo likifanyika bila utaratibu huo huku akisisitiza serikali kumsaidia mmiliki wa GODAUNI hilo na kumpa haki yake kwani sehemu aliyojenga ni halali na yupo nje ya barabara

“Mimi ni mtu wa zamani sana katika mtaa huu nachojua barabara hii imefuata wananchi na nashangaa kuona kitendo hiki cha kubomolea wananchi kiholela na buila kutowapa stahiki zinazofanana na aamani ya mali zao”amessisitiza

STORY PICHA NA IZACK MAGESA-DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA MASUALA YA USALAMA BARANI AFRIKA.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
(Picha na OMR)

MAJALIWA AHUDHURIA IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI MKUU WA KKKT TANZANIA ASKOFU SHOO MJINI MOSHI

4
Waziri MkuuKassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

Saturday, January 30, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARY 31,2016 YAPO HAPA


Picha --Majangili watungua Helkopta ya Doria serengeti na kuua rubani

 Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanayamapori.

Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.

Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa helkopita hiyo katika safari iliyokuwa na msukosuko mingi ya barabara na hasa kipindi hiki cha mvua na kuikuta helkopita iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.

Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo ambapo mkurugenzi mkuu shirika la hifadhi za taifa Tanzania Tanapa Allan Kijazi amesisistiza umuhimu wa wadau kuongeza nguvu katika kukabiliana na matatizo ya ujangili nchini.

Inauma sana--Mtu mmoja auwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka Geita


Zoezi la usafi wa mazingira katika kijiji cha Muungano nje kidogo ya mji wa chato mkoani Geita limeingiwa dosali baada ya tukio la mtu mmoja kuuwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka hali iliyosababisha mamia ya watu kufurika kushuhudia tukio la kusikitisha na kuacha kufanya usafi kwenye maeneo yao.


ITV imeshuhudia mamia ya watu wakiwa wamefurika katika mashine ya kusaga nafaka inayomilikiwa na Bi.Jamira Abdu Mkazi wa chato ambaye amemtaja marehemu kuwa anafahamika kwa jina la Juma Saidi alikuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka katika mashine hiyo zaidi ya miaka saba na kusema kwamba hivi karibuni marehemu alikuwa na ugomvi na mkewake ambapo alihama nyumbani kwake na kuanza kulala mashineni hapo.
 

Mabadilikoo--Tizama Mradi wa kwanza wa Meya mpya wa Kinondoni.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob akisikiliza maswali ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya mradi huo utakavyosaidia Manispaa ya Kinondoni ikiwemo suala hilo la usafi. Kushoto ni Florian Koelesch mshauri mtaalam wa mpango huo kutoka Ujerumani.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob (katikati) akizungumza katika mkutano maalum juu ya ushirikiano baina ya Manispaa hiyo ya Kinondoni na jiji la Hamburg la nchini Ujerumani watakavyojenga dampo la kisasa huko katika eneo la Mabwepande. Kushoto ni Florian Koelesch mshauri mtaalam wa mpango huo kutoka Ujerumani. Wengine ni watendaji wa Manispaa hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MNADHIMU MKUU WA JWTZ, BALOZI WA TANZANIA KUWAIT NA KATIBU TAWALA WA KATAVI NA MWANZA LEO IKULU DAR ES SALAAM

Q1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. 
Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha  Luteni Jenerali Venance Salvatory
 Mabeyo  kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve   kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza  Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016
Q8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses  Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es salaam leo January 30, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA AFRIKA ETHIOPIA LEO

sul1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Yuthra Bawaid alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bolo Nchini Ethiopia leo Januari 30, 2016 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa Wakuu wa Nchi za Afrika unaoanza leo mjini Addis Ababa Ethiopia
sul2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Gwaride la Heshima kutoka kwa Jeshi la Ethiopia alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa
sul3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwambata wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania Nchini Ethiopia Meja Generali John Bishoge alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia
sul4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 26 kwa wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Januari 30,2016 Mjini Addis Ababa Ethiopia.
sul5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifuatilia kwa Makini mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi za Afrika ulioanza leo Mjini Addis Ababa Ethiopia. (Picha na OMR)

TFF YAMPONGEZA SAMATTA


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amempongeza mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya Racing Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ubeligiji.

Malinzi amempongeza Samatta kwa kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Ubeligiji baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuichezea RC Genk inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo.
Kufuatia kupata nafasi hiyo, Malinzi amemtaka Samatta kujituma kwa nguvu zake zote na uwezo wake wote ili kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika nyanja za kimataifa na kwa sasa barani Ulaya.
Aidha Malinzi amewataka wachezaji wengine kujituma na kutumia nafasi wanazozipata katika vilabu vyao kwa kufanya vizuri na kupata nafasi ya kuvuka kwenda kucheza soka la kimataifa nchi za nje.

MAMA YASSODA AFUNGA KOZI YA MAKOCHA WANAWAKE




Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda leo amefunga kozi ya ukocha wa wanawake ngazi ya juu (High Level Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.

Akiongea wakati wa kufunga kozi hiyo, Mama Yassoda amesema anaishukuru TFF/FIFA kwa kuona wanawake wanapata nafasi ya kushiriki kozi mbalimbali, ikiwemo kozi hiyo ya ukocha kwa ngazi ya juu kwa wanawake.
Mama Yassoda amewataka washiriki wa kozi hiyo kuyafanyia kazi mafunzo waliyopatiwa katika kuhamasisha wanawake wengi kuupenda mpira wa miguu na kuzalisha vipaji vya wachezaji wengi wa kike kuanzia ngazi za chini, na sio kuhitimu na kuweka vyeti ndani tu.


Naye Mariam Mchaina akiongea kwa niaba ya washiriki wenzake, ameishukuru TFF kwa kuwakumbuka wanawake na kuwapatia kozi hiyo ya ukocha, na kuahidi watakaporudi sehemu wanazoishi watatumia ujuzi walioupata kufundisha wanawake mpira miguu kwa ngazi zote.
Kozi hiyo ya ukocha kwa wanawake, ilianza Jumatatu na kumalizika leo ambapo jumla ya washiriki 25 wameshiriki kozi hiyo ya awali kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, Iringa, Ruvuma, Pwani na Tanga na kupewa vyeti ya ushiriki na mpira kama kifaa cha kuanzia kazi ya ukocha.

Friday, January 29, 2016

BAWATA WAUNGA MKONO TAMKO LA SERIKALI

WMkurugenzi wa Baraza la Waganga Tanzania (BAWATA)David Wiketye akiongea na waandishi wa habari kuhusu waganga wanaokiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali juu ya utoaji huduma ya tiba asili nchini, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Shaka Mohamed Shaka.
Picha na Beatrice Lyimo

Baada ya SUMAYE kupona,Hili ndilo tukio la kwanza alilofanya leo na serikali

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.
 WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye (wa pili kulia), na mke wake mama Esther (kushoto), wakimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kulia) eneo la shamba lake la ekari 33 lililopo Mabwepande Manispaa ya Kinondoni lililovamiwa na wananchi walipotembea eneo hilo Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa Sumaye na viongozi wengine wakitafakari jambo.

LIGI KUU KUENDELEA JUMAMOSI


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Simba SC watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mchezo mmoja ambapo Maafande wa Mgambo Shooting watawakaribsiha Ndanda FC kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Sakata la Bunge kurushwa TBC LIVE lawaibua LHRC,watoa Tamko kali,Soma Hii

Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki zaBinadamu LHRC IMELDA LULU URIO akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam kuhusu sakata lililoibuka  bungeni la TBC kusitisha matangazo ya bunge kwa sababu ya Gharama 
 Na Exaud mtei( Msaka Habari)
Sakata la bunge la Tanzania kutokurushwa moja kwa moja na shirika la habari Tanzania TBC limechukua sura mpya baada ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kuibuka na kulaaani maamuzi hayo huku ikiyaita ni kuminywa kwa democrasia na uhuru wa habari nchini Tanzania na kuitaka serikali kuheshimu na kuzingatia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayojenga uhuru wa kujieleza kwa nchi wananchama.

Akizungumza na wanahabari mapema leo kaimu mkurugenzi wa kituo hicho IMELDA LULU URIO amesema kuwa kusitishwa kwa matangazo ya bunge na chombo ambacho ni cha umma ni kuonyesha dhahiri kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuheshimu yaki ya kupata habari ya kikatiba.

Amesema kuwa sababu zilizotolewa na waziri mwenye dhamana ya habari,utamaduni,sanaa na michezo Mh NAPE NAUYE kuwa kusitishwa kwa matangazo hayo kunalenga kupunguza gharama za uendeshaji ni sababu ambazo zinaleta maswali kuwa gharama hizi ni za nini?,na kwa ajili ya nini?na zikitumika ni kwa manufaa ya nani?,na mchangiaji wa gharama hizi ni nani?huku akisema kuwa TBC ni chombo cha Umma hivyo kunawajibika kwa wananchi wote bila kujali gharama.
Wakili Anna Henga kutoka katika kituo cha sheria na haki za binadamu akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ambapo amesema kuwa hakukuwa na sababu yoyote ya kufanya maamuzi hayo kwani kupata habari ni haki ya kila mtanzania 
Ameongeza kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimesaini makubaliano mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha upatikanaji wa taarifa  ikiwa ni pamoja na ule wa OPG –Open government partnership ambao ni jukwaa la serikali zenye uwazi mkataba ambao una misingi ya uwepo wa uwazi,ushiriki,wa wananchi,uwajibikajina uweledi na ubunifu wa kutumia Tehama.
Waandishi wa Habari wakipata Habari
Amesema kuwa LHRC inaitaka serikali kutekeleza kwa vitendo maazimio ya makubaliano ya kimataifa na kikanda katika kulinda haki ya kupata habari na kufuta sheria kandamizi zenye kuminya uhuru huu kwa mfano sheria ya magazeti na sheria ya makosa ya mitandao na kutunga sheria wezeshi.


Pia LHRC wameitaka serikali kuacha kuminya haki za watanzania ya kupata habari za bunge kwa kisingizio cha gharama,na kutenga rasilimalin nyingi kuwezesha shirika hilo waweze kuonyesha moja kwa moja matangazo ya bunge.
Tangazo la kutokuonyeshwa kwa bunge kupitia TBC lilitolewa bungeni na waziri wa Habari NAPE NAUYE na baadae jana waziri mkuu Mh KHASIM MAJALIWA alitoa msisitizo kuwa wameamua kusitisha matangazo hayo kutokana na kupunguza gharama za uendeshaji

Thursday, January 28, 2016

BABU DUNI YUPO,AREJEA CUF RASMI,USHAHIDI WA PICHA UPO HAPA

Aliyekuwa mgombea mwenza wa Urais Wa ukawa kupitia chama cha Democrasia na maendeleo Chadema JUMA HAJI DUNI maarufu kama Babu duni sasa ameanza kurejea kwenye chama chake cha zamani cha Cuf baada ya uchaguzi kumalizika mwaka jana.

Juma Duni alilazimika kuchukua kadi ya chadema ghafla ili aweze kuungana na mgombea wa Chadema EDWARD LOWASA katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka jana ambao John Pombe Magufuli aliiibuka kidedea.

Baada ya uchaguzi huo kumalizika kumekuwa na mijadala mingi ikijadili Je mgombea mweza Babu DUNI atarejea kwenye chama chake cha CUF ambapo alikuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho au ataendelea kuwa ndani ya CHADEMA.

Katika mkutano mkuu wa baraza la CUF lililokuwa linajadili hatma ya uchaguzi wa marudo zanzibar hapo jana mtandao huu ulifanikiwa kushughudia Babu duni akishiriki katika vikao hivyo kama picha zilivyonaswa hapo jambo ambalo linaloonyesha wazi kuwa DUNI amerejea ndani ya CUF.

Wanachama wa CUF waliopata nafasi ya kuzngumza na mtandao huu wameeleza kuwa DUNI hakuondoka CUF bali kilichotokea ni kupewa kadi ya chadema ili aweze kukidhi masharti ya kugombea nafasi ya Mgombea mweza na sasa amerejea ndani ya chama chake kama kawaida,
CHINI KUNA PICHA KADHAA DUNI AKIWA MAKAO MAKUU YA CUF JANA

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARY 29,2016