Wednesday, December 10, 2014

TIGO YATOA DOLA 40,000 KWA MIRADI YA WAJASIRILIAMALI JAMII

unnamedMkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Severin Philemon wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed1Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez akimkabidhi cheti cha ushiriki kwenye shindano la Tigo Digital Changemakers kwa Mohamed Juma wakati wa kutangaza washindi wa shindano hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
unnamed2Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mmoja wa washindi wawili wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana, mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi wa dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leokwa mradi wake wa kijitali eAfya.
unnamed3Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez (kushoto) akiwa na mshindi mmoja wa shindano la Tigo Digital Changemakers Innocent James Sulle mara baada ya kumkabidhi zawadi ya mfano wa hundi dola 20,000 za Kimarekani ikiwemo cheti cha ushiriki kutoka Tigo na Reach for Change mapema leo kwa mradi wake wa kijitali Travelling Library.
unnamed6 Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez (kushoto) na Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa Reach For Change Bi.Amma Lartey(kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la Tigo Digital Changemakers, Leka Tingitana na Innocent James Sulle baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano hilo lenye kutumia nyenzo za kidijitali kwa ajili yakuwasaidia watoto nchini.
……………………………………………………………………………..

RAIS WA ZANZIBAR DR. ALI MOHAMMED SHEIN MGENI RASMI TUZO ZA TASWA

2
Makamu mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw. Egbert Mkoko kushoto   na Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando wakionyesha tuzo zitakazotolewa kwa wanamichezo bora wa mwaka wa TASWA  katika hafla itakayofanyika ijumaa kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh Dr. Ali Mohammed Shein. Mkutano wa uongozi wa TASWA na  waandishi wa habari umefanyika kwenye mgahawa wa City Sports Lounge jijini Dar es salaamMakamu mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari za Michezo TASWA Bw.
1 Egbert Mkoko  katikati akielezea mambo mbalimbali yatakayojiri katika tuzo hizo wakati akiongea na waandishi wa habari leo kushoto ni Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando na kushoto ni Mjumbe wa TASWA Mwani Nyangasa.


LHRC WAADHIMISHA MIAKA 66 YA TAMKO LA HAKI ZA BINADAMU ULIMWENGUNI,TUKIO LIKO HAPA


Baadhi ya wanafunzi waliojitokeza katika maadhimisho hayo leo jijini Dar es salaam
 Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kwa kushirikiana na wadau wengine wa haki za binadamu leo wameadhimisha miaka 66 tangu kuanzishwa kwa tamko la haki za binadamu la ulimwengu  ambalo lilitoka tarehe 10,mwezi wa 12 mwaka 1948,tamko ambalo ndio hasa chimbuko la misingi ya haki za binadamu kote duniani.
Tamko hilo ambalo linaainisha haki za kiuchumi,utamaduni,kiraia n kijamii lilifwatiwa na mikataba miwili ambayo ni mkataba wa kimataifa wa haki za kiraia,pamoja na mkataba wa kimataifa wa haki za kiuchumi,kijamii,na utamaduni 1966.
 Akizungumza katika maadhimishohayo ambayo awali yalitanguliwa na maandamano ya wadau wa haki za binadamu kaimu mkurugenzi wa LHRC Ezekieli Masanja amesema kuwa ipo haja ya serikali kuanza kuweka masimo ya haki za binadamu katika mitaala ya shule za msingi ili kuanza kuwajengea wanafunzi uelewa mapema wa haki za binadamu na jinsi ya kuzilinda,ikiwa ni pamoja na kukuza uelewa wa vijana wa shule juu ya haki za binadamu.


Kwaya mbalimbali zikitoa burudani
 Amesema kuwa pamoja na mambo yote  kufanyika lakini  bado kna haja kubwa ya kuanza kujenge uelewa wa vijanawadogo juu ya haki za binadamu wakiwa shuleni.
Aidha LHRC wametoa tathimini yao ya haki za binadamu kwa Tanzania ambpo bado inaonyesha zipo changamoto kubwa za ulindaji wa haki hizo mfano maeneo kama kiwango cha elimu bado kipo chini kwa watanzania,migogoro hasa ya ardhi bado imeendelea kuwa tatizo kwa watanzania,pamoja na ajali za barabarani na mauaji mbalmbali yameendlea kuwa changamoto kubwa kwa watanzania.

Tuesday, December 9, 2014

PICHA MBILI ZA SIKU,WAZIRI NYALANDU

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akitoka nje ya nyumba ya kimasai alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika eneo la Loliondo.

KAMA HUKUFIKA TAIFA LEO MIAKA 53 YA UHURU PICHA ZOTE ZIKO HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange.
Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Sunday, December 7, 2014

TIZAMA JINSI COMRADE MWIGULU NCHEMBA ALIVYOUTEKA MJI WA GEITA

Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini.
Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba yakiendelea kwa shamrashamra za kutosha.
Hisia za Wananchi kwa Mwigulu Nchemba ambaye katika Bango moja wapo anasomeka kama SOKOINE WA PILI NCHINI TANZANIA.

TIZAMA JINSI MBOWE ALIVYOWANADI WAGOMBEA WA SERIKALI ZA MITAA KUPITIA UKAWA KATIKA KATA YA VIJIBWENI

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe  akihutubia katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika katika viwanja Kata ya Vijibweni Kigamboni jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)


PICHA HII YA RAIS KIKWETE ILIYOTIZAMWA SANA WIKIEND HII ICHEKI HAPA


Hapa   Rais  Kikwete  akifanya  mazoezi    hivi  karibuni  HUKO ikulu   kutokana  na kufanyiwa  operesheni  ya  tezi  dume   ambapo  walimshauri  awe  ana fanya  mazoezi!!!!   Inawezekana  rais  anataka  afya  yake  ikae  sawa   KWANZA  ili  aweze  kufanya  MAAMUZI   yake vizuri    hasa  ile  issue     inayosubiliwa  kwa  hamu   na  watu  wengi  kuhusiana  na  maazimio  ya  bunge  maana  watu   wengi  wamekuwa  wanasema kuwa  Rais  yupo  kimya  sana  kuhusiana  na  kashfa   ya  ESCROW !!!!



Saturday, December 6, 2014

SHULE YA AWALI YA ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL SASA KUANZA KUTOA ELIMU YA MSINGI MWAKANI,MAHAFALI YAO YAFANA

Wanafunzi ambao ndio wamehitimu shule ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo shule ambayo ipo bunju jijini Dar es salaam hapa wakikata keki pamoja na mwalimu wao ishara ya kufurahia mafanikio waliyoyapata pamoja na mafanikio ya shule hiyo tanghu kuanmzishwa kwake
Wahitimu wakiwa katika pozi za kusubiri sherehe ya kuwaaga rasmi kutoka elimu ya awali kuingia elimu ya msingi
Mgeni rasmi wa mahafali hayo mama NEEMA KIBANGA ambaye ni afisa elimu wa kata ya bunju akikabidhi vyeti kwa wahitimu shuleni hapo

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kukabidhiwa vyeti vyao

  Na Exaud Mtei
           Shule ya wanafunzi wa awali ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo imefanya mahafali ya wanafunzi wa awali wanaovuka kuingia elimu ya msingi huku ikiwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake shule hiyo mnamo mwaka 2012.
             Shule hiyo ambayo inapatikana BUNJU jijini Dare s salaam ambayo ilianza mwaka 2012 ikiwa na jumla ya watoto tisa tu na mwalimu mmoja ambapo mwaka 2013 idadi iliongezeka na kufikia watoto 13 na hatimaye mwaka huu wa 2014 shule hiyo ina watoto 31 pamoja na walimu wawili jambo ambalo limetajwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa shule ya watoto iliyoanzishwa na watanzania wazalendo kwa ajili ya kuinua elimu ya watoto wa Tanzania.
Akizungumza katika mahafali ya shule hiyo leo meneja wa shule hiyo Bwana STANSLAUS ABED MWALONGO amesema kuwa lengo lilikuwa ni kuanzisha shule ya secondary lakini baada ya kutafakari jkwa kina akaona ni vyema kuanzisha shule ya awali na msingi ili kutoa msingi bora wa elimu kwa watoto wetu.
Bwana STANSLAUS ambaye baba yake ndiye aliyekuja na wazo za kuanzisha shule hiyo na kufanya shule hiyo kuitwa jina lake amesema kuwa moja ya mafanikio makubwa ya shule hiyo ni kuongezeka kwa watoto wanaoenda kujiunga na shule hiyo ambapo mpaka sasa watoto sita wamehitimu shuleni hapo na sasa wanaendelea na masomo ya shule ya msingi katika shule mbalimbali zenye ushindani nchini Tanzania.
Katika hali ya kutia moyo meneja wa shule hiyo amesema kuwa shule yake imekamilisha taratibu zote za usajili na kuwa mwakani 2015 shule hiyo itaanza kutoa elimu ya msingi kwa mara ya kwanza ambapo amesema kuwa wanatarajia kuanza kutoa elimu ya darasa la kwanza kwa masomo yote huku akibainisha kuwa lengo la shule hiyo ni kutoa elimu bora inayoendana na maadili ya kitanzania ili kuwasaidia watoto waweze kuwa kizazi bora hapo baadae.


Kwa upande wake mgeni rasmi wa mahafali hayo ambaye ni afisa elimu kata ya BUNJU mama NEEMA KIBANGA amesema kuwa ni mafanikio ya kupongezwa kwa wamiliki wa shule hiyo kwani wamefanya jambo ambalo linatakiwa kuigwa na kila mtanzania ambaye anapenda maendeleo ya watoto bila kujali rangi,dini,wala kabila analotoka huku akikumbuka kuwa watoto bni wetu sote.
Mmoja wa wamiliki wa shule hiyo ambaye ni mke wa meneja wa shule hiyo BI ROSE MWALONGO akizungumzas na watoto wa shule hiyo mapema kabla ya kuanza shughuli rasmi ya mahafali ya shule hiyo
Maadili ya kidini ni moja ya nguzo kuu za shule hiyo bila kuchagua imani ya mtu mtumishi wa mungu akitoa neni la mungu kwa wazazi na watoto waliohudhuria sherehe hiyo iliyyofanyika shuleni hapo BUNJU jijini Dar es salaam
Picha mbili zikiwaonyesha wazazi waliofika kujumuikana watoto wao katika kuhitimu elimu yao ya awali
Baadhi ya wazazi waliobahatika kuzungumza na mtandao huu wamesema kuwa wameridhika kabisa na utoaji wa elimu shuleni hapo kwani unazingatia vigezo na maadili yote hivyo hawana hofu juu ya watoto wao huku wakiwahimiza wazazi walio na watoto wadogo kuwaleta ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL kwa ajili ya mafunzo bora kwa watoto wao.
Katika mahafali ya leo wanafunzi takribani 6 wamehitimu shuleni hapo katika masomo yao ya awali na wataanza elimu ya msingi shuleni hapo mwakani

Watumishi wa bwana walitumia muda wao kubariki eneo la shule hiyo kwa maji ya baraka ili watoto wanaosoma hapo kuwa na baraka za mungu muda wote


CHUO KIKUU HURIA CHAFANYA KWELI KUHUSU UGONJWA WA UKIMWI-SOMA HAPA KUJUA

Kulia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi  Chuo Kikuu Huria upande wa Kinondoni Mussa h Omari kushoto ni Rais Mwezake  wa Chuo hicho upande wa Temeke Mganwa Nzota wakitoa Elimu kuhusu Maambukizo Mapya ya Ukimwi Leo Jijini Dar Es Salaam
Wanafunzi wa Chuo chuo Kikuu Huria cha Tanzania Kampus ya temeke wakisikiliza Jambo kwenye Semina hiyo
Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Kampus ya Temeke David Malangalila akiwaelekeza Jambo viongozi wenzake katika Semina hiyo
Viongozi wa juu wa Serikali ya Wanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Huria wakimasikiliza Mtoa Mada Mussa h Omari

KHERI YA KUZALIWA KWA MWANA LIBENEKE GEOFREY WA PAMOJA BLOG

Kwanza kabisa natoa shukrani kwa mwenyezi mungu kwa kunifikisha leo tarehe 06 mwezi wa 12 maana ndio kumbukumbu yangu ya kuingia duniani.
 Namshukuru mama yangu mzazi aliyanizaa na kunilea mpaka hapa nilipo ni kwa uwezo wake nampenda sana mama yangu.
Nawashuku sana ndugu zangu wote kwa support wanazonipa ili nifikie malengo niliyojiweke na Pia sina budi kuwashukuru Mablogger wanaonipa support ya nguvu maana bila ninyi mablogger sidhani kama kazi hii ingeendelea mpaka kufikia hapa na pia kuna baadhi yao unielekeza kwa kunikosoa hata kunifundisha ni kipi cha kufanya il niweze kufikia malengNa pia washukuru wadau wetu wanaotembelea Blog Yetu http://pamojapure.blogspot.com/
maana bila nyie mimi nisingekuwa nafanya kazi hizi. Asanteni sana na pia nawapenda sana munguawalinde na awasimamie katika ujenzi wa taifa letu

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DISEMBA 17-21, 2014 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.Aidha alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa
 Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi  21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.Akizungumza  jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik  Mollel, alisema  lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)Kauli mbiu ya maonesho hayo KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA