Monday, September 5, 2016

BENKI YA MAENDELEO YADHAMINI SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH JIJINI DAR ES SALAAM


Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Benki ya Maendeleo, Peter Tarimo akisaini mkataba wa udhamini wa shindano la Gospel Star Search (katikati) huku meneja wa Mrado huo wa GSS, Samwel Sasali (kushoto) akishudia tukio hilo lililofanyika leo hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Siku Ya Leo Kamati Ya Gospel Star Search na Kampuni 2.....Maendeleo Bank na Grace Product Wametiliana Mkataba wa Udhamini wa Gospel Star Search 2016. Pichani tukio likifanyika Regency Hotel. Milango ipo wa Wadhamini wengine Pia Makampuni na watu Wa Mavazi Mnakaribishwa. Meza kuu. Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu siu ya leo, katika project hii kubwa inayoendelea ya Gospel star search. 

MBEYA CITY FC WAANZA KUJIANDAA KUIVAA AZAM FC

BAADA ya safari ndefu katika mikoa ya kanda ya ziwa, kikosi cha Mbeya City Fc tayari kimewasili jijini Mbeya kujiwinda na mchezo ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.

Muda mfupi  uliopita meneja wa kikosi hiki Geoffrey Katepa amesema kuwa Mwalimu Kinnah Phiri ameamua kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni wataingia  kwenye uwanja wa Sokoine  kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo wa jumamosi.

TAARIFA MPYA KUTOKA CUF MCHANA HUU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpvC2ANFXkOYMfRUkNVnexxmNzZP3DjAoYWvU7Vs8oPebhBdTOwOcADeHDsKujeD6ay0UyWAnJ16OpnMLQXLN0h5k173s_njm6HVojEm23Nxs9UN-x370hA6GA6UB83Eerbygt44yNe5o/s640/SAM_5072.JPGTAARIFA ZA UPOTOSHWAJI ZINAZOTOLEWA NA BAADHI YA WANACHAMA WALIOPELEKEA MALALAMIKO YAO KWA MSAJILI
WA VYAMA VYA SIASA NCHINI

BREAKING NEWZZ--TETESI ZA LIPUMBA KUHUSISHWA KUJIUNGA ACT WAZALENDO ,SOMA KINACHOENDELEA HAPA

Habari ambazo zimeanza kuenea mitandaoni kuanzia asubuhi ya jumatatu ya leo ni kuhusu Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF Pro Ibrahim Lipumba akihusishwa kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO.
 
Habari hizo zimechagizwa zaidi na Baadhi ya maafisa wa ACT WAZALENDO kutumia mitandao ya kijamii kumnadi kwa kasi Mwenyekiti huyo wa zamani wa CUF aliyejiondoa mwenyewe.
Moja ya maafisa wa kitengo cha mawasiliano wa ACT WAZALENDO ameonekana akitumia mitandao kutuma baadhi ya post za kumuonyesha LIPUMBA akiwa na ZITTO huku akiandika maneno ambayo yamekuwa yakiibua midadala kwa watanzania.

Habari nyingine ni kuhusu Kikao cha ndani acha ACT ambacho kimeanza leo kinachofanyika kwa usiri mkubwa huku Kiongozi Mkuu wa ACT WAZALENDO akiwaahidi wanahabari kuwa Taarifa rasmi juu ya kikao hicho itatolewa Muda ukifika.

ZITTO KABWE amekanusha hakuna mwanachama mpya anayejiunga na chama hicho na wala hakuna ajenda kama hiyo inayojadiliwa ndani ya kikao hicho.
2/2 hatuna mjadala kuhusu wanachama wapya.Mkumbuke tu hao wanaoeneza tuna wanachama wapya ndio hao hao walisema hivyo hivyo 2015. Ikawaje?

Labda kuna kikao kingine kujadili Hilo. Sio hiki nilichomo Mimi sasa hivi 
Kikao cha Kamati kuu ya Chama kinaendelea. Narudia - hakuna ajenda ya kumpokea Kiongozi yeyote wa chama kingine
Wataalam wa siasa wanasema ni muda wa kusubiri na kuona Je nini Kitajiri na kujua Ukweli na uongo wa jambo hili

TIGO FIESTA YAACHA HISTORIA KWA WAKAZI WA SHINYANGA

Benpol na Jux wakiimba kwa pamoja wimbo wa NAKUCHANA katika jukwaa la Tigo Fiesta viwanja vya Kambarage Mjini Shinyanga
Chemical akionesha umahiri wake na kuburudisha umati wa wakazi wa Shinyanga waliohudhuria Tamasha la Tigo Fiesta mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Umati wa wakazi wa Shinyanga wakitoa SHANGWE ya IMOOOO katika Tamasha la Tigo Fiesta liliofanyika katika viwanja ya Kambarage mwishoni wa wiki iliyopita
Jay Moe akiwarusha wakazi wa Shinyanga katika Tamasha la Tigo Fiesta mwishoni wa wiki hii
Billnas na Linah wakiimba kwa pamoja katika jukwaaa la Tigo Fiesta

Heineken in Partnership with Samaki Samaki Unveil East Africa’s First Bucket Lounge

Country Manager for Heineken Tanzania, Michael Mbungu cuts the ribbon to open the Heineken Bucket Lounge at Samaki Samaki Masaki. Looking on second right is Heineken East Africa General Manager Uche Unigwe and 3rd left is Samaki Samaki Owner Carlos Bastos.
Heineken in partnership with Premium outlet Samaki Samaki have unveiled a brand new state-of-the-art consumer experience aimed at engaging beer consumers in Dar es Salaam City.

Located in Masaki, Msasani Peninsula, the Iconic Heineken Bucket Lounge, which is also first of its kind in the East African region, is open to all consumers. The space features an interactive and innovative live viewing experience for sports enthusiasts which includes a custom designed setting allowing football fans to engage, and get a first-hand live viewing of all exciting football matches around the globe.

“Samaki Samaki is one of the best nightlife outlets in Tanzania &  a passion point for our Heineken consumers and we are very proud and excited to support Samaki Samaki in its cool milestones,” shared Michael Mbungu, Country Manager, Heineken Tanzania. “This year, we enhanced our presence at the outlet by going big on interior design and transforming a simple space into an innovative, digitally-infused consumer offering with the chance to engage in the iconic Heineken Experience.”

“It is a space designed as a tribute to Heineken, from the background pictures on walls, the roof uniquely boasts of 5,000 empty green bottles. For the sitting & tables, designers borrowed a leaf from ‘Vijiwe vya uswahilini’ with an urban twist specially designed to bring out conversations and ensure patrons are engaged,” says Samaki Samaki Owner Carlo Bastos.
Heineken East Africa General Manager Uche Unigwe (second right) with Samaki Samaki Owner Carlos Bastos (right) and Country Manager for Heineken Tanzania, Michael Mbungu at the unveiling  Heineken Bucket Lounge in Masaki. The Lounge is first of its kind in the East African region
The space is fully-equipped with complementary free WiFi from 4G TIGO, charging stations and seats a maximum of 40 persons.
This space is made to bring people, friends, closer and is uniquely different from the rest and allows patrons to watch all football matches comfortably with 5 big screen Tvs, while enjoying cold Heinekens. 
 
Nowadays, a lot of people like to drink by buckets....so this space is special for them...in that people can drink only buckets. We have buckets of everything...whisky, gin, beer. It also targets corporates or individuals that want to do a party, birthday, or corporate meetings,” he expounded.

Sunday, September 4, 2016

STARTIMES KUONYESHA MICHUANO YA ULAYA KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018




Na Dotto Mwaibale

MBEYA CITY IMERUDI MAHALA PAKE,YAIADHIBU MBAO FC GOLI 4-1



IMG- Copy 11Licha ya kucheza kwenye uwanja wa  nyumbani, Mbao  Fc ya Mwanza  imejikuta  ikishindwa  kuhimili  vishindo vya Mbeya City Fc na kukubali kufungwa  mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara  uliochezwa  leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba  jijini hapa.
Kwenye Mchezo huo  ulioanza kwa kasi  timu zote zikishambuliana kwa zamu, wenyeji walikuwa wa kwanza kulifikia lango la City  baada ya Vicent Philipo kufanikiwa kumtoka Haruna Shamte aliyekuwa anacheza beki ya kulia  lakini mpira wa krosi wa mchezaji huyo wa Mbao  uliishia  mikononi mwa kipa Owen Chaima.
City ilijibu shambulizi kwenye dakika ya 20 kupitia Ayoub Semtawa  aliyefanikiwa  kuwatoka walinzi wa Mbao Fc lakini mpira aliompenyezea Omary Ramadhani uliokolewa na walinzi wa timu hiyo mwenyeji kabla  ya  Raphael Daud  kufanikiwa kuandika bao la kwanza  baada ya kuunganisha  mpira  ulikuwa umepigwa na Ayoub Semtawa kwenye dakika ya 28, bao lililodumu kwa dakika 10  baada ya Vicent Philipo kuswazisha  dakika ya  38 na kumaliza kipindi cha kwanza timu zote zikiwa na bao 1-1.
Kipindi cha pili Kocha Kinnah Phiri alifanya mabadiliko  ya kumtoa alifanya mabadiliko ya kumtoa  Ayoub Semtawa na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi  mabadiliko ambayo  yaliongeza  uhai kweny safu ya ushambuliaji kwani  dakika chache baadae Omary  Ramadhani aliiandika  bao la pili, bao lilofuataiwa na mabao mengine mawili kutoka kwa Ramadhani Chombo na Raphael Daud waliohitimisha dakika 90  ubao ukisomeka  mabao 4 kwa City na 1 kwa Mbao Fc.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa City  Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia  aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizui kwa kufuata Maelekezo na hatimaye  kuibuka na ushindi  huo mnono.
“Vijana wangu wamecheza  vizuri,  wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana  kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita,  tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha  kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, alisema.
Dondoo za mchezo,mahojiano ya Kinnah Phiri yapo hapa : http://mbeyacityfc.com/event/mbao-fc-vs-mbeya-city/
City  itaondoka Mwanza  alfajiri ya kesho kuelekea jijini Mbeya tayari kwa matayarisho ya mchezo dhidi ya Azam Fc  uliopangwa  kuchezwa  tarehe 10 mwezi huu kwenye uwanja wa Sokoine.
IMG-20160903-WA0027Haruna Shamte(katikati) Rajab Zahir (kushoto) wakishangilia bao la pili lililofungwa na Omary Ramadhani (Kulia)

Saturday, September 3, 2016

MBOWE AFUNGUKA HUJUMA ALIZOFANYIWA NA NHC "SIASA ZINATUMIKA KUNIONEA"


Freeman Mbowe akana kudaiwa kiasi chochote na NHC akisema katika jengo hilo yeye si mpangaji bali ni mmiliki mwenza wa NHC.

Alisema anamiliki jengo hilo kwa asilimia 75 tangu mwaka 1997 na kinachofanywa na shirika hilo la umma kinasimamiwa na viongozi wa dola kwa kuwa yeye ni mpinzani.
“Mimi sidaiwi na NHC na madai yanayofanyika hayapo kisheria bali ni uharibifu wa makusudi unaolenga kunikomoa ambao unatokana na msimamo wangu kisiasa” alisema Mbowe.
Alisema kuzongwazongwa huko ni kwa kuwa yeye ni mpinzani na kabla upinzani haujawa mkubwa alikuwa hafanyiwi hivyo.
Kama ni kudaiwa, Serikali ina madeni, wafanyabiashara wana madeni lakini hawajafanyiwa kama anachofanyiwa Mbowe. Kwa nini Freemedia iwe ya kwanza kushambuliwa kwa kutoa kompyuta zake nje na kujaribu zake nje na kujaribu kuzikagua kwa ndani zina nini? Mbowe alihoji.

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 235 KWA SHULE ZA MSINGI MKOANI MARA

Meneja wa Tigo  Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi  wilayani Rorya wakati   wa  hafla ya kukabidhi madawati kwa shule hiyo jana. 
Meneja wa  Tigo  kanda ya  ziwa, Edgar Mapande  akiongea na  walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Utegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi  madawati kwa shule  hiyo  jana, Wengine  pichani  kushoto  kwake  ni  mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt.Charles  Mlingwana  Mkuu wa wilaya ya   Rorya, Simon Chacha.

Mkuu wa mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  na  Meneja  wa   Tigo  kanda  ya  ziwa, Edgar Mapande  wakinyanyua mikono   juu   mara  baada  ya  makabidhiano  ya  madawati 135 kwa  wilaya ya Rorya na jumla ya   madawati 235 kwa  mkoa  wa Mara, hafla  iliyofanyika  shule yamsingi  Utegi wilayani  Rorya  jana

Mkuu wa Mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  akipokea  madawati 235 kwa  mkoa   wa Mara toka  kwa  Meneja  wa Tigo kanda ya  ziwa, Edgar Mapande  kwenye hafla  iliyofanyika  shule  ya  msingi   Utegi  wilayani   Rorya    jana

Mkuu  wa  Mkoa  wa Mara Dkt. Charles Mlingwa  akiongea na wazazi,walimu na wanafunzi wa shule ya msingiUtegi wilayani Rorya wakati wa hafla ya kukabidhi  madawati   kwa  shule hiyo  jana. Jumla  ya madawati 235 yalitolewa kwa mkoa huo. Pichani kutoka kushoto Meneja waTigo Mkoa wa Mara, Edwin Kisamo,Meneja wa Tigo kanda ya  ziwa, Edgar Mapande ,Mkuu wa wilaya ya  Rorya, Simon Chacha  na   Mwenyekiti wa  Halmashauri  mka Mara, Albert Machiwa 
Wanafunzi wa  shule  ya   msingi   Utegi   wakiwa  wameketi kwenye madawati waliopewa na kampuni ya simu za mkononi Tigo    jana.

KESI YA SIMBA NA YANGA KUHUSU KESSY YAAHIRISHWA


Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iimeahirisha kikao chake kilichokuwa kikae kesho Jumapili Septemba 4, 2016 kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15, 2016.

SERENGETI KUONDOKA USIKU WA KESHO KWENDA SHELISHELI


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa mara nyingine ametimiza ahadi yake kwa kuipeleka nje ya nchi timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ambako itapiga kambi ya utulivu kabla ya kucheza na Congo-Brazzaville katika mechi ya mkondo wa kwanza kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.

DIANA EDWARD NDIYE LETE RAHA MISS KINONDONI 2016

 Malkia wa Kinondoni 2016 Diana Edward ndiye huyu hapa.
 Lete Raha Miss Kinondoni 2016, Diana Edward (katikati), akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa mshindi Dar es Salaam jana. Kulia ni  mshindi wa pili Regina Ndimbo na kushoto ni mshindi wa tatu, Sia Pius.
 Warembo hao wakiserebuka wakati wakijitambulisha.
 Wadau wakifuatilia kwa karibu shindano hilo. 
 Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika vazi la ubunifu. Kutoka kushoto ni Catherine Liston, Hafsa Mahamoud na Mariana Charles.

 Washiriki hao waliofanikiwa kuingia 10 bora.
 Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora. Kutoka kulia ni Hafsa Mahamoud, Diana Edward ambaye ndiye Miss Kinondoni 2016. Regina Ndimbo, Sia Pius na Jackline Kimambo.
Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.

Mgeni rasmi wa shindano hilo, Gift Msuya (kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano hilo.

 Hapa ni sebene kwa kwenda mbele.
 Wakina mama wakimtuza mwanamuziki Christian Bella wakati akiimba wimbo wa Nani kama mama.

Mgeni rasmi wa shindano hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya (katikati), akikabidhi zawadi.