Sunday, July 31, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NDANI NA NJE YA TANZANIA YAPO HAPA

Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake.
“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.
“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.
Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.
Rais Magufuli aliwataka wananchi kutokubali kudanganyika na kufanya maandamano na badala yake wajikite katika kufanya kazi itakayowaletea maendeleo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kile walichokiita ‘Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)’, akiwaalika wafuasi wake kufanya maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

WAZIRI NAPE,LOWASA,MBOWE WAWAONGOZA WANAHABARI KUMUAGA MWANDISHI SENGA

S1Wapiga picha wakibeba jeneza la marehemu Joseph Senga aliyekuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima ili  kuliweka kwenye tayari kwa safari ya kwenda Wilayani Kwimba  Mkoani Mwanza kwa mazishi wanaoongoza mbele katikati ni Rafiki yake Mkubwa Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania aliyeshika Msalaba , kulia aliyeshika Shada la maua ni John Bukuku mpigapicha na  Mkurugenzi wa Blog ya Fullshangwe  na  kushoto aliyeshika picha ya marehemu  ni Joachim Mushi mpiga picha na Mkurugenzi wa Mtandao wa The Habari akiwa pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger Tanzania TBN wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Sinza jijini Dar es salaam.
S2Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania kulia Mpiga Picha Loveness aliyekuwa mfanyakazi mwenzake na marehemu kwenye kampuni ya Free Media inayoendesha gazeti la Tanzania Daima na Mpiga Picha Halima Kambi kutoka Guardian  wakiwa wamebeba mashada ya maua na msalama.
S3S4Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga na kushoto ni Mpiga Picha mkongwe Juma Dihule.
S5
Carthubert Kajuna Mpiga Picha na Mkurugenzi wa Blogu ya Habari na Matukio akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga.
S6
Mpiga Picha wa Gazeti la Habari leo Robert Okanda akiaga mwili wa marememu.
S7
Mpiga picha Muhidin Sufiani akitoa hesgima zake za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S8
Baadhi ya wapiga picha wakijadiliana mambo kadhaa.
S9S10
Mpiga Picha wa Jambo Leo Dotto Mwaibale akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S11
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa akiongozana na Nape Nnauye Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S12
Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowasa akijadiliana jambo na Nape Nnauye Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo wakati walipoongoza waombolezaji katika kuaga mwili  wa mwanahabari Marehemu Joseph Senga
S13

MBOWE ALIVYOJISALIMISHA POLISI LEO

index
Mwenyekiti wa Chama Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongozana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu, Edward Lowassa, John  Mnyika, Mkiti wa Baraza la Wazee Hashimu Issa Juma na  Mwanasheria Mkuu wa Chama Tundu Lissu, wakiwasili  Kituo Kikuu cha Polisi (Central) Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambapo Mwenyekiti Mbowe ameitikia wito wa jeshi hilo kupitia wa ZCO Wambura wa kumhitaji afike hapo leo.
12472494_1656089934709103_3034388568427549281_n
13907088_1656090014709095_2493182602921163246_n

JAMES LEMBELI NJIA NYEUPEE KURUDI CCM,MAGUFULI AMKARIBISHA

indexMhe Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa CCM  na Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli akiwa meshikana mikono na Mhe Lembeli  huku akiongozana naye , Lembeli Amesema yuko tayari kurudi CCM wakati wowote   akihitajika kurudi ili kumasidia Rais “Nilitoka CCM kwa sababu Ruswa ilitamalaki” Lembeli amezungumza hayo  mchana wa leo katika mkutano mkubwa wa  hadhara huko mjini Kahama.
Rais Dk. John Pombe Magufuli akizungumza katika mkutano huo  amemwambia Lembeli “Rudi kundini kadiri utakavyoguswa ili tuijenge nchi kwa sababu huko uliko huwezi kujenga nchi.

RAIS WA SIMBA, AVEVA AKITANGAZA MKUTANO KURIDHIA KUFANYA MABADILIKO

Hilo limethibitishwa na Rais wa Simba, Evans Aveva katika mkutano mkuu wa Simba ambao ulikuwa unafunga msimu wa 2015/2016 kwa kutolewa taarifa na kuweka mipango mipya kwa msimu ujao.
Hatua hiyo imekuja baada ya mmoja wa mashabiki wa Simba na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa makampuni ya Mohammed Enterprises, Mohammed Dewji “MO” kutangaza nia ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 na kutoa Bilioni 20 kwa ajili ya kuisaidia Simba kurudi katika makali yake ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, kocha mzuri, kujenga kiwanja, kuweka vituo vya kukuzia vipaji vya Simba na vingine vingi.
Kutokana na jambo hilo, mashabiki wa Simba walionekana kuvutiwa na mipango ya MO na hivyo kuandamana katika ofisi za klabu na kushinikiza uongozi kukubaliana na MO ili kununua hisa na kuanza kuwekeza ili Simba irudi katika makali ya kushinda mataji.
Ipo hapa video ikimuonyesha Rais wa Simba, Evans Aveva akitangaza mkutano wa Simba kuridhia kufanya mabadiliko.

Saturday, July 30, 2016

Mahafali ya KKKT Chuo Kikuu Muhimbili Yapigwa Marufuku Baada ya Wanafunzi Hao Kumwalika Lowassa Kuwa Mgeni Rasmi

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) umezuia mahafali ya wanafunzi  waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA LEO JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India.

MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said)

MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS


Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.

Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba SC, Young Africans SC, Azam FC na Mtibwa Sugar FC.

SKY SPORTS YAUNGANA NA STARTIMES KUONYESHA LIGI YA CHINA



Na Dotto Mwaibale

Kituo cha matangazo ya luninga cha Sky Sports cha nchini Uingereza katikati ya wiki hii kilisaini mkataba mnono wa kuonyesha moja kwa moja ligi kuu ya China kwa misimu mitatu ijayo ambayo pia kwa Tanzania inaonekana kupitia visimbuzi vya StarTimes.

Sky Sports wameamua kuanza kuionyesha ligi hiyo baada ya kuvutiwa na jitihada kubwa zinazofanywa na China katika kukuza soka la nchini mwao hususani kupambana sambamba na vilabu vikubwa vya barani Ulaya katika kusajili wachezaji nyota kutokea ligi hiyo.

Ligi hiyo imeanza kujizolea umaarufu na kuvuta hisia za watu baada ya kuona majina ya wachezaji wakubwa yakielekea huko kama vile Ramires aliyetokea Chelsea, Gervinho aliyewahi kuchezea Arsenal, Obafemi Martins aliyechezea Newcastle United na hivi karibuni nyota wa Italia Graziano Pelle aliyetokea Southampton na kujiunga na Shandong Luneng.

Akizungumzia juu ya taarifa hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania,  Lanfang Liao ameelezea kuwa hiyo ni habari njema kwetu sisi pia kwani mapema mwaka huu tuliingia makubaliano ya kuitangaza ligi hiyo pia baada ya kuona mbali kuwa itakuja kuwa maarufu na hilo linaanza kujidhihirisha.

“Ukiwa unazungumzia ligi ambazo zinakua kwa kasi duniani kwa sasa hutoacha kuizungumzia ligi kuu ya nchini China au maarufu kama ‘Chinese Super Cup’. Na hii ni kutokana na ushindani uliopo hivi sasa unaopelekwa na wachezaji pamoja na makocha wazuri katika soka ukiachilia mbali malipo makubwa wanayoyapokea ambayo yanakwenda sambasamba na vilabu vikubwa vya barani Ulaya. Mashabiki wa soka hivi sasa wanaweza kutazama mechi za ligi hiyo na kuziona sura ambazo awali walikwishaziona barani Ulaya kama vile Graziano Pelle, Ramires, Gervinho, Hulk, Asamoah Gyan, Jackson Martinez, Ezequiel Lavezzi na wengineo wengi.” Alifafanua  Liao

“StarTimes kadiri siku zinavyokwenda mbele ndivyo tunazidi kuboresha zaidi huduma zetu hususani ligi mbalimbali za soka kwani tunatambua watanzania ni wapenzi wakubwa. Na kwa kuwa na wigo mpana wa mashindano mbalimbali kunawafanya waweze kufurahia zaidi huduma zetu. Ligi ya China kwa sasa ni ligi kubwa duniani na ndiyo maana Sky Sports wameamua kuinonesha barani Ulaya huku kwa sisi Tanzania na Afrika kwa ujumla ni kupitia visimbuzi vyetu pekee unaweza kutazama mechi zote moja kwa moja.” Alihitisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ya matangazo ya dijitali nchini

Baada ya kusaini makubaliano hayo kwa mara ya kwanza kabisa Sky Sports wataingia mzigoni kuanza kuonyesha mechi za ligi hiyo siku ya Jumamosi ya Julai 30, 2016 ambapo timu za Shanghai Greenland Shenhua itakuwa kiburuani kuwakabili Jiangsu Suning FC (saa 8:35 mchana) na siku ya Jumapili, Julai 31 timu ya Guangzhou R&F inayonolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, Sven Goran Eriksson kumenyana na Shanghai SIPG (saa 8:35 mchana).

Mechi hizo zote kwa hapa nchini Tanzania zitaonekana moja kwa moja kwenye visimbuzi vya StarTimes kupitia chaneli za Sports Focus na World Football.

SIA PIUS NDIYE WINDHOEK DRAUGHT MISS SINZA 2016

 Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd akisema chochote kwenye shindano hilo.
 Mtoa huduma wa kampuni hiyo akitoa huduma kwa wadau wa windhoek.
 Wadau wa Windhoek ndani ya Defrance Hotel katika shindano hilo.
 Hapa ni windhoek tu kwa kwenda mbele.
 Wadau wa windhoek wakiwa kwenye shindano hilo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Jerome Rugemalira (kushoto), akigongesha chupa ya windhoek na mdau wa kinywaji hicho, iliyokatika muonekano mpya katika shindano hilo.
 Wacheza shoo wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia wakishambulia jukwaa katika shindano hilo.
 Wasanii wa kampuni ya mabibo wakionesha umahiri wa kucheza wakati wa shindano hilo.
 Washiriki wa shindano hilo wakijitambulisha kwa kucheza kabla ya kuanza kwa shindano hilo.
 Wanenguaji wa Bendi ya FM Academia wakiwa kazini.

 Washiriki wakiwa katika vazi la ubunifu.
 Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.
 Baadhi ya washiriki ambao hawakufanikiwa kuingia tano bora.
 Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.
 "Jamani tuchangechange mapene tuongeze windhoek meza imekauka hapa"
 Hapa ni furaha tu kwa kusonga mbele.
 Majaji wakiwa tayari kuwatangaza washindi.
 Mdau wa Windhoek na mashindano ya Miss Tanzania, Rutha Lucas akitoa sh.100,000 kwa kila mshiriki wa shindano hilo ikiwa ni kifuta jasho.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto),  akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Friday, July 29, 2016

BREAKING NEWZZ---ZITTO KABWE ATOA MAELEKEZO MAZITO KWA WANACHAMA WA ACT NA WATANZANIA KWA UJUMLA



Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC ) kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo ( KC/01/2016 ).
Mamlaka
Katiba ya ACT Wazalendo toleo la mwaka 2015 Ibara ya 29 inatoa mamlaka kwa Kiongozi wa Chama kutoa maelekezo kwa Viongozi na Wanachama wa Chama kila inapobidi. Maelekezo yafuatayo ( KC/01/2016 ) nayatoa kwa kila mwanachama kufuatia Hali ya Siasa inayoendelea nchini. Maelekezo haya yabandikwe kwenye kila Ofisi ya Chama kuanzia Taifa mpaka Tawi na yasomwe kwenye Mikutano Mikuu ya Chama ya Matawi yote nchini ndani ya Mwezi huu wa Agosti, 2016. Maelekezo haya pia yatumwe kwenye kila ' Whatsapp Group ' la Chama na Ngome zote za Chama.

Maelezo
Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020. 

CHADEMA NYANDA ZA JUU KUSINI NA NYASA WASEMA WAPO TAYARI KWA OPARESHENI UKUTA


      Bw  Frank  Mwaisumbe
CHAMA   cha  Demokrasia  na maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) wameunga  mkono maazimio yote yaliyotolewa na kamati  kuu  cha Chadema  chini ya mwenyekiti wake   Taifa   Bw  Freeman  Mbowe  ya  kuazisha  oparesheni UKUTA .
 
Taarifa   iliyotolewa kwa  vyombo  vya habari  leo   na mwenyekiti wa  kanda   ya nyanda
za  juu  kusini Bw  Frank  Mwaisumbe alisema  wamepokea  kwa mikono  miwili maamizimio  hayo  ya  kuanzisha  oparesheni UKUTA  nchini  nzima  na  kuwa wapo  tayari  kwa  kushiriki .
 
“Kwa ujumla wake (Mkoa wa Mbeya, Songwe, Rukwa, Iringa na Njombe) inaunga mkono maazimio ya Kamati kuu ya Chama Chetu iliyoketi tarehe 27/07/2016 ya kupinga vikali aina zote za udikteta zinazoendelea na kufanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM)….. na kuwa tupo tayari kuona Demokrasia
ya  vyama vingi  nchini Tanzania inaendelea  kuimarika kama iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius kamabarage Nyerere, ambayo aliiacha ikiwa na amani na utulivu na kuwa nchi yenye kuruhusu mfumo wa vyama vingi”