Friday, September 2, 2016

TANZANIA na URUSI zabadilishana Uzoefu wa Kudhibiti Uhalifu

Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao  hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.

Rais Dkt MAGUFULI azungumza na Wananchi Kisiwani PEMBA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuhutubia mkutano wa katika uwanja wa Gombani ya kale Chake chake kisiwani Pemba.

KLABU ZATAKIWA KUJISAJILI GPX KABLA YA JUMATATU


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine, limeagiza klabu tisa za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Klabu sita za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (TFDL) kujiunga mara moja na mfumo huo unaoitwa GPX yaani Global Players Exchange ambao malengo yake ni kurahisisha kufanya usajili kwa mchezaji.

LIGI KUU YA VODACOM, MECHI NNE KESHO

Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 3, 2016 kwa michezo minne wakati kwa Jumapili Septemba 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TBLB).
Michezo ya kesho ni kati ya Mbao FC na Mbeya City utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Kagera Sugar itazindua uwanja wa nyumbani kwa kucheza na Mwadui ya Shinyanga.

TAIFA STARS KAZINI KESHO JUMAMOSI


Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho Septemba 3, 2016 inatarajiwa kuingia kibaruani kwa kucheza na Super Eagles ya Nigeria katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Mchezo huo utafanyika kuanzia saa 11.00 (17h00) jioni kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabo, mjini Uyo katika Jimbo la Akwa Ibom. Muda huo uko mbele kwa saa mbili kamili kwa maana hiyo Taifa Stars itacheza dhidi ya Nigeria saa 9.00 alasiri (15h00).

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akabidhi daipa elfu 85,000 kutoka Taasisi ya GSM Foundation katika Hospitali ya Amana

Moja ya Ahadi za Rais Magufuli alipokuwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kampeni ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya, na jambo hilo limekuwa likifanywa na watendaji mbalimbali alio wateua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
DC MJEMA GSM (3)

Ambapo siku ya leo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amekabidhi daipa elfu 85,000 kutoka Taasisi ya GSM Foundation katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa Daipa hizo zitagawiwa katika vituo vya afya 26 vya wilaya yake ambapo wazazi wenye watoto wanaohudhuria kliniki na wale watakaojifungua hivi karibuni watakabidhiwa.
DC MJEMA AMANA GSM (1)

Aidha Mkuu wa wilaya huyo ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha Huduma za Afya, na kupongeza jitihada zinazofanywa na GSM Foundation huku akiwataka wadau wengine waige mfano huo, na kuwaomba GSM Foundation waendelee kuwasaidia kwani yapo masuala mbalimbali ya kiafya yanayohitaji msaada wao.
DC MJEMA GSM (1)

Thursday, September 1, 2016

SAKATA LA MBOWE KUDAIWA NA NHC,HII STORY INAFAFANUA


SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeeleza kuwa, hatua ya kufungia Kampuni ya Hotels Limited (MHL) ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa si ya kisiasa, anaandika Pendo Omary.

Leo NHC kupitia wakala wake Fosters Auctioneers (Sio Action Mark) wamevamia jengo lililopo kampuni hiyo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam na kuchukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji gazeti.

Hatua hiyo inatokana na madai kwamba, NHC inadai kampuni hiyo jumla ya Sh. 1.3 Bilion na kwamba, bado hazijalipwa mpaka sasa licha ya kutoa muda stahili wa kulipwa deni hilo.

Ndani ya Hampuni ya MHL kuna Kampuni ya Free Media inayozalisha Gazeti la Tanzania Daima la kila siku.

Japhet Mwasenga, Meneja wa Kitengo cha Ukusanyaji Madeni katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) amesema, kuondolewa kwa kampuni ya Mbowe katika jengo hilo hakuhusiani na masuala ya kisiasa.

Mwasenga amewaambia waandishi wa habari leo mapema asubuhi wakati NHC ikisimamia shughuli ya uondoshaji vifaa kwenye jengo hilo kuwa “hiki kinachofanyia sio siasa. Hili sio suala la Mbowe peke yake. Ni suala la kiutendaji, pamoja na kwamba wadaiwa wako wengi, tumeamua kuanza na Mbowe.
“Tumefuata taratibu zote kumwondosha mpangaji wetu. Alishapewa taarifa na sisi kama taasisi ya umma, tuliendelea kumvumilia kwa muda mrefu lakini leo tumefika mwisho,” amesema Mwasenga.

Joshua Mwaituka, Mkurugenzi wa Kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers inayosimamia shughuli ya uondoshaji vifaa katika nyumba hiyo amesema, vifaa vyote vilivyondolewa vitahifadhiwa na kampuni hiyo mpaka hapo deni hilo litakapolipwa

Rais Dkt JOHN MAGUFULI aipongeza JWTZ kwa kutimizia Miaka 52



Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania  Jeneral Davis Mwamunyange mara baada ya kuzungumza katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania  katika kikosi cha Usafirishaji wa anga (Air Wing) Ukonga jijini Dar es Salaam.

SHULE NNE ZA WILAYANI GEITA ZAPIGWA “TAFU” YA MADAWATI NA TIGO FIESTA

 Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga (kushoto)akipokea moja kati ya madawati 185 yenye thamani ya shillingi milioni 31 jana, toka kwa Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande ikiwa ni mpango wa kampuni ya simu za mkononi Tigo kutoa madawati kupitia kauli mbiu “ Dawati kwa kila mwanafunzi ni msingi wa elimu bora fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo imooo”

Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga(katikati)  akiwa ameketi kwenye dawati mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Wengine pichani kulia ni Meneja wa Tigo kanda ya ziwa, Edgar Mapande na Afisa elimu mkoa wa Geita, Catheline Mashala.

Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga akiwa ameketi na wanafunzi wa shule ya msingi Mwatulole mara baada ya kukabidhiwa madawati 185 toka kampuni ya simu za mkononi Tigo hafla iliyofanyika shule ya msingi Mwatulole jana mkoani humo, Pembeni mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi.

TPSF yatoa wafunzo kwa wajasiriamali mkoani Geita

Katibu Tawala wa wilaya ya Geita Thomas Dimme akifungua semina ya wajasiriamali ya taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation iliyofanyika wilayani humo
Mkuu wa kitengo cha wajasiriamali kutoka kutoka mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha (FSDT) akiongea wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mwandamizi kutoka ofisi ya RAS ya Geita akiongea wakati wa mafunzo hayo.

USAJILI: FIFA YALETA WARAKA MPYA


Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limesambaza waraka mpya kwa wanachama wake, likiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ukisema mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

MAKOCHA KILIMANJARO QUEENS WATAJWA


Shirikisho la Mpira Miguu Tanzania (TFF) limemteua Sebastian Nkoma kuwa Kocha Mkuu wa timu ya soka taifa ya wanawake wa Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens ambayo kwa mara ya kwanza inakwenda kushiriki mashindano ya kuwania Kombe la Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika kwa siku tisa kuanzia Septemba 11, 2016 jijini Jinja, Uganda.

Uteuzi huo wa Nkoma unakwenda sambamba na wasaidizi wake, ambao ni Hilda Masanche na Edna Lema wakati Meneja wa timu hiyo, Furaha Francis. Mtunza vifaa ni Esther Chabruma maarufu kwa jina la Lunyamila.

YONDAN ABAKI, STARS IKIIFUATA NIGERIA

Sentahafu wa Young Africans, Kelvin Yondani si miongoni mwa wachezaji 18 walioondoka leo Septemba mosi, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).
Taarifa ambazo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipata ni kwamba Yondani ana matatizo ya kifamilia ambako hajayaweka sawa hadi timu hiyo inaondoka kwenda Nigeria na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa hajajaza nafasi hiyo.